Rais Magufuli huhitaji kujieleza unapomtoa Waziri. Kwa January Makamba jikalie kimya

Tatizo wewe ni msahaulifu, hivi uliwahi kumuona hata kwa dakika mbili tu makamba anatoa pole au kulaani kitendo cha kupigwa risasi Lissu, au kutekwa wananchi, au kuwekwa jela wapinzani akiwemo Zitto mwenyewe, kuuawa wananchi n.k.?
Hakuwahi kuongea chochote kuhusiana na dhahama zote hizo,so na yeye matatizo yake apambane nayo mwenyewe na dingi ake.

Full stop.
 
siku moja weekend nilikua na wageni wakiwepo wazazi wangu na vijana wangu wawili nikajitusu kwenda kukodi CD nikaipenda ya VAN'DAMEZ nikiwa najiamini kabisa nikampa kijana mmoja akaiweke kwenye kwenye deki na huku nikimuagiza alete na remote ya deki hahaha ile imeanza tu hata remote haijanifikia alaula! dah! kumbe ni PORN aisee sikua na namna zaidi ya kuisukuma TV idondoke
 
Inasikitisha sana...

Ni kweli kabisa... ila hapo naona kuna neno "Dhaifu" limetumika tena... hili neno sii lina jinai ndani yake?

Bunge liliitwa "Dhaifu" habari yake haikua ndogo...

Cc: mahondaw
 
Kwenye hili la Makamba kutolewa ni kwa ajili ya ule waraka, hizo nyingine ni sababu za kulazimisha. Ila mtu kama Makamba sio wa kutetea kwani ni mtu anayekalia kimya uovu ili kulinda madaraka yake. Kilichomkuta Makamba ni vita dhidi ya shetani aliye madarakani dhidi ya genge la maibilisi walio nje ya madaraka. Hapo Zitto anamtetea tu mshikaji wake lakini Makamba ni useless kwa upinzani.
Naunga mkono hoja.
 
nimependa makamba ambavo hajaenda leo ikulu kama watumbuliwa wengine huwa ni lazima waendee kusujudu kijana kaonesha kuwa ikulu kaanza kuingia kitambo so si lazima akasujudu
Ulikuwa husikilizi au hukuelewa
Kasema kulikua na miradi hewa ya kupanda mikoko, matumizi mabaya ta fedha za wafadhili, na marufuku ya mifuko ya plastiki aliichelewesha kwa miaka 4 na hata lilipotekelezwa juzi ni yeye alimlazimisha
Sijui kama ni kweli au ni kumpaka matope jamaa, Makamba nae katia ngumu, kagima kwenda Ikulu leo kama watumbuliwa wengine wanavyohudhuria
 
Aibu kubwa sana jamani. Huyu vipi? Mbona hadi watoto wanajua kuwa January kaonewa! Bora angepiga kimya tu. Hii sasa inatia hasira. [emoji35]
 
Rais Magufuli kwenye sababu za kumuondoa January Makamba bora jikalie zako kimya.

Nimekusikia Rais leo ukijaribu kuelezea sababu za kumuondoa Uwaziri Bwana January Makamba. Kwa kweli hukuwa umejiandaa na maelezo ya kuridhisha.

Rais, kwenye suala la mifuko ya plastiki tunajua ukweli kwamba wewe ndiye ulizuia lisiendelee ulipoambiwa kwamba litaua viwanda. Tunajua kwamba January ndiye ametumia miaka mitatu kuwaandaa wenye viwanda vya mifuko ili wabadilishe teknolojia na wasipate hasara. Tunajua kwamba January alifanya vikao vya umma (public hearings) kuanzia Karimjee mwaka 2017 hadi Mwanza mwaka 2018 na kwingineko kushirikisha wananchi kwenye jambo hili. Tunajua kwamba hatukusikia kauli yako kwenye mifuko ya plastiki hadi baada ya suala hili kufanikiwa. Hii sio kawaida yako maana wewe ni very predictable.

Tunajua kwamba mlimtegea Makamba ili afeli halafu mumtimue. Hakufeli. Sasa mnamtimua kwa kukamilisha kazi kwa weledi mkubwa! Mhe Rais wewe ni mkali maelekezo yako yasipotekelezwa. Umemuachaje Waziri miaka minne kwa kutotii maelekezo halafu unamtoa baada ya utekelezaji? Hakuna mwenye akili timamu anayeweza kukubali hoja yako hii dhaifu sana.

Bwana Rais ulikutana na wafanyabiashara kote nchini kutwa nzima. Walitaja kero zao zote, nami nikaziorodhesha. Sikusikia hata mmoja akilalamikia NEMC. Kwasababu gani? Kwasababu January ameibadilisha NEMC. Alitaka kuibadilisha huko nyuma na akavunja bodi na kuondoa menejimenti lakini kwakuwa inasemekana kulikuwa na ndugu zako walioguswa ukaagiza uamuzi ule ubatilishwe. Unadhani Watanzania wamesahau?

Bwana Rais fedha zinazotolewa na wahisani kwenye miradi ya mazingira zinakaguliwa na CAG na hakuna popote palipoonyesha ubadhirifu au upotevu. Kama upo uweke hadharani kama sisi tulivyoweka hadharani ubadhirifu wa TZS 1.5 Trilioni. Wacha wahisani, Serikali yako haijaweka hata senti tano kwenye miradi ya mazingira nchini. Mimi ni Mbunge na ninapitia kila Bajeti ya Serikali na Taarifa za CAG. Hujawahi kutenga fedha za Mazingira. Kwa kifupi, tunajua wewe binafsi sio mpenzi wa mazingira na umesema hivyo mara kadhaa. Hata huyo January mwenyewe “ulimtupa” kwenye mazingira ili apotee lakini ghafla kila Mtanzania leo anaongea mazingira. Hata wewe nawe leo unayaongea.

Bwana Rais hulazimiki kutoa sababu unapomuondoa Waziri. Kwa kutafuta kutoa sababu zisizoshiba leo, umeonyesha kwamba umesikia hisia za Watanzania kuhusu kuondolewa January Makamba. Umeondoa Waziri kipenzi cha Watanzania na Waziri weledi. Tunajua umemfukuza kwasababu nyingine, sio uchapakazi. Watanzania wote tunajua kwamba siku zote alikuwa anatafutiwa sababu tu ya kuondolewa. Ukisema uchapakazi ndio sababu Watanzania tunakushangaa kwasababu hawa mawaziri umewateua wewe lakini tathmini tunafanya sisi Watanzania. Na January Makamba ndiye alikuwa Waziri mbunifu na bora kabisa. Na ataendelea kuwa maarufu miongoni mwa Watanzania. Hakika ana nafasi kwenye uongozi siku sio nyingi sana zijazo. Mabadiliko ni lazima na January naamini atakuwa sehemu ya mabadiliko ili kujenga Tanzania inayojali watu wake na yenye Demokrasia iliyokomaa

Zitto ZR Kabwe
Mbunge Kigoma Mjini

Haaaahaaaaa….kwani hata wewe ni lazima ujibu kila kitu anachozungumza Rais? At least ukienda Kigoma labda.

una baadhi ya wana siasa mna mikono yenu kwenye matatizo ya rushwa na wizi wa mali ya umma yaliyokithiri Tanzania. Manahangaika sababu hamjazoea kula bila kukomba mboga
 
Huu uchapakazi ni pamoja na ule wa ku injinia goli la mkono?
 
Aibu kubwa sana jamani. Huyu vipi? Mbona hadi watoto wanajua kuwa January kaonewa! Bora angepiga kimya tu. Hii sasa inatia hasira. [emoji35]
Nani aliyemuonea? Kuchaguliwa na kutenguliwa si ridhaa ya anayechagua kwa katiba ya nchi yetu?
 
Zitto hujakosea kuhusu ubunifu wa huyu jamaa maana kaibuka na usanifu wa Waraka wa makatibu wakuu wawili wastaafu Adonia wa zama za Magufuli katika ubora wake.
 
Rais Magufuli kwenye sababu za kumuondoa January Makamba bora jikalie zako kimya.

Nimekusikia Rais leo ukijaribu kuelezea sababu za kumuondoa Uwaziri Bwana January Makamba. Kwa kweli hukuwa umejiandaa na maelezo ya kuridhisha.

Rais, kwenye suala la mifuko ya plastiki tunajua ukweli kwamba wewe ndiye ulizuia lisiendelee ulipoambiwa kwamba litaua viwanda. Tunajua kwamba January ndiye ametumia miaka mitatu kuwaandaa wenye viwanda vya mifuko ili wabadilishe teknolojia na wasipate hasara. Tunajua kwamba January alifanya vikao vya umma (public hearings) kuanzia Karimjee mwaka 2017 hadi Mwanza mwaka 2018 na kwingineko kushirikisha wananchi kwenye jambo hili. Tunajua kwamba hatukusikia kauli yako kwenye mifuko ya plastiki hadi baada ya suala hili kufanikiwa. Hii sio kawaida yako maana wewe ni very predictable.

Tunajua kwamba mlimtegea Makamba ili afeli halafu mumtimue. Hakufeli. Sasa mnamtimua kwa kukamilisha kazi kwa weledi mkubwa! Mhe Rais wewe ni mkali maelekezo yako yasipotekelezwa. Umemuachaje Waziri miaka minne kwa kutotii maelekezo halafu unamtoa baada ya utekelezaji? Hakuna mwenye akili timamu anayeweza kukubali hoja yako hii dhaifu sana.

Bwana Rais ulikutana na wafanyabiashara kote nchini kutwa nzima. Walitaja kero zao zote, nami nikaziorodhesha. Sikusikia hata mmoja akilalamikia NEMC. Kwasababu gani? Kwasababu January ameibadilisha NEMC. Alitaka kuibadilisha huko nyuma na akavunja bodi na kuondoa menejimenti lakini kwakuwa inasemekana kulikuwa na ndugu zako walioguswa ukaagiza uamuzi ule ubatilishwe. Unadhani Watanzania wamesahau?

Bwana Rais fedha zinazotolewa na wahisani kwenye miradi ya mazingira zinakaguliwa na CAG na hakuna popote palipoonyesha ubadhirifu au upotevu. Kama upo uweke hadharani kama sisi tulivyoweka hadharani ubadhirifu wa TZS 1.5 Trilioni. Wacha wahisani, Serikali yako haijaweka hata senti tano kwenye miradi ya mazingira nchini. Mimi ni Mbunge na ninapitia kila Bajeti ya Serikali na Taarifa za CAG. Hujawahi kutenga fedha za Mazingira. Kwa kifupi, tunajua wewe binafsi sio mpenzi wa mazingira na umesema hivyo mara kadhaa. Hata huyo January mwenyewe “ulimtupa” kwenye mazingira ili apotee lakini ghafla kila Mtanzania leo anaongea mazingira. Hata wewe nawe leo unayaongea.

Bwana Rais hulazimiki kutoa sababu unapomuondoa Waziri. Kwa kutafuta kutoa sababu zisizoshiba leo, umeonyesha kwamba umesikia hisia za Watanzania kuhusu kuondolewa January Makamba. Umeondoa Waziri kipenzi cha Watanzania na Waziri weledi. Tunajua umemfukuza kwasababu nyingine, sio uchapakazi. Watanzania wote tunajua kwamba siku zote alikuwa anatafutiwa sababu tu ya kuondolewa. Ukisema uchapakazi ndio sababu Watanzania tunakushangaa kwasababu hawa mawaziri umewateua wewe lakini tathmini tunafanya sisi Watanzania. Na January Makamba ndiye alikuwa Waziri mbunifu na bora kabisa. Na ataendelea kuwa maarufu miongoni mwa Watanzania. Hakika ana nafasi kwenye uongozi siku sio nyingi sana zijazo. Mabadiliko ni lazima na January naamini atakuwa sehemu ya mabadiliko ili kujenga Tanzania inayojali watu wake na yenye Demokrasia iliyokomaa

Zitto ZR Kabwe
Mbunge Kigoma Mjini
Jibu kuhusu hili
IMG-20190722-WA0013.jpeg
 
ila wewe mkuu Zitto ndiye kiboko hasa cha JPM.

naona huwa unampaga za uso kiasi kwamba si yeye mwenyewe wala system yake wote huwaga wana paralyse kabisa wasijue cha kukufanya wala kukujibu.

mkuu kongole sana - umewaweza haswa na wanakuogopa mnoo.

wewe na another fearless Lissu mkifanya collabo 2020 patachimbika!
 
Zitto unamtetea January? Haaa, rafiki yako unayepeana majungu na kumsema vibaya JPM katumbuliwa, sasa ZZK si umchukue aingie ACT ww si mwenyekiti..!! Hii nchi vituko vingi sana
 
Back
Top Bottom