Rais Magufuli: Mtu akipotea, marufuku kuhusisha vyombo vya Dola, utakamatwa na utoe ushahidi

Rais Magufuli: Mtu akipotea, marufuku kuhusisha vyombo vya Dola, utakamatwa na utoe ushahidi

Hapo sawa kabisa maana vyombo vyetu vinachafuliwa hovyo
Ili visichafuliwe, inabidi vionyeshe kuwa havishiriki kufanya vitendo hivyo.

Na watu wanapopotea vyombo hivyo vionekane kufanya kazi ya kuchunguza matokeo hayo na kuzuia mengine ya aina hiyo yasitokee.

Kutofanya hivyo, maana yake ni kwamba vyombo hivyo vinashiriki katika uovu huo.

Mbinu ni zile zile anazotaka zitumike. Watishie wananchi wanyamaze, ili ufanye unavyotaka bila ya wananchi kukubughudhi.

Ukipotelewa na ndugu, utasita hata kwenda polisi kutoa taarifa ya kupotelewa.

Sisi tutakuwa ni taifa la namna gani sasa!
 
Tatizo mnawajumuisha wote ili hali unakuta wengine hata hawana habari, kama yule Kamanda wa Kinondoni alivyolazimika kujitoa mwenyewe lawamani kwenye sakata la Tito Magoti.
 
Salary Slip,
hapa sasa ni sawa na kutaka Gwajima awe anatoa adhana kwenye msikiti wa kwa Mtoro au yule shehe wa Dar aanze kupata vipindi vya mahubiri Azania Front!!
 
Ama kweli hii ndio 2020 utake usitake lazima tuburuzwe mpaka siku tukijitambua kuwa sisi ni akina nani
 
Return Of Undertaker,
Ningeulizwa Mimi, angestahili aseme - Serikali itafuatilia jambo hilo ikishirikiana na taasisi za kimataifa, na itakapogundulika katekwa, basi waliomteka wachukuliwe hatua bila kujali ni nani kahusika, na ikigundulika hakutekwa bali kadanganya, basi achukuliwe hatua pia.

Hili la kusema vyombo husika visilifumbie macho, naona kama anawaunga mkono wahusika kwani kwa sehemu kubwa hivyo vyombo ndivyo vinalaumiwa kuhusika.
 
Back
Top Bottom