Rais Magufuli: Lukuvi hawezi kuwa Mgombea urais wa CCM 2025 kwa sababu ana umri mkubwa. Ni fursa ya Vijana

Safi sana JPM nafikiri hapa mawaziri wanatakiwa kufanya kazi kwa weledi na kuacha kupambania Uraisi na kwakweli itabidi uwe mkali ikibidi kuwatumbua watakaoenda kinyume na utaratibu.
 
Namuongelea huyu dikteta ,PM nimemsikia mkuu
Kumbe ulimsikia waziri mkuu amelizungumzia tatizo la bei ya cement, sasa kulikua na haja gani kwa JPM kurudia kuzungumzia tatizo hilo wakati limeshazungumziwa na waziri??
 
Kumbe ulimsikia waziri mkuu amelizungumzia tatizo la bei ya cement, sasa kulikua na haja gani kwa JPM kurudia kuzungumzia tatizo hilo wakati limeshazungumziwa na waziri??
Aongelee changamoto nyingine mbona ziko nyingi tu,ajira nk sio urais 2025 ambao hata yeye huenda asiwepo duniani au la
 
Alipoomba urais kundi kubwa la vijana lilikuwa asilimia ngapi? Tunapata rais wa nchi kwa legal processes na uwezo wa mtu kiutawala

Ujana tu hauwezi kuwa qualifications - anyway remain silent huenda nikawa mimi
Akina Lukuvi na watu waliomzidi umri wana haki ya kugombea uraisi.

Huyu Magufuli kwa kauli yake anataka kutwambia kuwa wananchi wakimchagua mtu wa chama chochote mwenye umri kymzidi yeye kuwa raisi atafanya kila mbinu ili asiwe rais kwa sababu anaamini raisi lazima awe mdogo kuliko yeye!.

Nchi haiongozwi kwa matakwa ya mtu, nchi inaongozwa kwa sheria

Hakuna sheria inayozuia mtu mwenye umri mkubwa kuliko Magufuli kuwa raisi

Haya ni mambo ya ajabu sana!
 
Aongelee changamoto nyingine mbona ziko nyingi tu,ajira nk sio urais 2025 ambao hata yeye huenda asiwepo duniani au la
Changamoto zote, au hiyo ya ajira uliyoitolea mfano, zitaendelea kuwepo hapa duniani.
 
Kama wapiga kura 65% ni vijana na logic ni Rais awe kijana, kumbe Lukuvi hakustahili kuwa Mbunge pia maana jimboni kwake vijana wako 65%. Kwa tamko hilo inaonekana bora ajiuzuru maana atawaongozaje vijana ilihali amechoka? Kwa hiyo Urais ni kubeba mawe au matofari? Huu ni ubaguzi wa kiumri.

Mimi nafikiri Urais ni Taasisi ambayo inafaa mtu mwenye maono na hekima bila kujali umuri, ndiyo maana America wamemchagu Biden (77) wakamwangusha Trump (74) kwa hiyo kwangu mimi umri si kigezo maalum cha kuwa Rais.
 
Magufuli hawafahamu vzr wajumbe, anyway wananchi ndo tutaamua asipangie watu
 
Kuweni waelewa. Mheshimiwa raisi amesema “mtu wa umri wake asijidanganye kugombea uraisi “.
Hakusema “hairuhusiwi”.
 
Nakazia hapo "wisdom"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…