Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Huyo makamba anayemtetea hatujawahi kumsikia hata siku moja angalao kulaani tu kitendo cha Lissu kupigwa risasi sasa ndiyo amekuwa wa maana
Zitto na January walisoma wote Kigoma Sekondary ni "mashosti"Mwambie Zitto itapendeza zaidi akikaa kimya, kuliko utumbo huo anaotoa mbele ya watanzania
Ndivyo siasa zilivyo lakini katika hili wapinzani wake kimya tu..!!Zito! sometimes unazingua babu! waache wachomane wao kwa wao!
mh Zitto, January kaondolewa ili kumkomoa baba yake, mzee Yusuph.Rais Magufuli kwenye sababu za kumuondoa January Makamba bora jikalie zako kimya.
Nimekusikia Rais leo ukijaribu kuelezea sababu za kumuondoa Uwaziri Bwana January Makamba. Kwa kweli hukuwa umejiandaa na maelezo ya kuridhisha.
Rais, kwenye suala la mifuko ya plastiki tunajua ukweli kwamba wewe ndiye ulizuia lisiendelee ulipoambiwa kwamba litaua viwanda. Tunajua kwamba January ndiye ametumia miaka mitatu kuwaandaa wenye viwanda vya mifuko ili wabadilishe teknolojia na wasipate hasara. Tunajua kwamba January alifanya vikao vya umma (public hearings) kuanzia Karimjee mwaka 2017 hadi Mwanza mwaka 2018 na kwingineko kushirikisha wananchi kwenye jambo hili. Tunajua kwamba hatukusikia kauli yako kwenye mifuko ya plastiki hadi baada ya suala hili kufanikiwa. Hii sio kawaida yako maana wewe ni very predictable.
Tunajua kwamba mlimtegea Makamba ili afeli halafu mumtimue. Hakufeli. Sasa mnamtimua kwa kukamilisha kazi kwa weledi mkubwa! Mhe Rais wewe ni mkali maelekezo yako yasipotekelezwa. Umemuachaje Waziri miaka minne kwa kutotii maelekezo halafu unamtoa baada ya utekelezaji? Hakuna mwenye akili timamu anayeweza kukubali hoja yako hii dhaifu sana.
Bwana Rais ulikutana na wafanyabiashara kote nchini kutwa nzima. Walitaja kero zao zote, nami nikaziorodhesha. Sikusikia hata mmoja akilalamikia NEMC. Kwasababu gani? Kwasababu January ameibadilisha NEMC. Alitaka kuibadilisha huko nyuma na akavunja bodi na kuondoa menejimenti lakini kwakuwa inasemekana kulikuwa na ndugu zako walioguswa ukaagiza uamuzi ule ubatilishwe. Unadhani Watanzania wamesahau?
Bwana Rais fedha zinazotolewa na wahisani kwenye miradi ya mazingira zinakaguliwa na CAG na hakuna popote palipoonyesha ubadhirifu au upotevu. Kama upo uweke hadharani kama sisi tulivyoweka hadharani ubadhirifu wa TZS 1.5 Trilioni. Wacha wahisani, Serikali yako haijaweka hata senti tano kwenye miradi ya mazingira nchini. Mimi ni Mbunge na ninapitia kila Bajeti ya Serikali na Taarifa za CAG. Hujawahi kutenga fedha za Mazingira. Kwa kifupi, tunajua wewe binafsi sio mpenzi wa mazingira na umesema hivyo mara kadhaa. Hata huyo January mwenyewe “ulimtupa” kwenye mazingira ili apotee lakini ghafla kila Mtanzania leo anaongea mazingira. Hata wewe nawe leo unayaongea.
Bwana Rais hulazimiki kutoa sababu unapomuondoa Waziri. Kwa kutafuta kutoa sababu zisizoshiba leo, umeonyesha kwamba umesikia hisia za Watanzania kuhusu kuondolewa January Makamba. Umeondoa Waziri kipenzi cha Watanzania na Waziri weledi. Tunajua umemfukuza kwasababu nyingine, sio uchapakazi. Watanzania wote tunajua kwamba siku zote alikuwa anatafutiwa sababu tu ya kuondolewa. Ukisema uchapakazi ndio sababu Watanzania tunakushangaa kwasababu hawa mawaziri umewateua wewe lakini tathmini tunafanya sisi Watanzania. Na January Makamba ndiye alikuwa Waziri mbunifu na bora kabisa. Na ataendelea kuwa maarufu miongoni mwa Watanzania. Hakika ana nafasi kwenye uongozi siku sio nyingi sana zijazo. Mabadiliko ni lazima na January naamini atakuwa sehemu ya mabadiliko ili kujenga Tanzania inayojali watu wake na yenye Demokrasia iliyokomaa
Zitto ZR Kabwe
Mbunge Kigoma Mjini
ushawahi kumwamini Jiwe, u esahau ule ujinga wa dhahabu za mwanza na wale askari?Dah aisee sishangai haya maana sio mara ya kwanza Magufuli kusema uongo ....Alishasema alikuta sukari kilo ni 5000 wakati yeye ndiye aliyesababisha sukari kupanda bei.
halihitaji, kidogo kidogo ,awaziri wote kanda ya ziwa,sidhani kama linahitaji tochi jambo hilo kwa Bwana Muheshimiwa January?
Kwa hiyo wewe ndio mpanga mipango ya selikali?Hapana mkuu, kwenye issue ya Zitto kumchalenji JPM katika asemayo kuhusu January ni kweli kabisa.
Ni jambo baya sana mkuu wa nchi kusingizia mtu kwa vile anajuwa hawezi kubishana naye.
Kwenye mifuko ya plastiki Jpm anataka kujifanya alihusika wakati sio yeye maana imefanikiwa bila usumbufu kwa raia tofauti na operashini zake anazisema zina hitaji MTU kichaa kuzitekeleza.
Huna masikioSijamsikia popote Rais Magufuli akitaja sababu za kumtumbua January. Ni kama vile unamlisha maneno!
Huwezi kumsikia wewe si kiziwi? Labda ungekuwa bubu kidogo ungesikia.Sijamsikia popote Rais Magufuli akitaja sababu za kumtumbua January. Ni kama vile unamlisha maneno!
Sii yawekwe wazi! Mbona tumaneno maneno kama kitchen party?
Kwani angemtengua na akanyamaza angeulizwa na nani?
Au angesema namtengua kwa sababu wa waraka wa baba yake kuuliza kuhusu mwanangu Musiba kuna mtu angelalama?
Kisichofaa ni UONGO UONGO maana ni kudhalilisha kiti
Lioneni hili nalo! Kanywe supu kwanza uondoe hangover ndio utaelewa.Kwa hiyo wewe ndio mpanga mipango ya selikali?
Mbona mnatia aibu sana? Alafu kwanini Zitto kachukia sana kuondoka kwa Makamba?
Hii ni kwasababu kwa kawaida kiziwi huwa hasikiiSijamsikia popote Rais Magufuli akitaja sababu za kumtumbua January. Ni kama vile unamlisha maneno!
Tatizo huyo mkubwa mwenyewe unayemtetea hana staha,anadanganyaje vijana mchana kweupe?aseme ukweli isitoshe hata angekaa kimya hakuna ambaye angemuuliza kuliko kuelezea sababu ambazo ni mwendawazimu pekee ndiye atakubaliana nazo.Sijafurahishwa na ukosefu wa staha kwa Rais wa nchi yetu Tanzania. Nakushauri uwe na staha kwa Rais wetu hata kama amefanya yasiyopendeza utashi wako wewe binafsi. Nakuzungumzia wewe mleta mada.
===
Vitu vidogo vidogo hivi vinasababisha baadhi ya vinaja kukosa kuaminiwa kupewa madaraka makubwa. Tuulinde ujana wetu na kuaminiwa kwetu kwanza kwa kuwa na staha kwa wakubwa na mamlaka zilizopo.
Sijamsikia popote Rais Magufuli akitaja sababu za kumtumbua January. Ni kama vile unamlisha maneno!