Rais Magufuli: Lukuvi hawezi kuwa Mgombea urais wa CCM 2025 kwa sababu ana umri mkubwa. Ni fursa ya Vijana

Rais Magufuli: Lukuvi hawezi kuwa Mgombea urais wa CCM 2025 kwa sababu ana umri mkubwa. Ni fursa ya Vijana

Umesema kweli kabisa. Kama tumeshindwa kukombolewa na Lisu, basi kwisha habari yetu...
Nyomi na moto wa Mrema haujapata kutokea. Hata Lowassa ilikuwa zaidi ya Lissu.

Bahati mbaya sana CCM na vyombo vyake wanajua wapi, namna gani na muda gani wafanye yao ili kutwaa Nchi. Hii circle inaweza kuendelea mpaka kizazi chetu hiki kitakapotoweka hapa duniani
 
Umesema kweli kabisa. Kama tumeshindwa kukombolewa na Lisu, basi kwisha habari yetu.
Kama ulivyosema Mtanzania akipata mihogo ya watot, jioni akapata kahawa , na mwanamke, basi inatosha ...... tumefikishwa hapo. Majitu mazima yanamuita Jiwe Yesu...
Binafsi nimejifunza mengi ndani ya utawala huu, najaribu kujifunza pia roho mbaya na kutowaamini watu.

Unakuta anakuomba Jero, au muuza kahawa yuko busy na Mitano Tena.

Wenfine wakipewa elfu 5 ndio basi tena, wanachukulia siasa kama ushabiki wa mpira.

Nadhani katika hili Watu maarufu wanawajua wabongo vizuri, wao wameamua ku-side na mwenye uwezo wa kuwapa pesa, fursa na vyeo basi.

Mostly wabongo wako hoiii, fo fofo. Ndio maana watu wenye akili wanapata tabu sana nchi hii
 
Nyomi na moto wa Mrema haujapata kutokea. Hata Lowassa ilikuwa zaidi ya Lissu.

Bahati mbaya sana CCM na vyombo vyake wanajua wapi, namna gani na muda gani wafanye yao ili kutwaa Nchi. Hii circle inaweza kuendelea mpaka kizazi chetu hiki kitakapotoweka hapa duniani
CCM haina lolote kama chama.

Uchaguzi wa mwaka huu umeporwa na Dola.
 
Sina hakika kama katiba ya nchi hii ina ukomo wa umri kwenye sifa za kuwa rais wa JMT.

Chochote kinawezekana ikiwemo na Lukuvi kuwa Rais wa JMT.(Ndani au nje ya CCM)😁

What if Magu asiwepo hiyo 2025 yenyewe na "king makers" waliobaki wakawa hawana mawazo kama yake?

Michael Chilufya Sata (King Cobra) mwenyewe aliukwaa akiwa 74.
 
CCM haina lolote kama chama.

Uchaguzi wa mwaka huu umeporwa na Dola.
CCM na dola ni chanda na pete. Hujaona majaji na RPCs wastaafu wakichukua form za uchaguzi CCM? Hawa walikuwa wanachama watiifu kitambo sana
 
CCM na dola ni chanda na pete. Hujaona majaji na RPCs wastaafu wakichukua form za uchaguzi CCM? Hawa walikuwa wanachama watiifu kitambo sana
Yes, hicho ndicho waluchofanikiwa kufanya.

Vyama vya upinzani Tanzagiza huwa vinapambana na Dola, siyo CCM.
 
Mwenyekiti wa CCM Rais Magufuli amesema uchaguzi mkuu wa 2025 utatoa fursa kwa vijana kwa sababu zaidi ya 65% ya wapiga kura ni vijana

Rais Magufuli ametoa mfano wa mh Lukuvi kwamba hawezi kuwa Rais wa JMT 2025 kwa sababu atakuwa na miaka zaidi ya 70.

Maendeleo hayana vyama!

=======

RAIS MAGUFULI: Hakuna mtu alitegemea Mwinyi atakuwa Rais wa Zanzibar lakini pia Mwinyi katika kipindi chake chote hakuutafuta Urais, vitu hivi vinapangwa. Hakuna mtu alijua profesa Ibrahim atakuwa Jaji mkuu wa Tanzania hata mimi sikujua kama nitakuwa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania.

Kwa sababu katika miaka yote ishirini nikiwa waziri na nikiwa mbunge sikuwahi kuomba hata ujumbe wa NEC.

Sikuwahi, wajumbe wa NEC walikuwa wakina Lukuvi, tangu aingie mle ni mjumbe wa NEC lakini Urais hakuupata na sina uhakika kama ataupata Urais. Wewe sasa hivi ana miaka sitini na kitu, tukapendekeze kwenye central committee tukachague Rais anaenizidi umri mimi, ndio ukweli.

Maneno mengine yanaumiza lakini nataka niwaeleze muwe mnajitayarisha kisaikolojia kusudi msipoteze hata hela zenu, hata wewe profesa Kabudi huwezi ukawa Rais, najua haya mambo ni magumu lakini huo ndio ukweli.

Mzee Kikwete wakati anaondoka, alisema hataona Rais ambae anamzidi umri wake, sasa muangalie mimi nina umri gani nitakapokuwa namaliza, ujipimie kuanzia kwenye umri pale. Yaani Malecela tumpendekeze awe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, haiwezekani! Ameshakuwa mstaafu, tunamheshimu, tunampenda.

Najua mmenyamaza kwa hiyo inawezekana umekaa na jirani yako ambae ndie atakuwa Rais ambae labda ni kijana zaidi kwa sababu 65% ya watanzania ni vijana na hivi ndivyo vilivyomsaidia Mwinyi kushinda kule, wapiga kura ni vijana wether you like or not huo ndio ukweli, sasa huwezi ukawapelekea wapiga kura mtu ambae sio saizi yao.

Maneno yanauma lakini si mmeniomba niseme hapa, mimi nilikuwa nimekaa kimya tu leo nisiseme, nilikuwa nachomekea tu.
Mi namtaka Makonda basi,kwingine huko ni kupotezeana muda.
 
Majaliwa je? Naona wagombea hapo ni Jaffo, January, Mwingulu.
Ongeza wengine
Miaka mitano bado Sana , hata hivyo chaguzi kwa Sasa sioni Kama Zina maana yoyote, ila pamoja na yote mshishangae kipindi hicho,MACKONDA akapitishwa na chama, hacha wanyukane sisi yetu macho
 
Binafsi nimejifunza mengi ndani ya utawala huu, najaribu kujifunza pia roho mbaya na kutowaamini watu.

Unakuta anakuomba Jero, au muuza kahawa yuko busy na Mitano Tena.

Wenfine wakipewa elfu 5 ndio basi tena, wanachukulia siasa kama ushabiki wa mpira.

Nadhani katika hili Watu maarufu wanawajua wabongo vizuri, wao wameamua ku-side na mwenye uwezo wa kuwapa pesa, fursa na vyeo basi.

Mostly wabongo wako hoiii, fo fofo. Ndio maana watu wenye akili wanapata tabu sana nchi hii
Nyerere alituroga akatumaliza....
 
Kitendo cha Mh Rais kutamka hadharani kuwa mtu yeyote aliyemzidi umri asijidanganye kuomba nafasi hiyo ni kwenda kinyume kabisa na katiba ya Nchi.

Hakuna sehemu katika katiba ya Nchi yetu inayomkataza mtu yeyote kugombea nafasi ya Urais kwa kigezo cha umri mkubwa.

Washauri wa Rais jaribuni kumshauri Bwana Mkubwa kuna kauli akizisema ninaleta mtafaruku mkubwa sana katika jamii.
Acheni mambo ya kinganga kanga hapa. Rais alikuwa analopoka tu lakini sio kuwa kitu cha kukitilia maanani. Yeye sio mungu na wala sio malaika. Saa nyingine yanaweza yakamtoka tu mambo.

Sure Lukuvi anaweza akawa Rais kama yeye alitoka. Watakao kuja wengine wanaweza kumpendekez kuwa Rais. You neuer know!
 
Nawaza tu, hivi Obama angekuwa na hayo mawazo, sijui Biden angeuonea wapi huo urais.

Tz ya CCM ni zaidi ya ukichaa.
 
Alikuwa Mkuu wa mkoa wa dar es salaam kipindi gani?
Umesahau kipindi kile watu walikuwa na vyeo hata 20.

Mtu ni mbunge, mkuu wa mkoa, mjumbe wa CC, Mjumbe wa NEC, Mwenyekiti wa kamati ya bunge n.k ila elewa Lukuvi ana miaka zaidi 20 ya ubunge Isimani.
 
Lakini yeye alianza akiwa kijana, mbona awamu ya pili kesha zeeka na amegombea? Si angewaachia vijana?
 
Back
Top Bottom