Rais Magufuli kufanya ziara ya siku 5 Zanzibar, kuzindua jengo la TISS Zanzibar

Rais Magufuli kufanya ziara ya siku 5 Zanzibar, kuzindua jengo la TISS Zanzibar

Hayo majengo ya TISS zamani yalikuwa Siri Sasa hivi yanaanikwa tu Kama karanga hadharani kila mtu ayajue

Something is wrong somewhere

Tatizo mumekalia kuponda kila kitu, nenda hata Marekani uliza yeyote barabarani utaonyeshwa makao makuu ya CIA na Pentagon.
 
Kujulikana kwa watu what for? Ofisi ya TISS sio public office ya kutoa huduma kwa public.Kuwa watu wote waijue ili iweje?
TISS ni Public Office mkuu na watu wanaenda kupata huduma kama ofisi zingine za serikali ila kuna uwezekana wateja wanaoenda siyo wengi sana kwa sababu wanaenda kwa purposes maalum.
 
Ziara ya kikazi Zanzibar ni sawa, ila yeye kuhudhuria sherehe ya Mapinduzi si sawa, utaratibu wa maadhimisho ya sherehe ya mapinduzi ni wa kiboya unamdogosha na kumzalilisha Raisi wa Muungano - ambaye ndiye Raisi wa Nchi na Amiri Jeshi Mkuu

Dr. Shein alikuwepo siku ya kumbukizi la uhuru wa Tanganyika kule Mwanza, so ujirani mwema
 
Rais John Magufuli leo anatarajiwa kuanza ziara yake ya kikazi visiwani Zanzibar baada ya jana kuwasili Dar es Salaam akitokea chato kwa mapumziko.

Taarifa iliyotolewa jana kwa vyombo vya habari na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu, ilieleza kuwa Rais Magufuli leo ataanza ziara ya kikazi visiwani huko, akitarajiwa kuweka jiwe la msingi la jengo la Idara ya Usalama wa Taifa Zanzibar.

Ilielezwa katika taarifa hiyo ya Ikulu kuwa, kesho Rais Magufuli ataweka jiwe la msingi la Shule ya Sekondari ya Mwanakwerekwe iliyoko Mjini Magharibi na atafungua hoteli yenye hadhi ya nyota tano iitwayo Hotel Verde Azam Luxury Resort and Spa iliyoko Mtoni.

"Mheshimiwa Rais Magufuli atashiriki sherehe za maadhimisho ya Miaka 56 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar zitakazofanyika Jumapili Januari 12 mwaka huu katika Uwanja wa Amaan, Mjini Magharibi," ilielezwa katika taarifa hiyo ya Ikulu.
 
Sawa kabisa. Tunaamini atafanya yale yale ambayo hufanya akiwa katika ziara zake huku bara
 
Raisi wa Jamuhuri ya Muungano ndiye Raisi wa Nchi na Amiri Jeshi Mkuu (TISS, Tanzania Peoples Defence Force, Police Force, Prison, Migration, JKT na nk. viko under his command) lakini anaingia uwanjani wa kwanza, hasalimii wananchi wa taifa lake - akiwa amepanda gari lile la heshima 'jeep iliyowazi', hakagui gwaride....hii haiko sawa
Waliofanya hivyo wanajua protokoli kuliko wewe.. ...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom