Naweza kusema huyu Anko ni mzalendo sana, sijui kama kuna Rais mwingine Afrika anayelipwa hela kama hii.
Anko Magu analipwa mil. 9 tuu. Kiasi ambacho ni kidogo kuliko hata mshahara wa wabunge ambao wao hulipwa mil 12.
Leo kwenye hafla ya kumwapisha Naibu waziri wa Madini, Mheshimiwa Rais alijikuta akitaja kiasi anacholipwa wakati akiongelea suala la mishahara ya watumishi waliokuwa TMA baadae kubadilishiwa sekta, watumishi hao ambao Rais alidai waliboronga huko TMA wanapaswa wasilipwe mil 10 tena mishahara yao ipunguzwe na kuongeza kuwa asiyetaka aache kazi. Maana kuna wengine wanalipwa mishahara ya ajabu sana.
Kwa mshahara huo wa Magu watumishi wengi mno wenye mshahara kumzidi, nashawishika kusema kuwa Rais Magufuli ana mabaya yake lakini ni Rais bora sana kwenye mambo mengi.