Rais Magufuli huhitaji kujieleza unapomtoa Waziri. Kwa January Makamba jikalie kimya

Rais Magufuli huhitaji kujieleza unapomtoa Waziri. Kwa January Makamba jikalie kimya

Rais Magufuli kwenye sababu za kumuondoa January Makamba bora jikalie zako kimya.
Nimekusikia Rais leo ukijaribu kuelezea sababu za kumuondoa Uwaziri Bwana January Makamba. Kwa kweli hukuwa umejiandaa na maelezo ya kuridhisha.
Rais, kwenye suala la mifuko ya plastiki tunajua ukweli kwamba wewe ndiye ulizuia lisiendelee ulipoambiwa kwamba litaua viwanda. Tunajua kwamba January ndiye ametumia miaka mitatu kuwaandaa wenye viwanda vya mifuko ili wabadilishe teknolojia na wasipate hasara. Tunajua kwamba January alifanya vikao vya umma (public hearings) kuanzia Karimjee mwaka 2017 hadi Mwanza mwaka 2018 na kwingineko kushirikisha wananchi kwenye jambo hili. Tunajua kwamba hatukusikia kauli yako kwenye mifuko ya plastiki hadi baada ya suala hili kufanikiwa. Hii sio kawaida yako maana wewe ni very predictable.
Tunajua kwamba mlimtegea Makamba ili afeli halafu mumtimue. Hakufeli. Sasa mnamtimua kwa kukamilisha kazi kwa weledi mkubwa! Mhe Rais wewe ni mkali maelekezo yako yasipotekelezwa. Umemuachaje Waziri miaka minne kwa kutotii maelekezo halafu unamtoa baada ya utekelezaji? Hakuna mwenye akili timamu anayeweza kukubali hoja yako hii dhaifu sana.
Bwana Rais ulikutana na wafanyabiashara kote nchini kutwa nzima. Walitaja kero zao zote, nami nikaziorodhesha. Sikusikia hata mmoja akilalamikia NEMC. Kwasababu gani? Kwasababu January ameibadilisha NEMC. Alitaka kuibadilisha huko nyuma na akavunja bodi na kuondoa menejimenti lakini kwakuwa inasemekana kulikuwa na ndugu zako walioguswa ukaagiza uamuzi ule ubatilishwe. Unadhani Watanzania wamesahau?
Bwana Rais fedha zinazotolewa na wahisani kwenye miradi ya mazingira zinakaguliwa na CAG na hakuna popote palipoonyesha ubadhirifu au upotevu. Kama upo uweke hadharani kama sisi tulivyoweka hadharani ubadhirifu wa TZS 1.5 Trilioni. Wacha wahisani, Serikali yako haijaweka hata senti tano kwenye miradi ya mazingira nchini. Mimi ni Mbunge na ninapitia kila Bajeti ya Serikali na Taarifa za CAG. Hujawahi kutenga fedha za Mazingira. Kwa kifupi, tunajua wewe binafsi sio mpenzi wa mazingira na umesema hivyo mara kadhaa. Hata huyo January mwenyewe “ulimtupa” kwenye mazingira ili apotee lakini ghafla kila Mtanzania leo anaongea mazingira. Hata wewe nawe leo unayaongea.
Bwana Rais hulazimiki kutoa sababu unapomuondoa Waziri. Kwa kutafuta kutoa sababu zisizoshiba leo, umeonyesha kwamba umesikia hisia za Watanzania kuhusu kuondolewa January Makamba. Umeondoa Waziri kipenzi cha Watanzania na Waziri weledi. Tunajua umemfukuza kwasababu nyingine, sio uchapakazi. Watanzania wote tunajua kwamba siku zote alikuwa anatafutiwa sababu tu ya kuondolewa. Ukisema uchapakazi ndio sababu Watanzania tunakushangaa kwasababu hawa mawaziri umewateua wewe lakini tathmini tunafanya sisi Watanzania. Na January Makamba ndiye alikuwa Waziri mbunifu na bora kabisa. Na ataendelea kuwa maarufu miongoni mwa Watanzania. Hakika ana nafasi kwenye uongozi siku sio nyingi sana zijazo. Mabadiliko ni lazima na January naamini atakuwa sehemu ya mabadiliko ili kujenga Tanzania inayojali watu wake na yenye Demokrasia iliyokomaa
Zitto ZR Kabwe
Mbunge Kigoma Mjini

View attachment 1159461
 
Makamba amejitambua
Ulikuwa husikilizi au hukuelewa
Kasema kwenye wizara yake kulikua na miradi hewa ya kupanda mikoko, matumizi mabaya ta fedha za wafadhili, na marufuku ya mifuko ya plastiki aliichelewesha kwa miaka 4 na hata lilipotekelezwa juzi ni yeye alimlazimisha

Sijui kama ni kweli au ni kumpaka matope jamaa, Makamba nae katia ngumu, kagoma kwenda Ikulu leo kama watumbuliwa wengine wanavyohudhuria
 
Rais Magufuli kwenye sababu za kumuondoa January Makamba bora jikalie zako kimya.
Nimekusikia Rais leo ukijaribu kuelezea sababu za kumuondoa Uwaziri Bwana January Makamba. Kwa kweli hukuwa umejiandaa na maelezo ya kuridhisha.
Rais, kwenye suala la mifuko ya plastiki tunajua ukweli kwamba wewe ndiye ulizuia lisiendelee ulipoambiwa kwamba litaua viwanda. Tunajua kwamba January ndiye ametumia miaka mitatu kuwaandaa wenye viwanda vya mifuko ili wabadilishe teknolojia na wasipate hasara. Tunajua kwamba January alifanya vikao vya umma (public hearings) kuanzia Karimjee mwaka 2017 hadi Mwanza mwaka 2018 na kwingineko kushirikisha wananchi kwenye jambo hili. Tunajua kwamba hatukusikia kauli yako kwenye mifuko ya plastiki hadi baada ya suala hili kufanikiwa. Hii sio kawaida yako maana wewe ni very predictable.
Tunajua kwamba mlimtegea Makamba ili afeli halafu mumtimue. Hakufeli. Sasa mnamtimua kwa kukamilisha kazi kwa weledi mkubwa! Mhe Rais wewe ni mkali maelekezo yako yasipotekelezwa. Umemuachaje Waziri miaka minne kwa kutotii maelekezo halafu unamtoa baada ya utekelezaji? Hakuna mwenye akili timamu anayeweza kukubali hoja yako hii dhaifu sana.
Bwana Rais ulikutana na wafanyabiashara kote nchini kutwa nzima. Walitaja kero zao zote, nami nikaziorodhesha. Sikusikia hata mmoja akilalamikia NEMC. Kwasababu gani? Kwasababu January ameibadilisha NEMC. Alitaka kuibadilisha huko nyuma na akavunja bodi na kuondoa menejimenti lakini kwakuwa inasemekana kulikuwa na ndugu zako walioguswa ukaagiza uamuzi ule ubatilishwe. Unadhani Watanzania wamesahau?
Bwana Rais fedha zinazotolewa na wahisani kwenye miradi ya mazingira zinakaguliwa na CAG na hakuna popote palipoonyesha ubadhirifu au upotevu. Kama upo uweke hadharani kama sisi tulivyoweka hadharani ubadhirifu wa TZS 1.5 Trilioni. Wacha wahisani, Serikali yako haijaweka hata senti tano kwenye miradi ya mazingira nchini. Mimi ni Mbunge na ninapitia kila Bajeti ya Serikali na Taarifa za CAG. Hujawahi kutenga fedha za Mazingira. Kwa kifupi, tunajua wewe binafsi sio mpenzi wa mazingira na umesema hivyo mara kadhaa. Hata huyo January mwenyewe “ulimtupa” kwenye mazingira ili apotee lakini ghafla kila Mtanzania leo anaongea mazingira. Hata wewe nawe leo unayaongea.
Bwana Rais hulazimiki kutoa sababu unapomuondoa Waziri. Kwa kutafuta kutoa sababu zisizoshiba leo, umeonyesha kwamba umesikia hisia za Watanzania kuhusu kuondolewa January Makamba. Umeondoa Waziri kipenzi cha Watanzania na Waziri weledi. Tunajua umemfukuza kwasababu nyingine, sio uchapakazi. Watanzania wote tunajua kwamba siku zote alikuwa anatafutiwa sababu tu ya kuondolewa. Ukisema uchapakazi ndio sababu Watanzania tunakushangaa kwasababu hawa mawaziri umewateua wewe lakini tathmini tunafanya sisi Watanzania. Na January Makamba ndiye alikuwa Waziri mbunifu na bora kabisa. Na ataendelea kuwa maarufu miongoni mwa Watanzania. Hakika ana nafasi kwenye uongozi siku sio nyingi sana zijazo. Mabadiliko ni lazima na January naamini atakuwa sehemu ya mabadiliko ili kujenga Tanzania inayojali watu wake na yenye Demokrasia iliyokomaa
Zitto ZR Kabwe
Mbunge Kigoma Mjini

View attachment 1159461
Tayari Zitto ameshaipost mwenyewe humu
 
Hilo ndiyo ombi la mamilioni ya watanzania abakie huko huko ccm na ikimpendeza naye zchukue fom ya kugombea uprezidaa
Tafadhali sana ndugu zito,
Usije ukamshauri bwana January kujiunga na upinzani.

Tunataka abakie huko huko ccm.

Januari usije ukaenda chama chochote ch upinzani.

Usije ukathubutu.

Baki hapo hapo.
Chezeni karata zenu vizuri.
 
Makamba kaona aibu kwenda Ikulu. The traitor. January shame on you. Halafu Zitto kwani JPM kasema hizo ndo sababu? Alikuwa anaelezea tu madudu yaliyopo kwenye wizara ya mazingira.
 
Zitto alimtegemea sana January......muda si mrefu tutayasikia ya NSSF!
Duh aiseeeeeeee....
Mwambie Zitto itapendeza zaidi akikaa kimya, kuliko utumbo huo anaotoa mbele ya watanzania
Kwani akaee kimya
umesoma bandiko au umerespond tittle?
Mkuu hapa ndipo ambapo siasa za tz zinaponichefuaga ndipo Kama taifa tunapofeli.

Unakuta Jambo zuri/hoja nzuri imeletwa na CCM/Serikali basi vyama upinzani watapinga 100% bila hata kuonyesha mapungufu yaliomo na kusema/kuleta njia/namna mbadala ya kuendelea.
The same tu CCM watapinga hoja na mapendekezo yote/zote za upinzani bila hata kuziangalia kwa undani wake Kama Ni nzuri ama la....

Nchi zilizoendelea US na UK na etc Mara nyingi TU wabunge wanapinga kwa hoja kwa mchanganyiko mfano ishu ya Brexit UK wabunge wengi tu wa chama Cha aliekuwa PM May wakiungana na baadhi wa vyama pinzani walikuwa wapinga mapendekezo yake/serikali, na pia wapinzani wengi tu wakiungana na cha cha May/Serikali kutetea hoja iliyokuwa inapendekezwa kuhusu Brexit. Never this in Tz as kila penda imekamilika kwa asimilia 800..

Siasa zetu zimefikia hatua kwamba kwa mtu aliye nje ya Tz (ulaya,aisa au hata marekani) Kama ikitoketea akawa anapata taarifa za Tz kutoka kwa watu wa vyama vya upinzani tu basi hatahitimisha kuwa TZ NCHI HAIKALIKI,HALI YA UCHUMI NI MBAYA MNO, MAISHA YA TABU/NJAA KILA MAHARI, USALAMA NI MDOGO SAAANA YAANI UWEZI ISHI SIKU IKAPITA(UTATEKWA KULIWA) ETC. na nihivyo hivyo mtu huyu ikiwa taarifa pekee anazopata ni kutoka kwa wafuasi wa Cha kilichopo madarakani/CCM atahitimisha kuwa TZ NI NCHI ILIYOENDELEA SANA KULIKO HATA FRANCE, SWISS OR CANADA, YAANA WANANCHI WOTE WANAPATA HUDUMA ZA AFYA,MAJI,ELIMU BORA KABISA NA KIWANGO CHA JUU, USAFIRI NI BORA SGR,NDEGE, UMEME KILA NYUMBA NI TANGU 1820 HIVI, WATUMISHI WA UMMA WANALIPWA STAHIKI ZAO NA NYOGEZA YA FIDIA IKIBAINIKA UMECHELEWESHEWA, HAKUNA MASIKINI WANAOMBA AU WANAO LALA NJAA, TZ NI DONOR COUNTRY KWA MAJIRANI ZAKE ETC..

tuna safari ndefu.....
Zitto kusema ishu ya makamba anaonekana msaliti what a f**ck
Maendeleo hayana chama na inapotea kiongozi ambaye ni mchapakazi anatuhumiwa pasi na sababu wapenda maendeleo ni lazima wakeme hii haki, na sio Zito tu mbona hata John Heche amezungumzia juu ya kutenguliwa kwa Mh January Makamba, kimbilio la watanzania na wapenda mazingira ya dhati
 
Huyo makamba anayemtetea hatujawahi kumsikia hata siku moja angalao kulaani tu kitendo cha Lissu kupigwa risasi sasa ndiyo amekuwa wa maana
Hivi mlitaka raia wote milioni 50 wakemee kupigwa risasi Lissu??? Siwapendi CCM lakini pia sipendi zaidi upumbavu na unafiki wa chadema... yaaani kila tukio LISSU , mazingira Lissu kapigwa risasi , mkiongelea Kilimo Lissu kapigwa Risasi ..asingepigwa Risasi hivi msingekuwa na hoja nyingine!!! Wengine hatuna vyama ila kwa mikumbomikumbo ya Chadema na Upinzani kwa ujumla wao kurukia tu kana ngedere msituni likitoke hili hawaaaa oooh Lissu likitokea lile ooooh Kutekwa ..../ alipigwa Risasi Rais wa Uturuki hadharani mbona maisha yaaendelea??? Kennedy ...., kuweni wabunifu kuendesha chama sio vururuvururu ....hamtakuwa na tofauti na hao CCM
 
Tunamfahamu mkuu wetu. Huwa hapendi watu wazuri. Hapendi watu wenye uwezona ubunifu kwa sababu anataka chanzo cha kila kitu kiwe yeye.

Watu anaowapenda ni wale wasio na uwezo, wanafiki, wenye kusifu usiku na mchana.

Kiongozi wetu hajui faida ya kuwa watu wengi. Hatambui kuwa uwingi wenye uweso tofauti, fikra tofauti na ubunifu ni faida kubwa kwa Taifa na jamii.
 
Zito! sometimes unazingua babu! waache wachomane wao kwa wao!

Duh, nilidhani ni mimi peke yangu niliwaza hivyo...najiuliza chamuuma nini "mpinzani" wa kweli pale waziri wa chama tawala anapotumbuliwa?
 
Membe baki CCM.
January baki CCM.
Nape baki CCM.
Kinana baki CCM.
Makamba Sr baki CCM.

Mkiwa na vinyongo vyenu endeleeni kubaki huko huko mkichochea kuni mpaka 2020.

LISSU rudi haraka Tanzania wakati ni huu, Mbowe kaa chini na ACT mkubaliane pamoja na Seif na akina Jussa na wazanzibar wote, bara asimame LISSU na visiwani kama kawa Maalim na ACT.. CCM kwa hali waliyonayo kuni zikichochewa wanaanguka mapema sana 2020..
mimi nakuambia ndugu yangu, kuwang'oa ccm kwa sasa ni kazi kubwa sana, ccm ya kung'oka ilikuwa ya 2015 ile ya jk
 
Back
Top Bottom