Rais Magufuli: Maabara Kuu ya kupima sampuli za COVID-19 yaonyesha mafenesi, mapapai na mbuzi yana uambukizi

Rais Magufuli: Maabara Kuu ya kupima sampuli za COVID-19 yaonyesha mafenesi, mapapai na mbuzi yana uambukizi

Taarifa ya uhakika kuhusu wagonjwa corona waliopo hivi sasa hasa baada ya kugundua kwamba idadi iliyotangazwa imehusisha matunda(mafenesi na mapapai) na wanyama kama Mbuzi.

Tunahitaji ufafanuzi zaidi kuhusu matunda(mapapai na mafenesi)haya yaliyotajwa pamoja na Mbuzi. Je kuanzia sasa wananchi hatukiwi kuyala matunda haya pamoja na nyama ya Mbuzi ni ikiwezekana kuyateketeza huku mitaani kwa kuepusha maambukizi zaidi?


IMG_20200503_151649.jpeg
IMG_20200503_151952.jpeg
IMG_20200503_151552.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama haujui wewe ndiye unayeonekana mjinga na kilaza mkubwa na hauna hoja wala point...
Mwenye hoja na point ni mzee wa kujifukiza siyo. Anasema watu waondoe hofu wakati yeye ana hofu ya kunguru!
 
Wanabodi,

Kwa mujibu wa Rais Magufuli wametuma sample kwa kuzipa majina ya binadamu baada ya kupimwa zimetest positive yaani zina corona

Hapa ndipo Magufuli ameprove uwana-science wake.

Magufuli ameonyesha uwezo mkubwa na kushauri nchi zingine zijaribu kupima sample zingine za mimea na wanyama kwa kutumia vipimo vya corona.

Soma hapa > Kutoka Chato: Rais Magufuli amwapisha Mwigulu Nchemba kuwa Waziri wa Katiba na Sheria - JamiiForums

Mkuu GUSSIE nashukuru kwa bandiko zuri. Naomba unitoe kidogo ujinga, hivi nini kinapelekwa kupimwa ili kubaini huyu MTU ameshambuliwa au hajaambuzwa Coronavirus? Naomba wataalam muliopo hapa JF mtutoe tongotongo.

Ahsante
 
Wewe jiulize kwanini watu wanazikwa usiku na wanakataza kupiga picha.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hadi kaona BBC inamsema sana kaamua kuilipua. Huyu mzee hataki udhaifu wake ujulikane. Hata alipokuwa waziri mara nyingi sana JK alikuwa anamgombezaga. Yani ndivyo alivyo na ukimsikiliza unaweza kufa na akakukana vilevile. Yani simuamini hata kidogo na akisema kitu nakipuuza muda huo huo bila kusubiri sekunde!
 
Wanabodi,

Kwa mujibu wa Rais Magufuli wametuma sample kwa kuzipa majina ya binadamu baada ya kupimwa zimetest positive yaani zina corona

Hapa ndipo Magufuli ameprove uwana-science wake.

Magufuli ameonyesha uwezo mkubwa na kushauri nchi zingine zijaribu kupima sample zingine za mimea na wanyama kwa kutumia vipimo vya corona.

Soma hapa > Kutoka Chato: Rais Magufuli amwapisha Mwigulu Nchemba kuwa Waziri wa Katiba na Sheria - JamiiForums
TULISHASEMA VIFAA VYOTE VILIVYOTOKA CHINA VINA MATATIZO HAMKUTUSIKIA....SASA NDIYO HAYO YANAYOTOKEA. TANGU LINI VIFAA VYA CHINA VINAFANYA KAZI VIZURI?
 
Kwani hizo sample zinazopelekwa ni nini damu au kitu gani?

Kama ni damu inamaana Mapapai na mafenesi nayo yana damu?

Nielewesheni jamani huyu Maliyamungu ameshanichanganya

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Vipimo vya korona vimelalamikiwa sana sio na Magufuli tu wewe hauoni kama kuna shida na hivyo vipimo ? Haiwezekani uchukuliwe ute wa papai uonekane una korona
unamuamini sana jiwe
 
Instrument and human error ni kitu cha kawaida katika Sayansi.

Human error inaweza kusababishwa na mpimaji kutokuwa makini au msafirishaji au muandaaji wa sample au mazingira ya utunzaji sample kabla ya kupima.

Instrument error nayo ni kitu cha kawaida. Ndiyo maana hata zile torch za barabarani, mtu akipatikana na speed ya 55, hastahili kuadhibiwa kwa sababu torch ina maximum error 10%. Kwa hiyo inaposoma 50km/hr, inaweza kuwa 45 au 55km/hr. Askari wasioelewa huwa wanadai eti amekusamehe. Kitu ambacho siyo kweli. Vifaa vingi vya kisayansi huonenesha percentage error (plus or minus). Na baadhi ya vifaa hutakiwa kufanyiwa re-callibration kila baada ya idadi fulani ya readings.

Kama hupeleki samples nje ya nchi yako, na una mashine moja tu, utawezaje kuhakiki ubora wa readings zako? Kisayansi, unahitaji kuwa na mashine angalao kiwango cha chini 3, lakini ni vema zaidi kuwa nazo 5. Kila baada ya readings idadi fulani, samples teule zinatakiwa kupimwa na maabara zote 5 ili kuona kama zote zitaleta majibu yanayofanana. Zile/ile ambayo inatofautiana na nyingine, inafanyiwa re-callibration.

Alichokiongelea Rais, kwa vipimo vya kimaabara, siyo jambo la ajabu.

Ushauri - tuongeze vipimo. Na sasa hivi vipo vipimo vya kisasa ambavyo ni automated. Vinatoa majibu haraka zaidi na vinapunguza human error.

Lakini hata kama vipimo vikiongezwa, kama maabara hazina utaratibu wa kufanya uhakiki kila baada ya muda fulani, haitasaidia kitu. Lakini nijuavyo, huwa wanakuwa na control samples kwaajili ya kucheck accuracy ya vifaa kila baada ya idadi fulani ya readings. Na kama ukiwa na control samples, huna haja ya kutumia mashine nyingine kuhakiki ubora wa kipimo chako maana una uwezo kuhakikisha mwenye kwa kuitumia mashine yako hiyo moja.

Observation aliyoisema Rais ni njema, japo kauli ya kusema kuna watu wanatumiwa, siamini kama ilikuwa sahihi. Tuwafikirie kwa mema wataalam wetu mpaka pale wanapotudhirisha kuwa imani yetu kwao haikuwa sahihi. Na pia Rais ameharakisha mno kuyatamka aliyoyatamka. Alikuwa na uwezo wa kuelekeza queries zake kwa wahusika. Kama anataka, baadaye angekuwa kuwaambia wananchi matatizo yaliyokuwepo na suluhu iliyopatikana. Siyo kuja kulalamika kwa raia wakati hajapata majibu ya wataalam.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nashangaa anawalaumu waliokuwa wanapima kule maabara ya kitaifa kuwa wanamhujumu, kwa kutoa matokeo positive Ya corona, anadai kuwa walionekana ni positive ni uongo, eti alipeleka sample Ya Mbuzi, papai, na vitunguu eti wale watu Wa maaabara ya taifa walimuhujumu, eti na hizo sample hao wa maaabara Walisema ni positive aiseee anaone kuwa hakuna corona anasema hata ligi ya mpira atairuhusu iendelee aisee huyu mzeee akishindwa Jambo anasingizia mabeberu na kuwa anazungukwa, yani hahahahaha, Halafu nashangaaa anaenda anasema corona kweli ipo halafu anasema vipimo ni vya uongo watu waliokuwa wanapima wachunguzwe yani mmmmh simwelewi

Sent using Jamii Forums mobile app
Asa tukusikilize wewe au?
 
Dunia kwa sasa kuna changamoto kubwa ya kupambana na Corona Virus Disease of 19, ni kweli wengi wameambukizwa na wengi wamefariki kutokana na ugonjwa huu. Familia zimepotea wapendwa wao wengi na chumi za mataifa mbalimbali kuzorota kutokana na ugonjwa huu. Pia shughuli mbalimbali za kijamii na kitaaluma kutoendelea kama ilivyo kawaida.
Katika mapambano yoyote kuna askari walio mstari wa mbele, katika ugonjwa huu wataalamu katika sekta ya afya ndio askari wetu wakuu. Wameamua kuyaweka maisha yao rehani ili tu kutupambania.
Wataalamu wa maabara ni sekta muhimu sana katika mapambano haya ya COVID-19, nasema wao ni muhimu kwani majibu yao ndio msingi wa mapambano yenyewe. Kukiwa na tishio la ugonjwa huu kuendelea na chanjo au matibabu kutopatikana mapema, ni kweli askari wetu wa maabara wanatakiwa kuja na majibu ya kuridhisha ya namna ya kutafsiri majibu ya kiamabara.
Katika mapambano ya COVID -19, tunategemea sana kifaa kinachoitwa RT-PCR ambacho kinapima RNA au vinasaba taarifa vya kirusi chenyewe cha CORONA.
Kifaa hiki si hitimisho la kusema kuwa mtu huyu ana ugonjwa wa COVID-19 au ni mtu tu anayeishi na maambukizi ya corona.
Naomba hapa mnielewe kuwa si wote watakaokutwa ni chanya kwenye kipimo hiki cha Corona basi wanaumwa COVID -19.
Mgonjwa wa COVID-19 no yule tu mwenye dalili za ugonjwa na akiwa na hizo dalili na kipimo kuonesha kuwa yupo chanya kwa vinasaba taarifa vya COVI-19 ndio tunasema yeye ni mgonjwa wa COVID-19.
Siyo wote watakaokutwa ni chanya kwa vinasaba taarifa RNA vya COVI-19 basi ni wagonjwa, wengine ni kuwa inawezekana miili yao imeshapambana na kirusi hiko na kukififisha, hivyo kutokuwa na ugonjwa kitaalamu wanaita "active disease". Aidha kila kipimo kina sehemu yake na kuwa na majibu chanya yasiyo halisi (False postive) au majibu hasi yasiyo halisi (False negatives)
Pia siyo wote watakaokutwa ni chanya ni wagonjwa, kwani wengine miili yao inakuwa imehifadhi tu taarifa ya kuwa katika kipindi kimoja ama kingine walishwahi kuwa na virusi hivyo mwilini mwao.
Yule mwenye dalili tu ndio mwenye "active disease".
Sasa tunakuja kwenye swali la msingi, je taaluma ya maabara imeshindwa kuja na kipimo cha kuweza kutofautisha baina ya mgonjwa na wale ambao si wagonjwa?
Je dunia nayo imeshindwa kutofautisha makundi hayo hapo juu.
Ujumbe wa leo ni kuwa bado dunia haijaweza kumfahamu vizuri huyu kirusi COVI-19, bado tupo kwenye mashimo yaliyo na giza. Hakika tunahitaji sasa wana taaluma wa maabara na wanasayansi wengine duniani kuja na majibu ya hakika ya kuweza kutofautisha wagonjwa wa COVID-19 na watu wanaoishi na maambukizi ya virusi vya Corona -19.
Hakika tumebaki kwenye mtanzuko, je ni nani wa kutohokoa?

Sent using Jamii Forums mobile app
Mtaalamu sio huyo amewahokoa leo
 
Huyu mtawala anachekesha hivi kama aligundua kuwa matokeo ya nasal and mouth swap yana
mashaka yeye kama kiongozi mkuu wa nchi alichukuwa hatua gani?
Ilikuwa yeye atuagizie test kits zilizo sahihi badala ya yeye kulalamika kana kwamba ni mpita njia.
Mbona huku nyuma alikuwa anaingilia kila idara na kutatua matatizo mara mmoja.
Au yeye kama mkemia PHD holder atengeneze test kit yake.Kwani wanaotengeneza kits hizo wanatokea sayari nyingine?
Tumechoka na drama.
 
Mkuu umemwelewa vyema rais, alijaribu kupata weledi wa vipimo vinavyotoka maabara kuu na hayo ndiyo majibu. Wanajiandikia tu Positive na Negative.

Leo ndio nimegundua waTanzania 90% mitandaoni ni wajinga na wapumbav na kuanzia leo napunguza uchangia mada kwa 90% kwani huwa naongea na wajinga wasiojielewa.
Una uhakika gani alichosema jiwe ni kweli, huwezi sema 90% ni wajinga utuombe radhi. Huwezi sema wanajiandikia tu positive na negative labda vifaa ndivyo havina accuracy na precision inayotakiwa na hii inaweza sababishwa na mambo mengi. Kiufupi jiwe aaminiki kwa kiwango hicho. Watu wa maabara lazima wavalidate vifaa vyao against known standards. Kiufupi kuna kitu hakiko sawa toka kwa hotuba ya leo.
 
Huyu mtawala anachekesha hivi kama aligundua kuwa matokeo ya nasal and mouth swap yana
mashaka yeye kama kiongozi mkuu wa nchi alichukuwa hatua gani?
Ilikuwa yeye atuagizie test kits zilizo sahihi badala ya yeye kulalamika kana kwamba ni mpita njia.
Mbona huku nyuma alikuwa anaingilia kila idara na kutatua matatizo mara mmoja.
Au yeye kama mkemia PHD holder atengeneze test kit yake.Kwani wanaotengeneza kits hizo wanatokea sayari nyingine?
Tumechoka na drama.
Sema umechoka ebho
 
Back
Top Bottom