Rais Magufuli: Huduma za NIDA ziwe kila Wilaya au NIDA watoe hela ya 'guest' kwa Wananchi. Ukiona bei ya mahindi iko juu, kalime yako

Mkuu FUSO, tatizo la JF ni moja.

Hata ukiweka ushauri na mawazo mhimu ya kujenga kama haya yako; yanaishia hapahapa, tena yakiwa yamesomwa na watu wachache tu kama akina wakuu Tindo na akina kalamu1. Heri ya mkuu tindo ambaye ni 'stakeholder' mkubwa katika eneo hili, labda anaweza kuendelea kulipigia kelele na kusikika!

Katika hali ya kawaida, mawazo yako haya yangedakwa na kupewa uwanja mkubwa wa kuyajadili kutokana na umhimu yaliyonao.
Hivi JF hawawezi kubuni utaratibu wa kuyafanya mawazo kama haya yapate mjadala mkubwa unaostahili na hata ikiwezekana kuupenyeza kunakohusika?

Haya mawazo yako si katika kilimo tu. Kuna vijana wengi wenye vipaji na uwezo kwenye nyanja nyingi zingine. Wote hawa serikali ingekuwa na utaratibu wa kuwawekea mazingira na kuwawezesha kukuza vipaji vyao na kujiendeleza lingekuwa jambo jema sana

Swala sio matumizi makubwa ya raslimali toka serikalini, kwani hawa vijana wangepewa miongozo na sera zinazosimamia wanayoyafanya na kuyafanya vizuri tungeona mafanikio na mabadiliko haraka sana.

Utaachaje nguvu kazi hii iishie kuuza visoksi na chupi mitaani?
 
Ni nani anataka kupigwa hapa?
Kwa nini serikali inatoa Ruzuku za pembejeo? Kwa nini bei ya kuuza korosho ilipangwa na serikali?
 
Kuna kitu hakiko sawa kwenye maadili yetu kama watanzania.

Humu JF watu atujuani umri wala nafasi kwa ivyo kanuni za heshima hazihusiki kwa vilee hila sio za ustaarabu.

Nimeshangaa sana kuona katika sehemu zote Magu alizosimama na watu alioongea nao ambao wote kawazidi umri ni mkurugenzi wa NIDA tu ndio alieanza na shikamoo; wengine wote mh raisi na kuanza kuropoka shida zao mpaka yule mwanafunzi something is not right; mie kaka yangu na dada zangu walionizidi umri tu nawaamkia kabla sijasema lolote.

Sijui ni malezi ya watu au nini lakini kwa wale ambao walipewa nafasi most of them walitakiwa kuanza na shikamoo.

Hayo ya bei kama push factor ni masoko ya nje just wait it will bite the government eventually in terms of maisha magumu complaints.

Time will tell Tanzanians can’t handle external push factors if relationship between ‘price elasticity’ and the purchasing power of many Tanzanians is considered to be a factor; someone as a to give in.
 
Hao vijana wameingia mjini baada ya kukuta kilimo hakina tija.
 
Bashe umetisha ,naamin niushari wabashe magufuli hilo alishindwa miaka mitatu yote,hivyo mwakan tutashuhudia mengisana
 
Tamko linaloonekana kuwa zuri sana kwa mkulima; lakini tamko ambalo utekelezaji wake ni mgumu kweli kweli!

Ajipange vizuri kuhakikisha kwamba kaziba mianya yote inayoweza kusababisha ufanisi wa tamko kupotea.

Kwa mfano, yupo tayari kuona mfumko wa bei ukipanda mara dufu, kwa vile mahindi mengi yameuzwa nchi za nje, tena mara nyingi kwa njia zisizoliingizia taifa kodi stahiki?
Kama Kenya wanaweza kununua gunia la mahindi ya Tanzania karibu ya mara mbili ya bei inayopatikana hapa, bado atakuwa tayari kuruhusu mpango huo bila ya serikali kuingiza pua yake?
 
Mkuu wengi huwa tuna na uchungu sana na namna nchi inavyokwenda, priorities za watawala hazi-reflect a real life ya mtanzania hasa kijana.

Huwa nikiwaangalia watoto wangu..napata jibu kuwa hawa watoto wakifikia umri wa kujitambua basi wakaishi kwa watu wanaojielewa.

Siwakimbizi hapana ila hizi sera zenu na utaratibu wake wa utekelezaji naona zinawakwepa vijana..zanawaacha pembeni....na watawala kama kawaida ya nchi za kiafrica wanatumia njia nyepesi mno kuwafunga vijana mdomo wasihoji kwamba kesho yao imekaaje..!! Hili ni janga kubwa !!
 
Hao vijana wameingia mjini baada ya kukuta kilimo hakina tija.
Thanks!! So cha msingi anza na hawa vijana kwanza kuhakikisha wanalima kweli kweli, wanazalisha kweli kweli na wewe unawasaidia masoko ya uhakika, hivi kuna kijana atakuja Dar es salaam? Kufanya Nino?. If this is done basi hata waosha magari na nauza soksi, na qatada wa kazi na wahudumu wa bar watakuwa simu kweli.
 
Hapana mkuu amekosea apeleke tena jeshi kwa wakulima wa mahindi wakaongeze ufanisi kama ule uliopatikana kwenye ununuzi wa korosho.
 
Wenyenyumba je? Serikali iliwasaidia kujenga hadi iwapangie kodi ya kupangisha?
 
khakika mwenye shibe hajui mwenye njaq
kwanini asizuie mahindi kuuzwa nje
sisi wananchi tuliomuweka kwenye wadhifa ndo tunataabika
sembe Imepaa mno kg-1 kuuzwa 1400 mpaka na 1500 ni tatizo
na hajawai kuongeza mshahara kwa waganyakazi
akaone huruma
ajue sisi atutengewo bajeti ya kulishwa
 
Safi sana, ngoja tukalime mahindi kwa wingi.Tatizo la watu wa mjini hawataki sisi wakulima tunufaike kabisa mahindi yakipanda kidogo tu kelele nyingi.
Kupanda bei sio hoja, hoja ni kununua hayo mahindi. Sasa mfano watumishi mwaka wa NNE huu hakuna nyongeza za mishahara wakati bei za vyakula ndio hizo zinapanda kila siku.
Jee ni sawa kumwambia muuguzi hospitalini kuwa "kama unaona mahindi yana bei kalime yako"?
Ishara za kushindwa kuongoza ni nyingi sana, kutoka isisubiri hadi nguvu itumike.
 
Hamna lolote kashindwa kustabilise bei ya unga kutokana na yeye kushindwa kununua mahindi na kuweka strategic reserve, huyu bwana ni actor of note, hakuna mkulima anafaidika na hili, mahindi yote yako kwenye kangomba ya mahindi anachemka tuu
 
Tatizo huyu mkuu ameshasema hashauriki hili ni tatizo, mwambieni wanaolia na bei ya mahindi sasa ni hao hao wakulima maana walisha yauza yote kwa mfanyabiashara, na huyo mfanyabiashara ndie anae panga bei kwa sasa..
 
Hivi Kwa mfano, wakulima wote wakiungana wakasema kuanzia Leo mahindi kilo ni sh 4,000/=, Mtanzania ataishi vipi?
Wadau, hii kitu ya ukiona being ipo juu acha kula au nenda na wewe ukalime ya kwako, tusiiangalie Kwa juu juu tu, nadhani ina madhara makubwa Kwa mustakabali Wa Umoja wetu.....
 

Uzembe pia wanao. Wangefanya kazi usiku na mchana km issue yenye uharaka vitambulisho vingepatikana. Msilee majipu. Kwani kitambulisho kinatengenezwaje? Ni mbao inarandwa manually then iandikwe kwa mkono?? NO. Seriousness na commitment haipo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…