Rais Magufuli: Lukuvi hawezi kuwa Mgombea urais wa CCM 2025 kwa sababu ana umri mkubwa. Ni fursa ya Vijana

Wakati wengine wanakimbia Nchi wengine wanapanga mikakati ya nani awe Rais 2025 alafu wanashangaa kwa nini CCM inawatawala.
 
Tayari atakuwa na mtu wake anayemuandaa. Otherwise hakuna sababu ya kuwazuia au kuwanyima haki yao ya kugombea kama wana uwezo.

Biden sasa anapiga 78 na amechaguliwa kwa kishindo ..... why not Kabudi or Lukuvi?
Kumbuka Rais uwe na degree. Je Lukuvi anayo kutoka chuo kipi?
 
Yeye amesema chama Cha mapinduzi (CCM) yeye Kama mwenyekiti hawawezi kumpitisha aliyempita umri, rejea hata mh. Mstaafu JK alisema hivyo. kwahiyo hapo Katiba haihusiki, usi-genaralize. Bali ni ndani ya chama na utaratibu wao.
Kwahiyo katiba ina mipaka ndani ya chama?
 
Magufuli ambaye ndo mwenyekiti ataingia na jina lake katika mchakato wa kumpendekeza mgombea
 
2005-2010 William Lukuvi alikosa Ubunge, hivyo katika muda huo akawa RC wa Dodoma na Dar es Salaam.

Tuweke sawa kumbukumbu zetu

Acha kupotosha wewe, tangu mwaka 1995 mpaka leo 2020, mheshimiwa Lukuvi ni mbunge wa jimbo la Isimani, Iringa

Mwaka 2005-2010 alikuwa ni mkuu wa mkoa wa Dodoma na baadaye Dar es Salaam huku akiwa ni mbunge pia
 
Hii ngoma italeta fujo sana ndani ya chama...kama alienda awamu ya kwanza vizuri asidhan awamu hii ya mwisho kuna wataomwonea aibu
Watu wakishajua unatoka hata ile aibu inaondoka, Na kwa kauli hii ya leo ya namba moja tutegemee magenge tayari yatakuwa yameanza kujiunda ili Kuhakikisha yanashika power hio 2025, Mzee baba kuongea ivo leo ni kama ame initiate, Hata amini kabisa reaction ya hawa wanao mlamba miguu kwa sasa.
 
Chadema wataanza kuongelea Urais miezi mitatu kabla ya uchaguzi hahaha... succession plan muhimu wakati kazi zingine zinaendelea
Tena walivyo wajinga watatupiwa tu Kapi mwezi kabla ya Uchaguzi lije liwazike kabisa
 
Kitendo cha Mh Rais kutamka hadharani kuwa mtu yeyote aliyemzidi umri asijidanganye kuomba nafasi hiyo ni kwenda kinyume kabisa na katiba ya Nchi..
Huyu mhutu ameapa juzi tu kuilinda katiba ya JMT. Leo hii anaisigina katiba hiyohiyo kwa kutamka jambo nyeti ambalo katiba halijaweka ukomo wake. Amekuwa akiisigina katiba mara kwa mara kipindi cha miaka 5 iliyopita. Sasa dalili zinaonesha hakuna mabadiliko kipindi hiki pia.
 
Labda kama neno "Mfumo" limepoteza maana yake halisi.

Sasa kama chama kina "mfumo" thabiti inakuwaje mtu mmoja anaweza akatoa kauli kama Ile? Tulitegemea kama mfumo upo thabiti, hawezi mtu mmoja akasimama hadharani na kutoa statement kama Ile. Statement Ile ninya kibaguzi na ina infringe rights za wanachama wengi Sana wa CCM. Kilichoonekana pale ni kuwa mtu mmoja anaweza akafanya atakalo na chama kikashindwa kumdhibiti.

Hivyo, kama bado mnapenda kufanyakazi kimfumo, mdhibitiane ninyi kwa ninyi kutokutoa kauli zinazodhalilisha huo mfumo kama upo.
 
Lukuvi alimkodi Harmonize akampa milioni 60 aende akaimbe Isimani wakati wapiga kura wake hata uhakika wa maji hawana.

Ikumbukwe Lukuvi ni mbunge wa Isimani kwa miaka 20 mfululizo.
Wewe umesha fanyia nini jamii inayo kuzunguka au hata tu familia yako..yamkini hata familia imesha kushinda afu unakazana kutoa kibanzi cha mwenzio
 
Cheo na madaraka hupangwa na Mungu mwanadamu hawezi zuia muda wa Mungu ukifika..... Joe Biden amehangaika kusaka Urais tangia mwaka 1988 zaidi ya miaka 32 lakini Mungu akaja kumpa wakati ana miaka 77. Ogopa sana mipango ya Allah, aliwahi kumruzuku mtoto Nabii Ibrahim akiwa mzee aliyekongoroka hata mkewe hakuamini...... Neema ya Mungu haiwezi kupingwa na mwanadamu
 
Mkuu uko sahihi. Refa wa mchezo huu ni Mungu pekee, anaweza kumpa mtu red card hata asiwepo kushuhudia hayo anayo yapanga sasa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nime andika comment yangu bila kusoma Maoni ya wadau...

Nakuheshimu Sana Mh. Raisi ambae ki umri Ni Kama Baba mdogo....

Rais haendi ikulu kunyanyua vyuma, au kubeba mizigo

Jpm anapo sema watu wenye MIAKA kuanzia 60_75 yrs
Waachane na ndoto za kua marais hii Ni kutokana na nchi Zetu za kiafrika kukosa
STRONG INSTITUTIONS

Yale yalikua Ni Maoni yake binafsi...

Tukiweza kuwa na strong institution na Katiba nzuri mtu yeyote anaweza kua rais wa nchi....

Jpm kuongoza nchi hii Ni akili ya kawaida Sana na huwa naona ndoto yangu ya kua Raisi ameikamilisha yeye...

Mbali ya kutoka ukanda mmoja JPM
Ana ile tabia yake ya ubabe na kukiamini like Ambacho anakiamini yeye kua Ni sahihi kuto kushaulika na tabia yake ya kuto kupenda kubishiwa.....

Kuna vitu huwa vinanifanya nimpende JPM japo Kuna mitazamo mingi Sana ambayo natofautiana nae katika uongozi wake......

Itoshe kusema...
Mungu ibarik Africa mungu ibarik Tanzania mungu mbariki Jpm
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…