Rais Magufuli: Mshahara wangu kwa Mwezi ni Sh. Milioni 9.5. Nitatoa salary slip...

Tatizo ni pale mnaposhindwa kutofautisha kati ya chuki na kukosoa,kuna watu wanamchukia Magu ndio hao muda wote hueleza mabaya hukuti wakimzungumzia Magu kwa jambo lengine tofauti na hayo mabaya ambayo wanaita kukosoa. Wameshindwa kujua kuwa kinachowasukuma ni chuki na huwezi kuona au kuzungumza zuri kwa unayemchukia.
 
Kwanza kabisa nani anamlipa?
Sie ambaye tumepanga na tunadaiwa kodi ndio tunamlipa yeye mshahara hiyo milioni 9 huku sie wenyewe tunalipwa laki mbili na tunagharamia maisha yake ya kifahari pale ikulu yeye anakula na kulala wala hatumii hiyo milioni 9 tunaomlipa. Ila sie hiyo laki mbili ndio tulipe kodi,tulipe matibabu na hiyohiyo tule.

Ni upumbavu wa hali ya juu.
 
Mazuri yakiwa mengi hufunika mabaya lakini sasa mabaya ni mengi kuliko mazuri ndiyo maana mazuri hayaonekani kwa haraka, mfano hayo mazuri ni kuleta maendeleo kwenye SGR bwawa la umeme flyover ununuzi wa Ndege nk lakini huko napo kuna ufisadi mkubwa mno, Pesa inacheleweshwa kwenye SGR mpaka baadhi ya makandarasi na watu wanaosambaza vifaa wamefungua kesi mahakamani, hapo napo watu wakisema utasema wana chuki na magufuli? tena magufuli angejua angekuwa anaishukuru JF kwa jinsi inavyojitahidi kumsaidia kujua mapungufu yake kwa undani kabsa
 

[emoji23]watu ni wajinga sana aisee yani hata hawajiongezi mkuu, yani jiwe ajilipe mshahara kidogo hivo yani hata “mambokale” mshahara wake ni zaidi ya 9mil
 
Akili yako ni kwaajili ya matumizi yafuatayo;
1. Kukitambua choo na kukitumia
2. Kutambua kitanda na kuweza kulala
3.Kuutambua ubwabwa na kuula
4.Kumtambua samaki na kuweza kumla.
Basi.
Hivi kwaakili zako ni bodi gani Tanzania inaweza kukaa na kumpangia mkurugenzi mshahara mkubwa kuliko Rais?
Hivi unadhani bodi ikipanga mshahara hakuna authority nyingine inayoruhusu huo mshahara kuanza kutumika.
Kweli mtaji wa CCM ni wajinga , wapumbavu na maskini.
 
Ebu agiza maji baridi hapo kwa mangi ntalipa alafu punguza jaziba

Life is not fair nadhani unajua hilo hivyo tulia tuu ndo uhalisia

Mimi nimeongelea mshahara wala si marupurupu ya ofisi ya urais elewa aiseee
 
Ameonyesha salary slip maana huu ni mwaka wa nne sasa toka aahidi mzee wa propaganda .
 
Mpuuzi wewe, hivi hujui kama jiwe anajilipa bilioni 1.2 kila mwezi kwaajili ya MATUMIZI BINAFSI (kupitia ofisi ya rais, ambazo ndio anatumia kununulia jogoo kwa laki moja n.k) mbali na mshahara na marupurupu yote anayopatiwa kupitia kado zetu?
 
peleka taarifa kwa mhe. Jafo au Mhe. Silinde naaamini hao mafisadi watashukiwa kama mwewe,
 
Posho zingine na marupu rupu kataja?
Naweza kusema huyu Anko ni mzalendo sana, sijui kama kuna Rais mwingine Afrika anayelipwa hela kama hii.

Anko Magu analipwa mil. 9 tuu. Kiasi ambacho ni kidogo kuliko hata mshahara wa wabunge ambao wao hulipwa mil 12...
 
Mshamba tu wewe.
 
Akili za kuambiwa changanya na zako.

Kama aliweka kila hila kwenye manunuzi ya ndege alizonunua zisikaguliwe na CAG ndo ataweza kukutangazia wewe figure yake halisi ya mshahara wake?

Kama ni mkweli aweke salary slip kila mtu aone na approve sio blah blah tu.

Kama kuongea kungekuwa ni kuthibitisha uhalisia uliopo basi tungeamini katika yale magari yaliookotwa bandarini
 
Nikikosoa unasema nina chuki

Nyie yeyote anaekosoa chochote cha Magufuli mnasema ana chuki binafsi as if nimemtukania mama yake au familia yake..
Naona sasa unanichamba kabisa.

Wewe unachanganya vitu,nimekwambia mimi namkosoa magufuli si kwa sababu namchukia bali nimeona amekosea ila pia naweza kumpongeza napoona amefanya vizuri na si kwamba nampenda au nina mshabikia. Sasa hilo ni jambo la kwanza na jambo la pili huwa mara nyingi nawakosoa watu kama nyie ambao mnaongozwa na chuki mnashambulia watu na kwa sababu ya chuki huku mkidai mnakosoa.

Kwenu nyinyi wanaokosea tu ni Magu na wana ccm wote,wengine wakikosea hamuwakosoi sana sana mtabariki hayo makosa kwa kukumbushia makosa mfano wa hayo yaliyofanywa na maccm na atakaye wakosoa(hao ambao nyie hamuwezi kuwakosoa) mnamshambulia na kumwita ni kuwa ni ccm.

Ndio maana nasema haupo huru maana hiyo chuki inakunyima uhuru,wewe huwezi kumzungumzia Magufuli kwa mazungumzo yasiyohusu mabaya ya Magufuli, kwako wewe Magu ana mabaya tu na hiyo ni dalili ya wazi ya chuki na ukiona mtu anampongeza Magu unaona ni mwanaccm au anafaidika na utawala wa magu hayo yote ni kwa sababu ya chuki hauamini kuwa magu ana jambo la kupongezwa au hautaki tu kuona akipongezwa.

Binafsi sijawahi kumchukia pamoja na kwamba kuna mambo anafanya ambayo si sahihi lakini pia sijawahi kuwa mshabiki wa magu humu.
 
Naweza kusema huyu Anko ni mzalendo sana, sijui kama kuna Rais mwingine Afrika anayelipwa hela kama hii.

Anko Magu analipwa mil. 9 tuu. Kiasi ambacho ni kidogo kuliko hata mshahara wa wabunge ambao wao hulipwa mil 12...

Unawezaje kuwalinganisha watumishi wa kawaida na mtumishi ambaye hana personal living expenses zozote (i.e., gharama zake zote ni burden ya walipakodi)?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…