Rais Magufuli kuvunja Jiji la Dar es Salaam

Rais Magufuli kuvunja Jiji la Dar es Salaam

... mkoa ni mkubwa kuliko jiji. Mkoa ni sehemu ya serikali kuu kiutendaji wakati jiji, manispaa, halmashauri ni serikali za mitaa.
Asante kwa maelezo yako mkuu. Mwanzo nilijua jiji ni kubwa kuliko mkoa
 
Yan akivunja maana yake kutakuwa hakuna dar es salaam.. Au nimeelewaje!!. Badala yake ilala ndo itakuwa jiji kama sasa tunavosema jiji la dar es salaam.. Niko sahihi au.
Na ndo nilivyo elewa mie.
 
Yan akivunja maana yake kutakuwa hakuna dar es salaam.. Au nimeelewaje!!. Badala yake ilala ndo itakuwa jiji kama sasa tunavosema jiji la dar es salaam.. Niko sahihi au.
Unafahamu nadharia ya City, kisha Metropolitan Area? Hiyo inaweza kuwa ni mojawapo. Kunakua na Jiji la Ilala kwa mfano, kisha Manispaa za MKOA WA DAR ES SALAAM.
Kwa mfano kuna jiji la Maputo na Jimbo la Maputo, haviingiliani. Kwa mfano jimbo la Maputo makao makuu yake ni Matola.
Pia kuna Jiji la Kinshasa na Jimbo la Kinshasa nafikiri pale GOMBE.
 
Napata tabu kuelewa hii concept
... wala usipate tabu, ni concept rahisi sana. Ili uipate vizuri, tuchuke mji ambao jina lake sio jina la mkoa mfano Moshi.

Moshi iko katika mkoa wa Kilimanjaro na ina hadhi ya manispaa. Moshi na Kilimanjaro ni ipi kubwa? Ni Kilimanjaro; Moshi ni mji/Manispaa ndani ya Kilimanjaro kama itakavyokuwa jiji la Ilala ndani ya mkoa wa Dar-es-Salaam.

Ukiacha Moshi, Kilimanjaro ina halmashauri nyingine kadhaa ambazo ziko katika wilaya ngingine nje ya Moshi - Halmashauri ya Wilaya ya Same (ndani ya Wilaya ya Same); Halmashauri ya Wilaya ya Hai (ndani ya Wilaya ya Hai); Mwanga, Siha, Rombo, n.k. kama ambavyo kutakuwa na Mainspaa ya Temeke (ndani ya Wilaya ya Temeke), vivyo hivyo Ubungo, Kinondoni, n.k. katika Mkoa (sio jijji) wa Dar-es-Salaam.
 
Sina tatizo sana na chochote kinachofanyika..., swali langu hili suala wamekaa wadau wakaangalia pro and cons au ndio kuamka asubuhi na kutoa maamuzi ?

Tusipoangalia kila siku tutakuwa tunapanga na kupanga..., badili na kubadilisha...., ingeandikwa proposal ikapitiwa kwa ufanisi na kuangalia faida na hasara alafu ndio likafanyika jambo (hata kama jambo zuri vipi ni vema kuwahusisha wote pamoja na wananchi kwa kuwafahamisha ) Maamuzi ya kiwa ni ya wote ni rahisi kupokelewa vizuri
 
Back
Top Bottom