Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,843
- 31,057
Nilimsikia Rais Magufuli, katika mkutano wake wa kampeni hapo Jana, huko Bagamoyo mkoani Pwani, akiwaahidi wafanyakazi kuwa atawaongeza mishahara yao wafanyakazi hao, iwapo watamchagua tena katika uchaguzi mkuu ujao!
Hivi si ndiyo huyu huyu Rais Magufuli amekuwa akigoma katakata kuongeza mishahara ya wafanyakazi, kila amapoonbwa na viongozi wa vyama vya wafanyakazi kutokana na kupanda kwa hali ya maisha kwa wafanyakazi hao, katika kila sherehe za Mei Mosi, kila mwaka tokea aiingie madarakani mwaka 2015, akidai kuwa hawezi kuongeza mishahara wafanyakazi, kwa kuwa katika kipindi hiki anajenga miundo mbinu mikubwa ya reli ya SGR na bwawa la umeme la Stieglers Gorge?
Wakati Rais Magufuli amekuwa akigoma katakata kuongeza mishahara ya wafanyakazi kwa sababu hizo zisizokuwa na mashiko hata kidogo, marais wenzake wote waliomtangulia walikuwa wakiwaongeza mishahara yao wafanyakazi, pamoja na marais hao pia walikuwa wakiendelea kujenga miundo mbalimbali hapa nchini
Hivi Rais Magufuli kutoa ahadi hiyo wakati huu wa kampeni, anatugeuza sisi wafanyakazi wa nchi hii ni wajinga mno na tunaoweza kudanganyika kirahisi hivyo?
Sisi wafanyakazi wa nchi hii, hatudanganyiki tena na Rais Magufuli na tuna jambo letu ambalo tutalitimiza ifikapo Oktoba 28 mwaka huu kwenye sanduku la kura kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu.