Rais Magufuli: Maabara Kuu ya kupima sampuli za COVID-19 yaonyesha mafenesi, mapapai na mbuzi yana uambukizi

Rais Magufuli: Maabara Kuu ya kupima sampuli za COVID-19 yaonyesha mafenesi, mapapai na mbuzi yana uambukizi

Watu wengi hawajaelewa hii kitu kabisa mkuu.

Ni kwamba TISS walichukua sample ya kamasi za mbuzi, sample ya ute ute wa papai, alafu wakapeleka maabara DSM.
Zote hizo zikakutwa zina corona.



Sent using Jamii Forums mobile app
Kama ndivyo unavyoamini ni nini kilichomkimbiza Ikulu zote mbili na kwenda kujichimbia huko aliko?? Pili kuna sababu gani ya kukimbilia kufanya teuzi wakati Wasaidizi wake Wakuu wako Msibani?? Wizara si ina Naibu Waziri?? Mambo mengine siyo ya kuyatetea Mkuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jiwe akiongea maneno kumi unakuta moja tu ndio la kweli, angekuwa kama anavyosema corona ni ugonjwa mdogo angekuja zake dodoma aendelee kuchapa kazi.

Kwamba unapima mananasi wakati watu wanalalamika vipo havitoshi sababu maabara ni moja watu wapo Arusha wanatuma sumpuri Dar halafu wewe unaweka jam kupima mananasi!

Ni upumbavu, narudia tena ni upumbavu kuapisha waziri kwenye makazi binafsi ya Rais wakati Ikulu ipo Geita, Mwanza.

Taasisi ya urais sio mali ya mtu binafsi.
Wewe ndio mpumbavu usiyejua kuwa Chato kuna Ikulu!
 
[emoji23][emoji23][emoji23] basi tuna madaktari wa hovyo kupata kutokea duniani yani uletewe sampuli ya utomvu wa papai uambiwe ni majimaji ya binadamu upime usijue wallahi hii nchi inaenda pabaya.. Hivi huyu ndugu yenu anatuona sisi mazuzu sana au??

Sent using Jamii Forums mobile app
Na ukweli sisi ni mazuzu! Jiulize wabunge walivyokuwa wanafanyiwa fumigation na mtambo wa Rostam Aziz wenye Chlorine pale bungeni wakati haiwezi kuua kirusi cha corona na badala yake ni kuua menda na viroboto....
 
Yani hao mabeberu anaowaongelea wenyewe wanahemelewa na corona vifo kila siku ndio waje wahangaike na Tz kweli?hivi CCm mbn mlitukosea sana heshima kutupa huyu mtu?
 
Hili la Mkuu wa nchi kupima Mbuzi na mapapai badala ya kupima watu, imetudhalilisha sisi Kama watanzania nimeona kule Kenya wameanza kutucheka na kutudhalilisha wakiandika kuwa kenya twapima binadamu Tanzania wao wapima mbuzi na mapapai, aiseee tumeanza kuchekwa Kama watoto wadogo, wakuuu hiii kitu imeshangaza Sana inamaana Mkuu wa nchi haaamini kuwa corona ipo?

Ninajiuliza kuwa tungekuwa na maaambukizi mengi Kama kenya Au Africa kusini Au zile nchi za ulaya ingekuaje? Ninasikitika Sana na kauli Kama hiii Ya mtu msomi kuhisi kuwa corona ni uongo huku anarudi kusema kuwa corona kweli ipo tuchukue hatua, sasa Mimi sielewi huku unasema kuwa corona kweli ipo huku unasema kuwa mabeberu wanatumika huku hao hao mabeberu unafaham kuwa ndio wenye idadi kubwa ya wagonjwa wa corona had majirani zako wako Juu kwa maaambukizi inamaaana wanakubeberu Halafu kwao wanaongeza Namba kwako wanakushusha?

Vipimo huviamini Wakati ndivyo vinavyopima kwao huko? Hivi ikitokea huyu akawa na maamabukizi Kama nchi zingne si ndio atatembea akiimba kuwa ameletewa corona? Haki ya MUNGU huyu Mkuu amedhalilisha nchi na kila Siku analete mambo ya hovyo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu we ni mtu mzima sio mwehu
Wapi asema mananasi?? Acha ujinga bas
Kasema fenesi ule utomvu wake
Mbona mnakuza mambo Sana tena uongo

Sent by IPhone
Utomvu wa Fenesi unafanana na umajimaji (Fluids) wa sehemu gani ya mwili wa binadamu!?
 
Ameyasema hayo leo wakati wa kumuapisha Waziri wa Sheria na katiba kuwa vyombo vya usalama vilipenyeza sampuli kutoka kwenye mananasi, mafenesi, mbuzi, kondoo, nk kwa siri na kuzifanya ni za binadamu. Jambo la kushangaza matokeo ya baadhi ya sampuli hizo au yalionyesha yana maambukizi ya corona.
"...tunawasiliana na Madagascar na wamehaidi kututumia dawa inayotibu covid 19...." JPM
Mambo ni mengi ngoja niweke clip ya video!
Chanzo ITV....
"...tunawasiliana na Madagascar na wamehaidi kututumia dawa inayotibu covid 19...." JPM [emoji44][emoji44][emoji44][emoji87][emoji87][emoji87][emoji40][emoji40][emoji40][emoji40]

Jr[emoji769]
 
Mtume Muhammad s.a.w anasema:

"If you dont have shyness, if you dont have this quality of bashfulness then you can do whatever you wish"

Kwa sababu hakuna kinakachokuzuia from doing a foolishness/shameless thing.. Hiki ni Qiyama!

Na akasema vilevile:

"(Ukiona) madaraka yameangukia kwa asiye na ujuzi(utaalamu kwa muhusika) subirini Qiyama"
 
Ila nyie watu wakatili wa nafsi aiseee...
Kuangalia tuu TBC inahitaji roho ngumu,
Sasa kumwangalia Huyo jamaa TBC inahitaji uwe bandidu na nusu.

Nilienda ugenini, wanaangalia TBC mda wote, Maisha yangu ile jioni yalikua magumu sanaaa, nje kuna mvua, chumbn hakwendeki maana unasubr mwongozo wa wenyeji, kuvaa earphones utaonekana wa ajabu, kuchezea simu mda wote nako hakuleti picha nzuri,
Nilitamani nianze kumchezea paka, bahat nzuri mtoto akaja akawa ananiongelesha.

Mzee mwenye nyumb anashangilia kila kitu, half anakuongelesha u comment...

Nilijitahd kuonesha unafk wa hali ya juu ile siku huku unajichekesha la sivyo naharibu hata kilichonipeleka.

Ila asikwambie mtu unafk wa nafsi yako unachoma moyoo aisee, naondoka huku najishangaa, hv kweli n mm wa kumshangilia yule jamaa...
Nilitamani nikatubu.

Na huwezi ukanishangaa,
Maana haya sasa wewe umesikiliza, ulichoambulia ndio hicho, umefurahia?
kwa maana hiyo wewe kijana kumbe ile siku ulivyokuja kwangu ulikuwa unanichora eeeehh!!!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Rais yuko sawa ila wewe ndiye unayepaswa kupima afya yako ya akili
Akili yangu inaumwa kila nikitafakari mnavyodanganywa na huyo tapeli wa Chato...
Kwanza kwa jinsi nilivoona anakohoa kohoa sidhani kama atatoboa...
Labda awahi dawa za Andre Rajoolina....
 
"...tunawasiliana na Madagascar na wamehaidi kututumia dawa inayotibu covid 19...." JPM [emoji44][emoji44][emoji44][emoji87][emoji87][emoji87][emoji40][emoji40][emoji40][emoji40]

Jr[emoji769]
download.jpg
 
Back
Top Bottom