Rais Magufuli huhitaji kujieleza unapomtoa Waziri. Kwa January Makamba jikalie kimya

Rais Magufuli huhitaji kujieleza unapomtoa Waziri. Kwa January Makamba jikalie kimya

Sasa mhehishimiwa Zitto, mimi ninashindwa kuelewa kuwa je wewe unahusikaje katika utendaji wa makamba na pia namna magufuri anapoamua nani afanye nae kazi.

Maana naona kama umekuja hapa kumtetea makamba as if una personal interest na yeye. Sasa kama mheshimiwa rais kaona haijafaa kufanya nae kazi na pia kuna lile swala la mazungumzo ya simu ambayo imeonyesha wazi kuwa huyu huyu January makamba alikuwa ana mipango ya hila inaendelea huko kando, why unataka mheshimiwa raisi ati amuache tu aendelee kuwapo.....?!

Sasa kimsingi nataka tu nikwambie raisi ni taasisi kamili. Sasa wanainchi tunafanya maelekezo yake.... Subiria muda wake utapita na ninyi mtapata wasaa wa kuongoza na kuhoji hayo maswala yenu ya kipolisi.
 
wazungu wanasema No research No Right to speak tusiwe tunapenda kuzungumza ili kupata public sympath na kumbuka m atukio ni mengi na kama majeraha yako kwa watu wengi tu na wala sio Lissu peke yako kama unavyosema, na hata kama Januar ana changamoto zake lakini ni mchapakazi asiye na makekena anapopanga jambo basi utekelezaji wake unakuwa ni rahisi na matokeo hasi yanaonekana( Angalio katazo la mifuko ya Plastic). Unadhani kama sio busara na akili yake huo mshike mshike wake barabarani na sokoni ingekuwaje. Mnyonge mnyngeni ila haki yake mpeni
Wewe ulikuwa nae huko ofisini akichapa kazi au kujipendekeza tu na haujui hata unalosema.

Kama ni mchapakazi mchukue ukachape nae kazi wewe
 
Hivi mlitaka raia wote milioni 50 wakemee kupigwa risasi Lissu??? Siwapendi CCM lakini pia sipendi zaidi upumbavu na unafiki wa chadema... yaaani kila tukio LISSU , mazingira Lissu kapigwa risasi , mkiongelea Kilimo Lissu kapigwa Risasi ..asingepigwa Risasi hivi msingekuwa na hoja nyingine!!! Wengine hatuna vyama ila kwa mikumbomikumbo ya Chadema na Upinzani kwa ujumla wao kurukia tu kana ngedere msituni likitoke hili hawaaaa oooh Lissu likitokea lile ooooh Kutekwa ..../ alipigwa Risasi Rais wa Uturuki hadharani mbona maisha yaaendelea??? Kennedy ...., kuweni wabunifu kuendesha chama sio vururuvururu ....hamtakuwa na tofauti na hao CCM
Mpumbavu mwenyewe, hapo nimetaja mambo mengi tu ila kwa sababu wewe ni mpumbavu huuoni ukweli
 
We zitto unakuwaga taahira saa zingine, hivi hii hoja ya trillion 1.5 kuna wapuuzi wanaowaamini

Kwa mwezi tu TRA inakusanya wastani wa trillion 1.3 na katika matumizi almost billion 600 zinaenda kulipa mishahara, sasa eti mtu aibe trillion 1.5? Nchi ingesimana. Na itapelekwa wapi mipesa mingi hivyo? Acacia tu imenunuliwa na Barrick kwa billion 980 (japo ni uongo)
CAG akamatwe kwa kuleta data feki maaan zitto sio CAG
 
Hatunywi sumu,
hatujinyongi ccm mbele kwa mbelee.
Wacha waisomee namba ehh ccm ni mbele kwa mbelee.
 
Rais Magufuli kwenye sababu za kumuondoa January Makamba bora jikalie zako kimya.

Nimekusikia Rais leo ukijaribu kuelezea sababu za kumuondoa Uwaziri Bwana January Makamba. Kwa kweli hukuwa umejiandaa na maelezo ya kuridhisha.

Rais, kwenye suala la mifuko ya plastiki tunajua ukweli kwamba wewe ndiye ulizuia lisiendelee ulipoambiwa kwamba litaua viwanda. Tunajua kwamba January ndiye ametumia miaka mitatu kuwaandaa wenye viwanda vya mifuko ili wabadilishe teknolojia na wasipate hasara. Tunajua kwamba January alifanya vikao vya umma (public hearings) kuanzia Karimjee mwaka 2017 hadi Mwanza mwaka 2018 na kwingineko kushirikisha wananchi kwenye jambo hili. Tunajua kwamba hatukusikia kauli yako kwenye mifuko ya plastiki hadi baada ya suala hili kufanikiwa. Hii sio kawaida yako maana wewe ni very predictable.

Tunajua kwamba mlimtegea Makamba ili afeli halafu mumtimue. Hakufeli. Sasa mnamtimua kwa kukamilisha kazi kwa weledi mkubwa! Mhe Rais wewe ni mkali maelekezo yako yasipotekelezwa. Umemuachaje Waziri miaka minne kwa kutotii maelekezo halafu unamtoa baada ya utekelezaji? Hakuna mwenye akili timamu anayeweza kukubali hoja yako hii dhaifu sana.

Bwana Rais ulikutana na wafanyabiashara kote nchini kutwa nzima. Walitaja kero zao zote, nami nikaziorodhesha. Sikusikia hata mmoja akilalamikia NEMC. Kwasababu gani? Kwasababu January ameibadilisha NEMC. Alitaka kuibadilisha huko nyuma na akavunja bodi na kuondoa menejimenti lakini kwakuwa inasemekana kulikuwa na ndugu zako walioguswa ukaagiza uamuzi ule ubatilishwe. Unadhani Watanzania wamesahau?

Bwana Rais fedha zinazotolewa na wahisani kwenye miradi ya mazingira zinakaguliwa na CAG na hakuna popote palipoonyesha ubadhirifu au upotevu. Kama upo uweke hadharani kama sisi tulivyoweka hadharani ubadhirifu wa TZS 1.5 Trilioni. Wacha wahisani, Serikali yako haijaweka hata senti tano kwenye miradi ya mazingira nchini. Mimi ni Mbunge na ninapitia kila Bajeti ya Serikali na Taarifa za CAG. Hujawahi kutenga fedha za Mazingira. Kwa kifupi, tunajua wewe binafsi sio mpenzi wa mazingira na umesema hivyo mara kadhaa. Hata huyo January mwenyewe “ulimtupa” kwenye mazingira ili apotee lakini ghafla kila Mtanzania leo anaongea mazingira. Hata wewe nawe leo unayaongea.

Bwana Rais hulazimiki kutoa sababu unapomuondoa Waziri. Kwa kutafuta kutoa sababu zisizoshiba leo, umeonyesha kwamba umesikia hisia za Watanzania kuhusu kuondolewa January Makamba. Umeondoa Waziri kipenzi cha Watanzania na Waziri weledi. Tunajua umemfukuza kwasababu nyingine, sio uchapakazi. Watanzania wote tunajua kwamba siku zote alikuwa anatafutiwa sababu tu ya kuondolewa. Ukisema uchapakazi ndio sababu Watanzania tunakushangaa kwasababu hawa mawaziri umewateua wewe lakini tathmini tunafanya sisi Watanzania. Na January Makamba ndiye alikuwa Waziri mbunifu na bora kabisa. Na ataendelea kuwa maarufu miongoni mwa Watanzania. Hakika ana nafasi kwenye uongozi siku sio nyingi sana zijazo. Mabadiliko ni lazima na January naamini atakuwa sehemu ya mabadiliko ili kujenga Tanzania inayojali watu wake na yenye Demokrasia iliyokomaa

Zitto ZR Kabwe
Mbunge Kigoma Mjini
well spoken mr.zitto keep it up[emoji1474]
 
Hivi mlitaka raia wote milioni 50 wakemee kupigwa risasi Lissu??? Siwapendi CCM lakini pia sipendi zaidi upumbavu na unafiki wa chadema... yaaani kila tukio LISSU , mazingira Lissu kapigwa risasi , mkiongelea Kilimo Lissu kapigwa Risasi ..asingepigwa Risasi hivi msingekuwa na hoja nyingine!!! Wengine hatuna vyama ila kwa mikumbomikumbo ya Chadema na Upinzani kwa ujumla wao kurukia tu kana ngedere msituni likitoke hili hawaaaa oooh Lissu likitokea lile ooooh Kutekwa ..../ alipigwa Risasi Rais wa Uturuki hadharani mbona maisha yaaendelea??? Kennedy ...., kuweni wabunifu kuendesha chama sio vururuvururu ....hamtakuwa na tofauti na hao CCM
Mzee rudi kwenye mikeka kule kuna friend game nyingi tu
 
Wewe ulikuwa nae huko ofisini akichapa kazi au kujipendekeza tu na haujui hata unalosema.

Kama ni mchapakazi mchukue ukachape nae kazi wewe
ni jinsi gani watanzania hatupendi kukubaliana na hali halisi, tusiendekeze chuki hata sehemu ambayo haina chuki, inawezekana anaka na mapungufu yake mengine ya kibinaadamu ilakwenye suala la uchapaji kazi January kwa kweli hakunaga kabisa
 
Kama ule Upinzani uliokuwepo kabla ya Uchaguzi wa mwaka 2015 ungekuwa sasa, Hizi vurugu za Chama Tawala sasa hvi wangepata Mtikiso mkubwa sana, Ila Ccm wanavurugana ila Upinzani Pia mishavurugwa hapo kabla so impact yenu na kutake advantage of this itakua ndogo sana.
Nakubaliana na wewe safari hii sababu ya Utenguzi tunaijua haitaji kutoa maelezo mengi sana.

Hapo kwenye bold, kwamba wapinzani wangeandamana au ................. inawahusu? Mana ndio silaha walioitumia sana. ila Impact ipo sio lazima uione leo
. Japo kuwa wamedhibiti mana kila mtu akijaribu kuangalia uwezekano wa kuhama NI MOTO, Wazichape umoumo
 
Si ACT wala CHADEMA wala CCM mimi ni mwanachama wa Zitto kama Zitto.


Kwa hili Mh. Zitto naomba ukae kimya tu.


Waparuane akili zikae sawa wenda watasikia walalahoi wanahitaji nini.


Ndege au Kuongeza kuajili walimu vijijini
 
Zito! sometimes unazingua babu! waache wachomane wao kwa wao!
Anamvizia January Makamba ! 🤔 Du ! Zitto mtu mbaya sana. Kwenye uchaguzi walisema January ndio alikua anadukua matokeo ya kura, Leo amekua waziri Bora kipenzi cha watu daa ! Mchikue tuuu ! Sio kumpambapamba !
 
Back
Top Bottom