Binafsi nampongeza Sana Kindamba ameleta mageuzi makubwa Sana TTCL,kutoka kuzalisha hasara kwa miaka 18 iliyopita mpaka kutengeneza faida na kutowa gawio kwa serikali.sikatai kwamba ttcl Wana changamoto zao especially za kiubunifu mfano kwenye bando zao bado wamebase kwenye watumiaaji wadogo wa data na voice mfano kwenye data ukiangalia bando zao nyingi mb200 mb500 1gb zikizidi Sana 5gb kwa mwezi ni kweli kwamba Bei zao ziko fair ila wawalenge na watumiaji wakubwa kuanzia gb 5 na kuendelea mpaka gb 100 kwa mwezi.
Kwa Bei nzuri maana kwanza ttcl ndo wanamiliki mkonga wa taifa kwahiyo hata iyo mitandao mingine wanawauzia wao ili waweze kusafirisha data zao huko kuwafikia watumiaji wa mwisho kwahiyo ttcl bando zao zinatakiwa ziwe chini kuliko mitandao mingine ili kuvutia wateja. Kingine ttcl iongeze upatikanaji wa vocha ni kweli unaweza kununua vocha kwenye simu na mitandao mbalimbali lakini Kuna yule mtu wa kijijini kabisa hajui ilo ameshazoea vocha za kukwangua kwahiyo waliangalie na Hilo.
Pia waongeze matangazo, kindamba najua unapenda kusave Ela ili kuongeza faida lakini sio kwenye matangazo jitaidini Sana kuongeza matangazo kila mahali mf, kwenye tv,barabarani,toweni ata Ile miavuli vile vile kwenye tpesa tumieni Ile njia ya Airtel money ya hakati mtu ikisha kubalika zaidi ndo mnaweka charges kidogo.kingine Kuna Huduma nyingi za ubunifu mfano Kuna wale wateja wa uhakika watengenezeeni Huduma ya post paid na prepaid tengeneza package za uhakika za mwezi mkilenga voice na data then mnafanya ka research kadogo then mnatengeneza hiyo.mkizingatia ivyo hamna mitandao utakao wazuia
The Black Godfather,
Sent using
Jamii Forums mobile app