Rais Magufuli huhitaji kujieleza unapomtoa Waziri. Kwa January Makamba jikalie kimya

Rais Magufuli huhitaji kujieleza unapomtoa Waziri. Kwa January Makamba jikalie kimya

Mkuu tuseme ukweli tu, umewahi kumsikia hata siku moja makamba analaani kupigwa risasi Lissu, kuteswa wapinzani, kutekwa wapinzani, kuuawa wapinzani n.k. eti leo kichwa cha panzi kasahau kila kitu anawatetea maccm
Kwani Chadema mko chini ya wizara ya mazingira?!
 
Tafadhali sana ndugu zito,
Usije ukamshauri bwana January kujiunga na upinzani.

Tunataka abakie huko huko ccm.

Januari usije ukaenda chama chochote ch upinzani.

Usije ukathubutu.

Baki hapo hapo.
Chezeni karata zenu vizuri.
Hata akihama hawezi kugombea nafasi yeyote we unafikiri kwanini ameondolewa saivi na si kipindi cha nyuma
Mda ushayoyoma na sheria ya vyama vya siasa inawazoom tu
 
Wazee wa bao la mkono wacha wakipate na wenyewe, huyu si nasikia aliiiii kuwa na timu ya vijana wa IT kutuibia kura zetu??Sina hakika sanaa, ila tulisikia hivyo, kwa hiyo bwana acha waonje machungu uovu haujawahi kumuacha mtu salama, kura zetu walizotuibia ndio matunda wanayopata,Lisu alisema wakimaliza upinzani watawarudia nyie,acha wavurugane hadi akili ziwakae vyema
 
Sijamsikia popote Rais Magufuli akitaja sababu za kumtumbua January. Ni kama vile unamlisha maneno!

Magufuli abainisha sababu ya kumng’oa Makamba

MONDAY JULY 22 2019

Kwa ufupi

Rais wa Tanzania, John Magufuli ametaja mambo matatu yaliyokuwa changamoto katika Wizara ya Nchi katika ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira na Muungano) akisema hayakutekelezwa kwa ufanisi kwa miaka minne ya utawala wake.
ADVERTISEMENT

By Elias Msuya, Mwananchi emsuya@mwananchi.co.tz
Dar es Salaam. Rais wa Tanzania, John Magufuli ametaja changamoto zilizochukua muda mrefu kutekelezwa katika Wizara ya Nchi katika Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira na Muungano) ikiwa ni siku moja baada ya kumng’oa aliyekuwa Waziri January Makamba aliyeitumikia wizara hiyo kwa miaka minne mfululizo.
Miongoni mwa sifa alizojizolea Makamba katika uongozi wake ni kutekeleza katazo la mifuko ya plastiki tangu Juni 1 mwaka 2019.
Hata hivyo, akizungumza wakati wa kuwaapisha leo Jumatatu Julai 22,2019 George Simbachawene (Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano na Mazingira) na Hussein Bashe (Naibu Waziri-Kilimo), Rais Magufuli amesema katazo hilo lilicheleweshwa.
“Nakumbuka kwenye suala la plastiki lilichukua muda mrefu, mpaka miaka minne. Nikasaini halikutekelezwa, Makamu wa Rais (Samia Suluhu Hassan) akazungumza, halikutekelezwa, Waziri Mkuu (Kassim Majaliwa) akaenda kuzungumza bungeni halikutekelezwa. Mpaka hapa mwishoni nilipotoa amri ya lazima ndipo likaanza kutekelezwa,” amesema Rais Magufuli.
Ametaja pia suala fedha za miradi ya mazingira akisema kuna fedha zinazotolewa na wafadhili lakini hazitumiki vizuri.
Bahati nzuri utajifunza (Simbachawene) kwa Makamu wa Rais, ambaye ni msimamizi mzuri.
 
Hapana mkuu, kwenye issue ya Zitto kumchalenji JPM katika asemayo kuhusu January ni kweli kabisa.
Ni jambo baya sana mkuu wa nchi kusingizia mtu kwa vile anajuwa hawezi kubishana naye.
Kwenye mifuko ya plastiki Jpm anataka kujifanya alihusika wakati sio yeye maana imefanikiwa bila usumbufu kwa raia tofauti na operashini zake anazisema zina hitaji MTU kichaa kuzitekeleza.
Bora akae kimya na wewe ukae kimya kwa sababu tutagombana, lini ulimuona au kumsikia makamba analaani manyanyaso zidi ya upinzani, kupigwa risasi, kufutwa ubunge, kuuawa wapinzani n.k. sasa yeye Zitto anajifanya kimbelembele kuwatetea maccm
 
Mchukueni awasaidie kwenye chama chenu,usimpangie rais cha kufanya ,yapo maovu mengi nyuma ya pazia aliofanya January ,na sasa kalipwa,
Sii yawekwe wazi! Mbona tumaneno maneno kama kitchen party?
Kwani angemtengua na akanyamaza angeulizwa na nani?
Au angesema namtengua kwa sababu wa waraka wa baba yake kuuliza kuhusu mwanangu Musiba kuna mtu angelalama?
Kisichofaa ni UONGO UONGO maana ni kudhalilisha kiti
 
Magufuli abainisha sababu ya kumng’oa Makamba

MONDAY JULY 22 2019

Kwa ufupi

Rais wa Tanzania, John Magufuli ametaja mambo matatu yaliyokuwa changamoto katika Wizara ya Nchi katika ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira na Muungano) akisema hayakutekelezwa kwa ufanisi kwa miaka minne ya utawala wake.
ADVERTISEMENT

By Elias Msuya, Mwananchi emsuya@mwananchi.co.tz
Dar es Salaam. Rais wa Tanzania, John Magufuli ametaja changamoto zilizochukua muda mrefu kutekelezwa katika Wizara ya Nchi katika Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira na Muungano) ikiwa ni siku moja baada ya kumng’oa aliyekuwa Waziri January Makamba aliyeitumikia wizara hiyo kwa miaka minne mfululizo.
Miongoni mwa sifa alizojizolea Makamba katika uongozi wake ni kutekeleza katazo la mifuko ya plastiki tangu Juni 1 mwaka 2019.
Hata hivyo, akizungumza wakati wa kuwaapisha leo Jumatatu Julai 22,2019 George Simbachawene (Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano na Mazingira) na Hussein Bashe (Naibu Waziri-Kilimo), Rais Magufuli amesema katazo hilo lilicheleweshwa.
“Nakumbuka kwenye suala la plastiki lilichukua muda mrefu, mpaka miaka minne. Nikasaini halikutekelezwa, Makamu wa Rais (Samia Suluhu Hassan) akazungumza, halikutekelezwa, Waziri Mkuu (Kassim Majaliwa) akaenda kuzungumza bungeni halikutekelezwa. Mpaka hapa mwishoni nilipotoa amri ya lazima ndipo likaanza kutekelezwa,” amesema Rais Magufuli.
Ametaja pia suala fedha za miradi ya mazingira akisema kuna fedha zinazotolewa na wafadhili lakini hazitumiki vizuri.
Bahati nzuri utajifunza (Simbachawene) kwa Makamu wa Rais, ambaye ni msimamizi mzuri.
Kwahiyo amesema amemtumbua kwa sababu hizo?
 
Wanaomuamini na kumkubali bwana yule ni wajinga wa kiwango cha SGR!!
 
Magufuli anachukua credit za kupiga marufuku plastic kama Rais lakini Makamba anachukua Credit zaidi kwa kuwa mbunifu na kulifanya hilo zoezi kwa umakini mkubwa

Ni kama yeye Magufuli tulivyokuwa tukimsifu kujenga barabara japo nyuma yake alikuwepo raisi wa wakati huo.

Halafu kama hela za wahisani zimeliwa si anapaswa apeleke watu mahakamani, maneno matupu yanatusadia nini sisi?
 
Kifupi huyo Jamaa anataka asifiwe yeye tu.... Hakubali mtu mwengine asifiwe
Hapana mkuu, kwenye issue ya Zitto kumchalenji JPM katika asemayo kuhusu January ni kweli kabisa.
Ni jambo baya sana mkuu wa nchi kusingizia mtu kwa vile anajuwa hawezi kubishana naye.
Kwenye mifuko ya plastiki Jpm anataka kujifanya alihusika wakati sio yeye maana imefanikiwa bila usumbufu kwa raia tofauti na operashini zake anazisema zina hitaji MTU kichaa kuzitekeleza.
 
Sijafurahishwa na ukosefu wa staha kwa Rais wa nchi yetu Tanzania. Nakushauri uwe na staha kwa Rais wetu hata kama amefanya yasiyopendeza utashi wako wewe binafsi. Nakuzungumzia wewe mleta mada.
===
Vitu vidogo vidogo hivi vinasababisha baadhi ya vinaja kukosa kuaminiwa kupewa madaraka makubwa. Tuulinde ujana wetu na kuaminiwa kwetu kwanza kwa kuwa na staha kwa wakubwa na mamlaka zilizopo.
 
Ulikuwa husikilizi au hukuelewa
Kasema kulikua na miradi hewa ya kupanda mikoko, matumizi mabaya ta fedha za wafadhili, na marufuku ya mifuko ya plastiki aliichelewesha kwa miaka 4 na hata lilipotekelezwa juzi ni yeye alimlazimisha
Sijui kama ni kweli au ni kumpaka matope jamaa, Makamba nae katia ngumu, kagima kwenda Ikulu leo kama watumbuliwa wengine wanavyohudhuria
Mkuu nimesikiliza vizuri na yote uliyoyaandika nimesikia ila sijasikia akisema kwamba kutokana na sababu hizo ndio kamtumbua January son of Makamba!
 
Mkuu mimi mwenyewe siyo ccm kabisa ila nilimwuunga mkono January kwenye issue ya kukomesha matumizi ya Plastic kwa hiyo.
Tunachozungumza hapa Zitto kama mpinzani aliwahi kumuona makamba anapinga kutekwa wananchi, kulaani kitendo cha kupigwa risasi Lissu, kulaani mateso kwa wapinzani, n.k. mbona yeye anajifanya kimbelembele kuwatetea maccm
 
Back
Top Bottom