Rais Magufuli: Maabara Kuu ya kupima sampuli za COVID-19 yaonyesha mafenesi, mapapai na mbuzi yana uambukizi

Mmmh, huyu mzee ana uhakika lakini? Mbona hatujasikia sehemu nyingine

Sent using Jamii Forums mobile app
Inawezekana ni vipimo vyetu tulivyonavyo.
Lakini hii inatia wasi wasi kama hamna hatua zilizochukuliwa kuhakikisha tunapata majibu sahihi ya sampuli zinazopimwa. Maana fact ni kwamba ugonjwa upo hata kama vipimo wakati mwingine vimetoa majibu ya uongo ( haijulikani kama ni mtu au vipimo ndio vimetoa majibu hayo), tahadhari ni muhimu
 
Umeongea professionally mkuu. Kudos.
 
Ila nahisi hapa imetumika lugha flani kuficha ukweli. Pengine hayo mapapai na mafenesi yanawakilisha kitu flani. Inaweza ikawa kweli sampuli za mtu mmoja zimepelekwa kwa majina tofauti na majibu yakawa positive na negative at the same time while it was from the same person. Ni mawazo yangu tuu.
 
Mkuu GUSSIE nashukuru kwa bandiko zuri. Naomba unitoe kidogo ujinga, hivi nini kinapelekwa kupimwa ili kubaini huyu MTU ameshambuliwa au hajaambuzwa Coronavirus? Naomba wataalam muliopo hapa JF mtutoe tongotongo.

Ahsante
Wanapima swab, siyo damu. Swab ni kama una unaingiza kitu kinachochukua majimaji kwenye sehemu ambayo unaamini kama mtu ana maambukizi ni lazima utakipata kisababishi.

Naona kwa suala la corona, wanaingiza kitu puani kinaitwa viral nose swab au wanaweza kuingiza kooni kitu kinachoitwa throat swab. Mchukuaji sample anakuwa kama anapangusa ndani ya pua yako au kwenye kooo ili kuweza kupata sample ya kupeleka maabara.

Lakini kuna taratibu za kuchukua. Siyo unakutana tu na mtu barabarani unaamua kumchukua sample. Samples hizi zinatakiwa kuchukuliwa kwenye chumba chenye ubaridi na negative pressure, na sample inabidi itunzwe kwenye vifaa maalum. Kosa katika uchukuaji, usafirishaji, vinaweza kuchangia kutoa majibu yasiyo sahihi.

Sample hizo za mbuzi zilichukuliwaje? Zilisafirishwaje, zilitunzwaje? Na vipi kuhusiana na reagents zinazotumika, zinaweza kutumika kwa wanyama kama mbuzi au tunda kama papai?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Siku nyingine jipange fikia guest house kama una muda mchache huko kama bajeti inaruhusu otherwise kwenye miji ya watu utateseka.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Mkuu Bams ubarikiwe kwa maelezo yako ya kitaalamu. Natumaini kupitia kwa maelezo uliyotoa tunaweza sasa ku argue critically katika mada iliyopo mbele yetu.

Ahsante
 
Alafu hayo ni mambo ya kitaalamu wala hakupaswa kuwavizia kama ni kweli kafanya hivyo. Naamini wataalamu wa wizara wanafanya kazi yao na kama kweli aligundua hilo angewasiliana na waziri ili warekebishe kasoro. Yote haya anayafanya lakini tayari mgeni Korona tunaye na inawezekana akatufanyizia sana siku si nyingi (siombei). Anafikiri anafunika kombe mwanaharamu apite lakini kuna tatizo kubwa kwake.
 
Magufuli baba lao, mabeberu na vibaraka wao wameze wembe. Hatutishiki, ng'o! Kinyago chao.
 
Mkuu GUSSIE nashukuru kwa bandiko zuri. Naomba unitoe kidogo ujinga, hivi nini kinapelekwa kupimwa ili kubaini huyu MTU ameshambuliwa au hajaambuzwa Coronavirus? Naomba wataalam muliopo hapa JF mtutoe tongotongo.

Ahsante
Kuna njia mbili So far za uchunguzi wa maambukizi haya ya Coronvirus Disease 2019 ( COVID-19) ... au ifanyike Chest CT scan

Njia ya kwanza ni kudetect antibodies ambazo mwili huzalisha kupambana na Adui , kwa case ya Corona tunaangalia IgG, IgM.. Kwa Bahati mbaya kabisa , hizi test kit za kudetect antibodies bado hazijakua confirmed na WHO ...nahii njia haijatumika sanaa.



Njia inayotumika kwa sasa ni kudetect uwepo wa Kirusi moja kwa moja ama kwakufanya rRT-PCR, au kudetect antigen wa COVID-19 yaan COVID-2019 n.k

Njia hii hutumia sample ambazo huchukuliwa kama swab ndani puani au kooni (kwa maambukizi yaliyo bado ktk eneo lajuu ya mfumo wa upumuaji).. Lkn punde maambukizi yanvyoshuka chini kuyafuata Mapafu, basi hapo lazima kufanyike aspiration ili kupata Aspirates kutoka katika Mapafu.

Kwa MTU aliyekufa, hufanyika Autopsy na kuchukua sehemu ya pafu na kwenda kuchunguza.


Kwa hapa bongo Nahiyo maabara , bila shaka wanafanya rRT-PCR test , ambapo wataalamu kwanza wana chukua sampo wanaitreat na Ku extract RNA pekeake , kisha wanaifanyia Reverse transcription kupata Viral DNA ndo sasa wanaingiza kwenye mashine kutengeneza copies zake kibao....

rRT-PCR ni nzuri kwa sababu hata kirusi kimoja kinaweza tumika kuzalisha copies kibao.


Turudi kwa JPM...


Kutokana na Mchakato mzima wa utendaji kazi wa Hii mashine., kwa kuzingatia hatua kwa hatua .

Na kwasababu amekiri kua Wataalamu Wetu sio kwamba hawana uelewa.




Basi niseme ivi, YEYE JIWE AACHE POROJO POROJO .


Kama hataki kusikia habari za maambukizi, asilazimishe mambo.


Aamue tu kuanzia Leo, Hamna kutangaza Idadi ya maambukizi.


Nasio kutisha tisha Watu nakufanya hawa wafanyakazi washindwe kutumia umahiri wa fani zao walizozisomea kwa miaka kadhaa ,badala yake waendelee kufanya Yale yanayompendeza yeye .



NASEMA IVI, HAMNA CHA PAPAI, WALA.OIL, WALA MBUZI ,WALA KWARE WALA BIBI YAKE MBUZI WALIOPIMWA.



JIWE NI MJANJA KTK KUZALISHA HOFU.














Sent using Jamii Forums mobile app
 
kuanzia Leo Kwa kipindi kisicho julikana watanzania tujiepushile na vitu vifuatavyo sababu vinaweza kutumiwa na mabeberu muda wowote.

Oil ya gari Kwa jina la Jabir Hamza.

Fenesi Kwa jina la Sarah Samweli.

Papai Kwa jina la Elizabeth Anne.

Mbuzi Kwa jina la mtaki mtwale.

Pamoja na kondoo Kwa jina la Juma kifuko.

N:B
Adumu jiwe kutoka chato




Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…