KalamuTena
JF-Expert Member
- Jul 7, 2018
- 13,187
- 17,167
Mkuu FUSO, tatizo la JF ni moja.Haitoshi, vijana wamezagaa mjini wanauza soksi. umetoka job unataka kupumzika sehemu unaona kundi la vijana aged 15- 30 wanakuja kundi as if wanakuvamia alaa kumbe wachuuzi...kila mtu na kiroba chake...
Hawa wanatakiwa wawe mashambani wakizalisha....hawa wanatakiwa kuingia ubia na Serikali...Serikali inatoa resources wao ni NGUVU KAZI...umri wao unarihusu...
Hii kauli haitoshi...ondoa hawa vijana mjini wakafanye kazi huko mashambani watajirike...weka utaratibu mzuri wa uzalishaji na masoko... hela ya Dreamliner moja tu unawabadilisha hawa vijana kabisa kabisa..!!
Hata ukiweka ushauri na mawazo mhimu ya kujenga kama haya yako; yanaishia hapahapa, tena yakiwa yamesomwa na watu wachache tu kama akina wakuu Tindo na akina kalamu1. Heri ya mkuu tindo ambaye ni 'stakeholder' mkubwa katika eneo hili, labda anaweza kuendelea kulipigia kelele na kusikika!
Katika hali ya kawaida, mawazo yako haya yangedakwa na kupewa uwanja mkubwa wa kuyajadili kutokana na umhimu yaliyonao.
Hivi JF hawawezi kubuni utaratibu wa kuyafanya mawazo kama haya yapate mjadala mkubwa unaostahili na hata ikiwezekana kuupenyeza kunakohusika?
Haya mawazo yako si katika kilimo tu. Kuna vijana wengi wenye vipaji na uwezo kwenye nyanja nyingi zingine. Wote hawa serikali ingekuwa na utaratibu wa kuwawekea mazingira na kuwawezesha kukuza vipaji vyao na kujiendeleza lingekuwa jambo jema sana
Swala sio matumizi makubwa ya raslimali toka serikalini, kwani hawa vijana wangepewa miongozo na sera zinazosimamia wanayoyafanya na kuyafanya vizuri tungeona mafanikio na mabadiliko haraka sana.
Utaachaje nguvu kazi hii iishie kuuza visoksi na chupi mitaani?