January ni mchapakazi?!
Utakuwa huna masikio weweSijamsikia popote Rais Magufuli akitaja sababu za kumtumbua January. Ni kama vile unamlisha maneno!
Just because you didn't hear doesn't mean he didn't say it. Labda umejaza pamba masikioni. But again, LISTENING is a skill na si kila mtu anayo.Sijamsikia popote Rais Magufuli akitaja sababu za kumtumbua January. Ni kama vile unamlisha maneno!
Ulikuwa husikilizi au hukuelewa
Kasema kwenye wizara yake kulikua na miradi hewa ya kupanda mikoko, matumizi mabaya ta fedha za wafadhili, na marufuku ya mifuko ya plastiki aliichelewesha kwa miaka 4 na hata lilipotekelezwa juzi ni yeye alimlazimisha
Sijui kama ni kweli au ni kumpaka matope jamaa, Makamba nae katia ngumu, kagoma kwenda Ikulu leo kama watumbuliwa wengine wanavyohudhuria
Zito! sometimes unazingua babu! waache wachomane wao kwa wao!
January ni mchapakazi?!
Tayari Zitto ameshaipost mwenyewe humuRais Magufuli kwenye sababu za kumuondoa January Makamba bora jikalie zako kimya.
Nimekusikia Rais leo ukijaribu kuelezea sababu za kumuondoa Uwaziri Bwana January Makamba. Kwa kweli hukuwa umejiandaa na maelezo ya kuridhisha.
Rais, kwenye suala la mifuko ya plastiki tunajua ukweli kwamba wewe ndiye ulizuia lisiendelee ulipoambiwa kwamba litaua viwanda. Tunajua kwamba January ndiye ametumia miaka mitatu kuwaandaa wenye viwanda vya mifuko ili wabadilishe teknolojia na wasipate hasara. Tunajua kwamba January alifanya vikao vya umma (public hearings) kuanzia Karimjee mwaka 2017 hadi Mwanza mwaka 2018 na kwingineko kushirikisha wananchi kwenye jambo hili. Tunajua kwamba hatukusikia kauli yako kwenye mifuko ya plastiki hadi baada ya suala hili kufanikiwa. Hii sio kawaida yako maana wewe ni very predictable.
Tunajua kwamba mlimtegea Makamba ili afeli halafu mumtimue. Hakufeli. Sasa mnamtimua kwa kukamilisha kazi kwa weledi mkubwa! Mhe Rais wewe ni mkali maelekezo yako yasipotekelezwa. Umemuachaje Waziri miaka minne kwa kutotii maelekezo halafu unamtoa baada ya utekelezaji? Hakuna mwenye akili timamu anayeweza kukubali hoja yako hii dhaifu sana.
Bwana Rais ulikutana na wafanyabiashara kote nchini kutwa nzima. Walitaja kero zao zote, nami nikaziorodhesha. Sikusikia hata mmoja akilalamikia NEMC. Kwasababu gani? Kwasababu January ameibadilisha NEMC. Alitaka kuibadilisha huko nyuma na akavunja bodi na kuondoa menejimenti lakini kwakuwa inasemekana kulikuwa na ndugu zako walioguswa ukaagiza uamuzi ule ubatilishwe. Unadhani Watanzania wamesahau?
Bwana Rais fedha zinazotolewa na wahisani kwenye miradi ya mazingira zinakaguliwa na CAG na hakuna popote palipoonyesha ubadhirifu au upotevu. Kama upo uweke hadharani kama sisi tulivyoweka hadharani ubadhirifu wa TZS 1.5 Trilioni. Wacha wahisani, Serikali yako haijaweka hata senti tano kwenye miradi ya mazingira nchini. Mimi ni Mbunge na ninapitia kila Bajeti ya Serikali na Taarifa za CAG. Hujawahi kutenga fedha za Mazingira. Kwa kifupi, tunajua wewe binafsi sio mpenzi wa mazingira na umesema hivyo mara kadhaa. Hata huyo January mwenyewe “ulimtupa” kwenye mazingira ili apotee lakini ghafla kila Mtanzania leo anaongea mazingira. Hata wewe nawe leo unayaongea.
Bwana Rais hulazimiki kutoa sababu unapomuondoa Waziri. Kwa kutafuta kutoa sababu zisizoshiba leo, umeonyesha kwamba umesikia hisia za Watanzania kuhusu kuondolewa January Makamba. Umeondoa Waziri kipenzi cha Watanzania na Waziri weledi. Tunajua umemfukuza kwasababu nyingine, sio uchapakazi. Watanzania wote tunajua kwamba siku zote alikuwa anatafutiwa sababu tu ya kuondolewa. Ukisema uchapakazi ndio sababu Watanzania tunakushangaa kwasababu hawa mawaziri umewateua wewe lakini tathmini tunafanya sisi Watanzania. Na January Makamba ndiye alikuwa Waziri mbunifu na bora kabisa. Na ataendelea kuwa maarufu miongoni mwa Watanzania. Hakika ana nafasi kwenye uongozi siku sio nyingi sana zijazo. Mabadiliko ni lazima na January naamini atakuwa sehemu ya mabadiliko ili kujenga Tanzania inayojali watu wake na yenye Demokrasia iliyokomaa
Zitto ZR Kabwe
Mbunge Kigoma Mjini
View attachment 1159461
Tafadhali sana ndugu zito,
Usije ukamshauri bwana January kujiunga na upinzani.
Tunataka abakie huko huko ccm.
Januari usije ukaenda chama chochote ch upinzani.
Usije ukathubutu.
Baki hapo hapo.
Chezeni karata zenu vizuri.
Duh aiseeeeeeee....Zitto alimtegemea sana January......muda si mrefu tutayasikia ya NSSF!
Kwani akaee kimyaMwambie Zitto itapendeza zaidi akikaa kimya, kuliko utumbo huo anaotoa mbele ya watanzania
Mkuu hapa ndipo ambapo siasa za tz zinaponichefuaga ndipo Kama taifa tunapofeli.umesoma bandiko au umerespond tittle?
Maendeleo hayana chama na inapotea kiongozi ambaye ni mchapakazi anatuhumiwa pasi na sababu wapenda maendeleo ni lazima wakeme hii haki, na sio Zito tu mbona hata John Heche amezungumzia juu ya kutenguliwa kwa Mh January Makamba, kimbilio la watanzania na wapenda mazingira ya dhati
Amka wewe bado umelala hujamsikia wakati anawaapisha wateule wake?Sijamsikia popote Rais Magufuli akitaja sababu za kumtumbua January. Ni kama vile unamlisha maneno!
Hukufatilia Hotuba!Sijamsikia popote Rais Magufuli akitaja sababu za kumtumbua January. Ni kama vile unamlisha maneno!
Hivi mlitaka raia wote milioni 50 wakemee kupigwa risasi Lissu??? Siwapendi CCM lakini pia sipendi zaidi upumbavu na unafiki wa chadema... yaaani kila tukio LISSU , mazingira Lissu kapigwa risasi , mkiongelea Kilimo Lissu kapigwa Risasi ..asingepigwa Risasi hivi msingekuwa na hoja nyingine!!! Wengine hatuna vyama ila kwa mikumbomikumbo ya Chadema na Upinzani kwa ujumla wao kurukia tu kana ngedere msituni likitoke hili hawaaaa oooh Lissu likitokea lile ooooh Kutekwa ..../ alipigwa Risasi Rais wa Uturuki hadharani mbona maisha yaaendelea??? Kennedy ...., kuweni wabunifu kuendesha chama sio vururuvururu ....hamtakuwa na tofauti na hao CCMHuyo makamba anayemtetea hatujawahi kumsikia hata siku moja angalao kulaani tu kitendo cha Lissu kupigwa risasi sasa ndiyo amekuwa wa maana
Zito! sometimes unazingua babu! waache wachomane wao kwa wao!
mimi nakuambia ndugu yangu, kuwang'oa ccm kwa sasa ni kazi kubwa sana, ccm ya kung'oka ilikuwa ya 2015 ile ya jkMembe baki CCM.
January baki CCM.
Nape baki CCM.
Kinana baki CCM.
Makamba Sr baki CCM.
Mkiwa na vinyongo vyenu endeleeni kubaki huko huko mkichochea kuni mpaka 2020.
LISSU rudi haraka Tanzania wakati ni huu, Mbowe kaa chini na ACT mkubaliane pamoja na Seif na akina Jussa na wazanzibar wote, bara asimame LISSU na visiwani kama kawa Maalim na ACT.. CCM kwa hali waliyonayo kuni zikichochewa wanaanguka mapema sana 2020..