Rais Magufuli: Huduma za NIDA ziwe kila Wilaya au NIDA watoe hela ya 'guest' kwa Wananchi. Ukiona bei ya mahindi iko juu, kalime yako

Sasa mkurugenzi akienda Morogoro ndio itakuwa nini? Matatizo ya NIDA yanajulikana, rasilimali walizonazo haziendani na mahitaji halisi,kimsingi wamezidiwa.

Wanahitaji, fedha, ofisi,rasilimali watu na vifaa vya kutosha sio mkurugenzi wao kwenda Morogoro! Wanasiasa waache kutafuta cheap popularity. Tufanye kazi,sifa zitakuja tu kama kweli ni za muhimu.

Naona hapo juu kuna watu wanasifia hiyo amri ya kwenda Morogoro,wananchi tujitahidi kupunguza ujinga, upumbavu na ushamba. Tujifunze kuwa critical thinkers, tuache ushabiki wa kitoto na ulimbukeni.
 
Nimesikia Muheshimiwa anasema hawezi kupanga bei ya mahindi, yakipanda yapande huu ni mwaka wa wakulima na wafanyabiashara.

Okay thats well and good free market in the workings, swali linakuja ni wapi soko huria linaishia, mbona kwenye korosho hatukufuata market inavyosema?

Sioni ubaya wa kuchagua njia hii au ile, ila we need consistency.
 
Ndio ubaya wa maamuzi ya mtu mmoja, anachosema yeye ndio hicho kifuatwe.
 
Eti mkirugenzi akae Guest. Huyu akija tu. Kila siku posho yake na malazi sio chini ya laki 6.
 
Rais kavaa kijeshi naona nchi inaenda kijeshi jeshi safi sana
 
We are really in big trouble.

Tatizo la NIDA si Morogoro peke yake, ni nchi nzima. Huyo Mkurugenzi maskini sijui atajigawa vipi. Kila wilaya ina ofisi siku hizi. Kwa nini isitumike hiyo? Hilo la kwanza, la pili, hizo ofisi za NIDA zinapewa fedha za kutosha kufanya kazi hiyo? Jibu ni dhahiri, bajeti yao ni ndogo sana.

Kuhusu biashara ya mazao, naona kuna mkanaganyiko mkubwa zaidi. Ni soko huria au serikali itaendelea kupanga bei kama kwenye korosho na pamba? Itaacha kuwazuia wakulima kuuza nje ya nchi ili wapate bei nzuri?
 
Mheshimiwa Rais napenda kukutaarifu kuwa wanaolalamika ni hao hao wakulima!! Mahindi toka kwa wakulima yalinunuliwa na wafanyabiashara na nafco.Rais wenye kipato cha chini wanaumia sana na bei!
Nchi yangu Tanzania Rais,waziri mkuu,waziri wa kilimo,naibuwaziri.............................
 
Rais Magufuli amesema serikali haiwezi kuwapangia wakulima wa mahindi bei ya kuuza mazao yao kwa sababu haikuwasaidia wakati wanalima.

Rais Magufuli amesisitiza kuwa wakati wa serikali kuwapangia wakulima bei za mazao yao umepita na hizi ni zama za soko kuamua.

Source Eatv habari!
 
Okk
Sasa kwa uzoefu kidogo uliyonao kwanini vitambulisho vina kuwa shida kutolewa

Ova
Hapana mkuu
Sisi tulikua Ni vibarua tu.
Hatukua na malmlaka ingawa sisi ndio tulikua watendaji
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…