Rais Magufuli: Lukuvi hawezi kuwa Mgombea urais wa CCM 2025 kwa sababu ana umri mkubwa. Ni fursa ya Vijana

Kipengele gani cha katiba kinaelekeza hivyo? Ndio maana mimi namuelewa sana Tundu Lissu linapokuja suala la utawala wa sheria. Kwa maneno hayo ya Mh. JPM ina maana hicho tayari ni kigezo wakati wa kupitisha mgombea, kitu ambacho ni kinyume na katiba.
 
Naona maamuzi ya mtu mmoja yameanza kufanya kazi
 
Kuweni waelewa. Mheshimiwa raisi amesema “mtu wa umri wake asijidanganye kugombea uraisi “.
Hakusema “hairuhusiwi”.
Maana ya kutokujidanganya maana yake hataruhusiwa kugombea, maana kugombea lazima mgombea adhaminiwe na chama cha siasa na mwenyekiti amesema mtu wa umri huo asijidanganye, akigombea atateuliwa na nani? Na wewe uwe mwelewa
 
Katiba siyo kipaumbele tena
 
Kwa jinsi watu wanavyo changia naona asilimia chache saana wamemwelewa Rais, ngoja niendelee kufuatilia,

"Haya mambo yanapangwa" [emoji118]
 
Maana ya kutokujidanganya maana yake hataruhusiwa kugombea, maana kugombea lazima mgombea adhaminiwe na chama cha siasa, na mwenyekiti amesema mtu wa umri huo asijidanganye, akigombea atateuliwa na nani? Na wewe uwe mwelewa
Tusubiri abadilishe katiba kuhusiana na hilo swala la umri. Tusiseme mengi sana.
Pia tuombe uzima kufika2015, tuuone umri wa mgonbea uraisi wa CCM.
 
Isitoshe anayetakiwa kuchagua Rais ni wananchi na sio mtu mmoja
 
Hahaha,fumbo mfumbie mjinga mwerevu atalitegua..

Mwinyi alitayarishwa zamani sana kuwa atakuwa Raisi wa Zanzibar..

Mwinyi hamalizikii hapo,atafata nyayo za Baba Ake,ni yeye ndie atakae kuwa Raisi wa Jamuhiri ya Tanzania akiondoka Magufuli

Kama Magufuli ataondoka

Tuweka hakiba ya maneno
 
Isitoshe anayetakiwa kuchagua Rais ni wananchi na sio mtu mmoja
Kama wananchi walichagua tarehe 28/10/2020 halafu Tume ikateua bila kujali chaguo la wananchi wakafuata maagizo vilevile maagizo yatatolewa kwa wajumbe
 
Haya ndio matatizo ya mdomo kuongea bila kuwasiliana na ubongo. Ndio maana wenzetu wa watu wanaitwa speech writer/editor et ela..
 
Raisi hakupangii lakini anasema Kwa kutumia chama chake , hajasema vyama vyote wasipeleke wagombea wenye umri zaidi ya 70. Kwa upande wake maana kila chama kina Sera zake.
 
Kamati ya CCM ikimptisha mtu ndio mnakuja kuchagua mbona uko local Sana wewe . Kwa mwenyekiti ambae ni raisi ndani ya chama atatumia nafasi yke kbl y kultw km mgombea wa chama cha mapinduzi
 
Lukuvi alimkodi Harmonize akampa milioni 60 aende akaimbe Isimani wakati wapiga kura wake hata uhakika wa maji hawana.

Ikumbukwe Lukuvi ni mbunge wa Isimani kwa miaka 20 mfululizo.
Kumbe na wewe ulimuamini Msigwa..!! Maskini ya Mungu
 
Lukuvi alimkodi Harmonize akampa milioni 60 aende akaimbe Isimani wakati wapiga kura wake hata uhakika wa maji hawana.

Ikumbukwe Lukuvi ni mbunge wa Isimani kwa miaka 20 mfululizo.
Alikuwa Mkuu wa mkoa wa dar es salaam kipindi gani?
 
'Hivi vitu huwa vinapangwa…hakuna mtu alitegemea kuwa Mwinyi au mimi ningekuwa Rais…'

Nmekuwa nawakumbusha vijana humu kuwa CCM haijawahi kwenda Dodoma kuchagua mgombea Urais ikiwa haina jina la Mgombea

Kuna watu bado wanaamini JK hadi anaenda Dodoma kuchagua Mgombea Urais alikuwa hajui kuwa JPM ndie Mgombea
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…