Rais Magufuli huhitaji kujieleza unapomtoa Waziri. Kwa January Makamba jikalie kimya

Zitto angalia usije kumponza January .... Kama kuchemsha kachemsha sana. Hakuna Kiongozi yeyote ambaye angemuacha madarakani kwa kitendo alichokifanya.

Rais ameonyesha ustarabu kwa kuongelea mengine na kuiacha sababu ya msingi ... Labda atakuwa ansubiri awafanyie kazi ndani ya vikao vya chama.
 
Na kinachonishangaza huyu huyu ambaye akiwatumbua Mawaziri wake huwa anatumia muda mwingi Kuwakosoa na Kutuaminisha Makosa ( Mapungufu ) yao hasa ya Kiutendaji ndiyo Yeye hata wakati Siku akiwaapisha aliwasifia sana na kutuaminisha mno Watanzania kuwa ameteua Watu very Competent katika hizo dockets zake.

Naanza sasa kupata wasiwasi kuwa huenda Yeye ndiye akawa tatizo na siyo hao Wateule wake. Kuna tatizo mahala na naungana nawe Mheshimiwa Mbunge katika hili uliloligusia hapa.
 
Ni haki yake ya kikatiba kutoa maoni na anaelezakwa uchungu wake toka moyoni anavyoumizwa na hali halisi ya nchi kwa wakati huu na ndo wabunge wachache wa upinzani wanaokemea kila jambo baya ndani ya bunge kwa wakati huu
Huyo makamba anayemtetea hatujawahi kumsikia hata siku moja angalao kulaani tu kitendo cha Lissu kupigwa risasi sasa ndiyo amekuwa wa maana
 
Zitto umekosea kubeba bango la kukosoa utenguzi na sababu za utenguzi alizotoa magufuli.

Au ndio fisi anavizia mkono wa bin adam!?
 
Huyo ni CCM-tetea tetea asikupe shida, hata kama amesikia atajifanya kutafuta tafsiri yake. Tunawajua wapuuzi wa aina yake. Hata mume wao aliposema fyatueni watoto walikuja na utetezi wa kitoto eti ni utani, lakini baada ya siku chache alipofuta matangazo ya mpango wa uzazi wakaabika.
 
Mchukueni awasaidie kwenye chama chenu,usimpangie rais cha kufanya ,yapo maovu mengi nyuma ya pazia aliofanya January ,na sasa kalipwa,
 
Naona sasa umegeuka na kuwa mtetezi wa CCM, tumeshakudharau
Hapana mkuu, kwenye issue ya Zitto kumchalenji JPM katika asemayo kuhusu January ni kweli kabisa.
Ni jambo baya sana mkuu wa nchi kusingizia mtu kwa vile anajuwa hawezi kubishana naye.
Kwenye mifuko ya plastiki Jpm anataka kujifanya alihusika wakati sio yeye maana imefanikiwa bila usumbufu kwa raia tofauti na operashini zake anazisema zina hitaji MTU kichaa kuzitekeleza.
 
Huyo makamba anayemtetea hatujawahi kumsikia hata siku moja angalao kulaani tu kitendo cha Lissu kupigwa risasi sasa ndiyo amekuwa wa maana
wazungu wanasema No research No Right to speak tusiwe tunapenda kuzungumza ili kupata public sympath na kumbuka m atukio ni mengi na kama majeraha yako kwa watu wengi tu na wala sio Lissu peke yako kama unavyosema, na hata kama Januar ana changamoto zake lakini ni mchapakazi asiye na makekena anapopanga jambo basi utekelezaji wake unakuwa ni rahisi na matokeo hasi yanaonekana( Angalio katazo la mifuko ya Plastic). Unadhani kama sio busara na akili yake huo mshike mshike wake barabarani na sokoni ingekuwaje. Mnyonge mnyngeni ila haki yake mpeni
 
Watu walitegemea JPM leo angeongea mengi sana,bahati nzuri naona washauuri wake walikuwa smart sana ktk hili tangu aingie madarakani,Ameongea short and clear hajaongea wengi walivyotarajia maana hata radio za mbao zilijiunga ikulu leo.

Tangu aingie madarakani,washauri wake wamefanya kazi yao vema sana.
 
Kama ule Upinzani uliokuwepo kabla ya Uchaguzi wa mwaka 2015 ungekuwa sasa, Hizi vurugu za Chama Tawala sasa hvi wangepata Mtikiso mkubwa sana, Ila Ccm wanavurugana ila Upinzani Pia mishavurugwa hapo kabla so impact yenu na kutake advantage of this itakua ndogo sana.
Nakubaliana na wewe safari hii sababu ya Utenguzi tunaijua haitaji kutoa maelezo mengi sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…