Kauli za makada wa ccm wakiongozwa na Hamprey Polepole mitandani na runingani,
"Marekani wapumbavu sana, wanatuonea wivu kwa kuwa Symbion haitapata ulaji wa umeme"!
Lakini hawafahamu ukweli huu hapa:
Fact 1
Bajeti ya Tanzania (ambayo haijawahi kutekelezwa kwa hata 75%) ni shilingi TRLIONI 22 kwa mwaka!
Fact 2
Bajeti ya jimbo la California pekee ni Dola Bilioni 122.6 kwa mwaka, sawa na shilingi TRILIONI 245.2 (exchange rate ya $1 kwa TZS 2,000) kwa mwaka. Hii ni sawa na Bajeti ya Tanzania kwa miaka 11.15
Hakika Marekani wanatuonea wivu!
Fact 3
Bajeti ya Serikali ya Shirikisho la Marekani (US Federal Budget) kwa mwaka 2015 ni Dola Trilioni 3.8 ambazo ni sawa na shilingi TRILIONI 7,600. Hiki kiasi ni sawa na bajeti ya Tanzania kwa MIAKA 345 NA MIEZI 6 na kiasi hiki ni 21% tu ya GDP ya nchi!
Kichwa kinaniuma sana sijui kwa nini hawa wamarekani wanatuonea wivu kwa ajili ya kasimbioni chao!
Kichwa kinaniuma sana, nimemwomba Dr aniandikie Bruffen kabisa maana Diclofenac imebuma