Mkwara wa Kabudi ulisaidia sana, MABEBERU yakisikia sauti ya mzalendo Kabudi yanaingia hadi chini ya meza kwa uwoga MABEBERU yaliposikia ya kwamba na sisi tumekuwa DONA KANTRE yaliona aibu sana, kongole kwa mawakili wetu
Naambiwa zilionyeshwa hadi picha za utawala katili wa makaburu ambao mkulima naye katokea huko. Vile vita vya korosho tulivyoshinda kwa kutumia jeshi mahiri kabisa duniani viliwatisha MABEBERU HAYO ya Canada yakaona bora yaishe. Mkwara wa Profesa Kabudi kuacha kutoa order za ndege Canada ulisababisha mamia na maelfu ya wacanada kuandika petition kwamba ndege iachiwe maana speed ya Tanzania kununua midege kwa cash tena na mengine yanakuja ni faida kwao na ajira nchini mwao hivyo wakihamia Brazil itawacost sana
Mawakili wetu pia wa li shine sana mahakamani,ilichukua dakika 20 tu judge Smith ku dismiss case huku mkulima akingua kilio na kuambulia patupu. Hongera sana awamu ya tano kwa kushinda kesi na kuwezesha mawakili kuwa na kiwango cha kimataifa
Hongera awamu ya tano kwa kumtoa Profesa Kabudi jalalani bila yeye sijui ingekuwaje kwa kweli, hongera sana mtukufu two phd's holder dr John Pombe Joseph Magufuli. Dege la nane linatua Mwanza ambapo nataarifiwa jiji limezizima likiisubiria kwa hamu kubwa na mapokezi hayo yanatarajiwa kuwa livestreamed nchi zaidi ya 75 duniani ambapo wengi wanashangazwa na KASI KUBWA NA KISHINDO KIZITO cha awamu ya tano kama vile ujenzi wa ma flyovers, viwanda 4000 ndani ya miaka 4, viwanda 100 kila wilaya, zahanati 357 nchi nzima, haijawahi kutokea dunia nzima inashangazwa na kumkubali sana DR JOHN JOSEPH POMBE MAGUFULI