pakaywatek
JF-Expert Member
- Dec 28, 2014
- 4,660
- 6,282
Akiwa katika uzinduzi wa daraja la juu Ubungo amesema atalivunja jiji na kuipa Ilala hadhi ya jiji na wilaya zingine zibaki kuwa Manispaa.
----
Rais Magufuli ameyasema haya
Nategemea Jiji la Dar es Salaam kulivunja na hii nawaambia hapa ili tutengeneze jiji la eneo fulani, tunaweza tukaifanya Ilala ndio ikawa jiji, ita-depend na mambo yatakavyoenda lakini kuwa na madiwani ambao wanakaa hapa juu, wanachangiwa hela, hawana miradi ya maendeleo, wanakula posho na hawakuchaguliwa na watu, hili nitalikataza.
Kwa hiyo ninalizungumza hapa, wale wanaojiandaa kuwa Mameya wa jiji la Dar es Salaam na wanakaa hawana maeneo wajue hicho kimekwisha. Tunataka Manispaa moja katika jiji la Dar es Salaam ndio ipandishwe hadhi iwe jiji halafu nyingine ziwe manispaa, ni kama ilivyo katika majiji mengine.
Kwahiyo mjiandae kisaikolojia wale waliokuwa wanataka umeya wajiji la Dar es Salaam, meya atapatikana kutoka Ilala au kutoka manispaa mojawapo ya hapa, huu ndio ukweli na ukweli utabaki kuwa ukweli na draft nimeshaletewa na mheshimiwa Jafo, nafikiri nikitoka huku nitakwenda kuisaini.
Ili turahisishe mambo, bajeti ya jiji ambayo haipo, fedha zilikuwa zinapotea ndugu zangu waheshimiwa wabunge, jiji la Dar es Salaam litaendelea kuwepo lakini tutachukua eneo fulani nafikiri Ilala inafaa kuwa jiji, ndio katikati ya jiji la Dar es Salaam, wewe Ubungo utasubiri kwanza kwasababu hata barabara bado hazijatengenezwa tengenezwa lakini nafanya haya ndugu zangu kwa kuangalia matumizi mazuri ya fedha zetu. Mwiso wa Nukuu