Nimefuatilia comments nyingi kwenye hii thread nilichogundua ni kwamba matatizo yatokanayo na huduma za TTCL ni mengi ila nadhani kuna uwezekano matatizo yote yanasababishwa na kitu kimoja au viwili tuu. Ni muhimu TTCL watambue shida inayopelekea kuzalishwa kwa haya matatizo lukuki ili wayape dawa ya kudumu.
Tunaweza kulalamika hapa tukatoa mapendekezo tele lakini kama hayatagusa mzizi wa matatizo tutalalamika bure miaka yote na kumaliza mabudle yetu na kuchakaza sim zetu bila suluhu
Ila kitu kimoja nimefurahi kuona uzalendo wetu watanzania, bado tunaipenda kampuni yetu, bado tunatamani kupata huduma zake na bado tunaamini wakibadilika wataweza kutoa huduma bora. TTCL waitumie hii nafasi kuwaonyesha watanzania kweli wamewasikia na wanaweza