Rais Magufuli kuvunja Jiji la Dar es Salaam

Jiwe hivi huwa anafanya economic impact ya decisions zake anazochukua?

Ilala ina adminstrative area kubwa kiasi gani?

Je maamuzi yake hayo yatakuwa na impact kiasi gani kwa wakazi wa Ilala vs wakazi wa let say Temeke, Kinondoni etc

Naona anataka Kuiinua Dodoma kwa kuharibu status ya Dar

Huyu mzee ni mharibifu azuiwe!
 
Unafahamu nadharia ya City, kisha Metropolitan Area? Hiyo inaweza kuwa ni mojawapo. Kunakua na Jiji la Ilala kwa mfano, kisha Manispaa za MKOA WA DAR ES SALAAM.
Kwa mfano kuna jiji la Maputo na Jimbo la Maputo, haviingiliani. Kwa mfano jimbo la Maputo makao makuu yake ni Matola.
Pia kuna Jiji la Kinshasa na Jimbo la Kinshasa nafikiri pale GOMBE.
Exactly!

New York City inside New York.

Manchester City inside (Great) Manchester.

Cairo inside (Great) Cairo.
 
Kwahiyo madiwani walichaguliwa na nani? (Anathibitisha wizi wa kura kufanyika?)

Kwahiyo jiji la Dar Es Salaam linaenda kuwa historia? (Dar inakuwa ya "mikoani")

Ikiwa Jiji la Dar linaenda kufa, jiji kubwa kuliko yote Tz linaenda kuwa Mwanza.... (ok ok ok inaeleweka)

Ukienda kutafuta majiji makubwa East Africa, Nairobi anakosa mpinzani rasmi.
Mwanza Mwanza Mwanza Mwanza Mwanza Mwanza Mwanza Mwanza

Kanda peeendwaaaaaaaaa
 
Akiwa katika uzinduzi wa daraja la juu Ubungo amesema atalivunja jiji na kuipa Ilala hadhi ya jiji na wilaya zingine zibaki kuwa Manispaa.

----
Rais Magufuli ameyasema haya

Nategemea Jiji la Dar es Salaam kulivunja na hii nawaambia hapa ili tutengeneze jiji la eneo fulani, tunaweza tukaifanya Ilala ndio ikawa jiji, ita-depend na mambo yatakavyoenda lakini kuwa na madiwani ambao wanakaa hapa juu, wanachangiwa hela, hawana miradi ya maendeleo, wanakula posho na hawakuchaguliwa na watu, hili nitalikataza.

Kwa hiyo ninalizungumza hapa, wale wanaojiandaa kuwa Mameya wa jiji la Dar es Salaam na wanakaa hawana maeneo wajue hicho kimekwisha. Tunataka Manispaa moja katika jiji la Dar es Salaam ndio ipandishwe hadhi iwe jiji halafu nyingine ziwe manispaa, ni kama ilivyo katika majiji mengine.

Kwahiyo mjiandae kisaikolojia wale waliokuwa wanataka umeya wajiji la Dar es Salaam, meya atapatikana kutoka Ilala au kutoka manispaa mojawapo ya hapa, huu ndio ukweli na ukweli utabaki kuwa ukweli na draft nimeshaletewa na mheshimiwa Jafo, nafikiri nikitoka huku nitakwenda kuisaini.

Ili turahisishe mambo, bajeti ya jiji ambayo haipo, fedha zilikuwa zinapotea ndugu zangu waheshimiwa wabunge, jiji la Dar es Salaam litaendelea kuwepo lakini tutachukua eneo fulani nafikiri Ilala inafaa kuwa jiji, ndio katikati ya jiji la Dar es Salaam, wewe Ubungo utasubiri kwanza kwasababu hata barabara bado hazijatengenezwa tengenezwa lakini nafanya haya ndugu zangu kwa kuangalia matumizi mazuri ya fedha zetu.
Mwiso wa Nukuu

Nimeshangaa sana kwa maneno haya kwasababu,Wananchi ndo wanachagua Madiwani,halafu Madiwani wanachagua Meya wa Manispaa halafu Mameya na wajumbe wengine kutoka Halmashauri zoote ndo wanamchagua Meya wa Jiji la Dar......sasa inanichanganya kwa mtu mzoefu wa maswala ya Uongozi kuwa haoni umuhimu wa Halmashauri hii
 
... wala usipate tabu, ni concept rahisi sana. Ili uipate vizuri, tuchuke mji ambao jina lake sio jina la mkoa mfano Moshi.

Moshi iko katika mkoa wa Kilimanjaro na ina hadhi ya manispaa. Moshi na Kilimanjaro ni ipi kubwa? Ni Kilimanjaro; Moshi ni mji/Manispaa ndani ya Kilimanjaro kama itakavyokuwa jiji la Ilala ndani ya mkoa wa Dar-es-Salaam.

Ukiacha Moshi, Kilimanjaro ina halmashauri nyingine kadhaa ambazo ziko katika wilaya ngingine nje ya Moshi - Halmashauri ya Wilaya ya Same (ndani ya Wilaya ya Same); Halmashauri ya Wilaya ya Hai (ndani ya Wilaya ya Hai); Mwanga, Siha, Rombo, n.k. kama ambavyo kutakuwa na Mainspaa ya Temeke (ndani ya Wilaya ya Temeke), vivyo hivyo Ubungo, Kinondoni, n.k. katika Mkoa (sio jijji) wa Dar-es-Salaam.
Mkuu kwa maana hii kuna siku tutaona jiji la Moshi, Bukoba, Kahama, Chato au Sumbawanga ndio maana yake?
 
Upuuzi tu wa kuongeza gharama za uendeshaji za Serikali. Husikii huu upumbavu nchi zilizoendelea wa kuongeza idadi ya mikoa au majimbo.
Akiwa katika uzinduzi wa daraja la juu Ubungo amesema atalivunja jiji na kuipa Ilala hadhi ya jiji na wilaya zingine zibaki kuwa Manispaa.

----
Rais Magufuli ameyasema haya

Nategemea Jiji la Dar es Salaam kulivunja na hii nawaambia hapa ili tutengeneze jiji la eneo fulani, tunaweza tukaifanya Ilala ndio ikawa jiji, ita-depend na mambo yatakavyoenda lakini kuwa na madiwani ambao wanakaa hapa juu, wanachangiwa hela, hawana miradi ya maendeleo, wanakula posho na hawakuchaguliwa na watu, hili nitalikataza.

Kwa hiyo ninalizungumza hapa, wale wanaojiandaa kuwa Mameya wa jiji la Dar es Salaam na wanakaa hawana maeneo wajue hicho kimekwisha. Tunataka Manispaa moja katika jiji la Dar es Salaam ndio ipandishwe hadhi iwe jiji halafu nyingine ziwe manispaa, ni kama ilivyo katika majiji mengine.

Kwahiyo mjiandae kisaikolojia wale waliokuwa wanataka umeya wajiji la Dar es Salaam, meya atapatikana kutoka Ilala au kutoka manispaa mojawapo ya hapa, huu ndio ukweli na ukweli utabaki kuwa ukweli na draft nimeshaletewa na mheshimiwa Jafo, nafikiri nikitoka huku nitakwenda kuisaini.

Ili turahisishe mambo, bajeti ya jiji ambayo haipo, fedha zilikuwa zinapotea ndugu zangu waheshimiwa wabunge, jiji la Dar es Salaam litaendelea kuwepo lakini tutachukua eneo fulani nafikiri Ilala inafaa kuwa jiji, ndio katikati ya jiji la Dar es Salaam, wewe Ubungo utasubiri kwanza kwasababu hata barabara bado hazijatengenezwa tengenezwa lakini nafanya haya ndugu zangu kwa kuangalia matumizi mazuri ya fedha zetu.
Mwiso wa Nukuu
 
Dah....

wanakula posho na hawakuchaguliwa na watu
 
Ohoo kwahiyo pale ufipa panabakia kua mkoani?? Duh.
 
Yan akivunja maana yake kutakuwa hakuna Dar es Salaam.. Au nimeelewaje!!. Badala yake ilala ndo itakuwa jiji kama sasa tunavosema jiji la dar es salaam.. Niko sahihi au.
Anataka avunje Dar es Salaam ili ndani ya miaka 5 ya Kipindi cha Pili cha uongozi wake ajenge upya iwe kama Chato aliyoijenga miaka 5 mpaka imekuwa kama Ulaya. Hongereni Wakazi wa Dar kupata Mkazi anayewajali!
 
Akiwa katika uzinduzi wa daraja la juu Ubungo amesema atalivunja jiji na kuipa Ilala hadhi ya jiji na wilaya zingine zibaki kuwa Manispaa.

----
Rais Magufuli ameyasema haya

Nategemea Jiji la Dar es Salaam kulivunja na hii nawaambia hapa ili tutengeneze jiji la eneo fulani, tunaweza tukaifanya Ilala ndio ikawa jiji, ita-depend na mambo yatakavyoenda lakini kuwa na madiwani ambao wanakaa hapa juu, wanachangiwa hela, hawana miradi ya maendeleo, wanakula posho na hawakuchaguliwa na watu, hili nitalikataza.

Kwa hiyo ninalizungumza hapa, wale wanaojiandaa kuwa Mameya wa jiji la Dar es Salaam na wanakaa hawana maeneo wajue hicho kimekwisha. Tunataka Manispaa moja katika jiji la Dar es Salaam ndio ipandishwe hadhi iwe jiji halafu nyingine ziwe manispaa, ni kama ilivyo katika majiji mengine.

Kwahiyo mjiandae kisaikolojia wale waliokuwa wanataka umeya wajiji la Dar es Salaam, meya atapatikana kutoka Ilala au kutoka manispaa mojawapo ya hapa, huu ndio ukweli na ukweli utabaki kuwa ukweli na draft nimeshaletewa na mheshimiwa Jafo, nafikiri nikitoka huku nitakwenda kuisaini.

Ili turahisishe mambo, bajeti ya jiji ambayo haipo, fedha zilikuwa zinapotea ndugu zangu waheshimiwa wabunge, jiji la Dar es Salaam litaendelea kuwepo lakini tutachukua eneo fulani nafikiri Ilala inafaa kuwa jiji, ndio katikati ya jiji la Dar es Salaam, wewe Ubungo utasubiri kwanza kwasababu hata barabara bado hazijatengenezwa tengenezwa lakini nafanya haya ndugu zangu kwa kuangalia matumizi mazuri ya fedha zetu.
Mwiso wa Nukuu
"hawakuchaguliwa na watu" Ahsante sana Magu you are my hero. Vunja hilo jiji la viongozi wavamizi waliochakachua uchaguzi! Vunja haraka sana. Vunja hata bunge tafadhali sana
 
Nimependa hapo hawakuchaguliwa na wananchi.
Uzuri wa huyu Mjomba huwa hanaga siri kabisa.

Jiulize, ni nani kaamua mtu gani awe diwani wa DSM City Council? Bila shaka, madiwani wa DCC wanachaguliwa na madiwani wa zile manispaa tano za mkoa wa DSM. Kwa maneno mengine, hakuna mwananchi aliyempigia kura mtu fulani kuwa diwani wa DCC. Hapo ndipo kauli “...hawakuchaguliwa na wananchi...” inapoanzia!
 
wakuu mnashidwa kuelewa nini mwanza kuna jiji la mwanza ambayo ni nyamagana madiwan wake wamechaguliwa na wanachi na Arusha hivyo hivyo na majiji mengne kwa nn dar tu jiji la dar es salaam lisiwe liko katika halmashauri yoyote
 
Upuuzi tu wa kuongeza gharama za uendeshaji za Serikali. Husikii huu upumbavu nchi zilizoendelea wa kuongeza idadi ya mikoa au majimbo.
Wew hakunaga hata kitu ulichowahi kukikubali kilichofanywa na serikali.
 
Hapana Dar litakuwa Jiji kibiashara na siyo kiutendaji! Alyetia uzi huu hakufafanua sana alivyoeleza Mhe Rais! Litabaki jiji la Dar lakini kihalmashauri hakutakuwa na halmashauri ya Jiji la Dar!
Afafanue nini wakati maelezo ya mkulu yako wazi?
 
Back
Top Bottom