Uchaguzi 2020 Rais Magufuli ndiyo anaibuka kuwa atawaongezea mishahara wafanyakazi. Tunamwambia kuwa hatudanganyiki ng'oo

Amesema ataongeza lakini hajasema atawaongezea kwa asilimia ngapi...

Hahah nitacheka sana pale watu watapopata ongezeko la 0.1%
 
Jeshi la Polisi la CCM kwa siku kadhaa sasa limeendelea kutoa vipigo vya haja kwa Wafuasi wa ACTwazalendo huko Kisiwani Pemba

Wananchi wengi sasa wamekimbilia vichakani bila chakula wala maji.Viongozi wa ActWazalendo wamezuiwa kwenda msituni kuwaona wafuasi wao.

Ndugu Srro jeshi lako limeshapoteza sifa ya kuwa jeshi huru lisilokuwa na Chama kwenye kuwahudumia Wananchi
 
Aliwatapeli watumishi 2015, sidhani kama kuna mtumishi mwenye akili timamu atamwamini na kumpa kura
 
Wafanyakazi wa umma ndio kundi la wasomi wa nchi hii, hivyo wana uwezo kutunza kumbukumbu za machungu yote waliyoyapitia! Watakumbuka ni huyohuyo aliwaambia mwenye anaona mshahara wa serikali ni mdogo aache kazi akalime! Kila wakati kwa miaka 5 alitoa sababu kuwa hawezi kupandisha mshahara kwakuwa anatekeleza miradi ya maendeleo bila kujali kuwa wafanyakazi hao pia wana miradi yao ya maendeleo kama kujenga, kusomesha n.k!

Huwezi kumwambia mtu eti hutaongeza mshahara wake sababu unatoa elimu bure, unatoa mikopo ya elimu ya juu, Hivi nani alisema elimu ina mwisho? Kama ni kwasababu hizo basi kudumaa kwa mshahara wa wafanyakazi itakuwa ni moja kwa moja labda ije serikali mpya kabisa! After all hiyo miradi yote aliyoitolea kama sababu ina bajeti yake nje kabisa ya bajeti ya mishahara ya watumishi, shida tu ni kutoheshimu taratibu za kabajeti katika matumizi ya fedha za serikali!

Watumishi shikamaneni, chagueni rais atakayejali maslahi yenu, kumbukeni jasiri huwa haachi asili, huyu hata akirudi tena mstegemee jipya!
 
Rais wangu uncle Magu naona maji yamekufika shingoni ,Lisu anakuandama na anaonekane yupo kwenye right track kuliko wewe, hakuna anayetambua impact ya hiyo miradi yako mikubwa kuliko mambo yanayogusa jamii moja kwa moja,kama tetemeko la Kagera, njaa mafuriko nk wakihitaji msaada wa serikali yako lakini ukawajibu makavu ,eti serikali haikuleta tetemeko, serika haina shamba n.k.wakulima hali si hali ,wafanyakazi kwa miaka mitano hujaongeza eti kupunguza payee kwa 2% ndio ongezeko hiyo ni sawa Tsh 6000 kwa anayepokea 300000/= kwa muda wote,na kila mara unawaambia nitaongeza wakati nakaribia kumaliza muda wangu.

Sasa unaposema utawaongezea leo ni kiasi gani au % ngapi na lini? Usipowapa hayo majibu ni ngumu kupewa kura na watumishi na wategemezi wao,kwani yaweza kuwa danganya toto kama ulivyoahidi kila kijiji 50,000,000/= na waalimu kompyuta katika kampeni ya 2015 lakini hakuna utekelezaji.

Mwisho kwakuwa tume sio huru kivile na labda ukashinda na bila kuwaridhisha watanzania hasa wakulima na wafanyakazi pia sekta binafsi ujue 2025 utaipa anguko kubwa CCM.Atakeye kurithi atapata wakati mgumu.
 
Kasema akiingia tu ikulu tena,ananunua ndege zingine.
Aende kununua ndege huku sisi mishahara ni ileile?kama ndege na barabara ndio ilimfanya asiongeze mishahara kwanini bado ndio kauli mbiu yake?
 
Sikiliza hii:

Huyu Magufuli ni mwongo na mnafiki haijawai tokea. Sikiliza hii:

Sikiliza kauli yake hapa:

Kiukweli hizi clip zingekuwa zinarushwa kama zamani kwenye ma group ya whatsap,Facebook hali ingekuwa mbaya zaidi ya sasa!
Watu wangewasikilizisha mpaka wazazi wao huko vijijini.
 
Kasema ataongeza mishahara kwa wafanyakazi. Mi5 tena kwa JPM
Akawadanganye hao Mafisi wenzake wa Lumumba!!
Magufuli alishawaambia WATUMISHI HAWEZI ONGEZA MISHAHARA MPAKA AKAMILISHE MIRADI YAKE YA FLYOVERS, UBUNGO INTER CHANGE, STIEGLERS GORGE, SGR, etc.
Hemu atuondolee upuuzi wake buana!!!
 
Nilimsikia Rais Magufuli, katika mkutano wake wa kampeni hapo Jana, huko Bagamoyo mkoani Pwani, akiwaahidi wafanyakazi kuwa atawaongeza mishahara yao wafanyakazi hao, iwapo watamchagua tena katika uchaguzi mkuu ujao!

Maji yakifika shingoni unaweza kujishika hata kwa utandu wa buibui
 
Muulize Mbowe kwanini uwanja wa Kia uko mbali na mlima kilimanjaro na ngorongoro
Hiyo ndiyo hasara ya kuandika uzi usio na mashiko ukihisi wasomaji wote wa JF ni vilaza wa kucheza wimbo wasioujua.
Revise and be wise otherwise no rise.
Karibu lunch hapa Tips Kiongozi
 
Akawadanganye hao Mafisi wenzake wa Lumumba!!
Magufuli alishawaambia WATUMISHI HAWEZI ONGEZA MISHAHARA MPAKA AKAMILISHE MIRADI YAKE YA FLYOVERS, UBUNGO INTER CHANGE, STIEGLERS GORGE, SGR, etc.
Hemu atuondolee upuuzi wake buana!!!
Kwa taarifa yako haijawahi kutokea Rais mkweli na mzalendo na mwenye mapenzi ya kweli kwa watu wake wote. Niwakumbushe aliwaomba wafanyakazi wavumulie hapo aliwapa ukweli ikiwa ni namna bora sana ya kuheshim wafanyakazi.

Pili alisema anapenda kuongeza mishahara minono na wala siyo ile ya nyongeza ya buku tano, ile ulikuwa dharau kubwa wafanyakazi wenyewe wanafaham hilo. Ikymbukwe kwamba unapoamua kujenga uchumi ni lazima upunguze matumizi.

Wafanyakazi wanafaham japokuwa mishahara haijapanda lakini kodi ya mishahara iliendelea kupunguzwa kwa kiasi kikubwa. Mfumuko wa bei umezibitiwa sana jambo ambalo limesaidia wafanyakazi kumudu ununuzi wa bidhaa za sokoni kwa kipndichote.

Sasa uchumiwetu unapaa juu na mishahara inaenda kupaa. mpaka wafanyakazi wa nchi jirani watapata wivu amini usiamini. Magu mi5 tena kazi iendelee.
 
Sisi Wafanyakazi wa Serikali tuliodhulumiwa nyongeza ya Mishahara katika Miaka mitano ya Huyu Mhutu, huku tukifukuzwa kazi hovyo na kutukanwa, tutamnyoosha tarh.28 wiki ijayo, Hatutaki Ujinga
 
Kwa kweli apige zaidi spana had Maji ayaite Mmaa. Sasa hivi tayari yupo desperate kila ahadi nzuri za Lissu naye adandia na kuahidi kama vile hakuwahi kuziahidi.

Wale wawasha mitambo wake wote Jamii imewapuuza wamebaki Kufokea watu Tu.
Haha ukisikiliza ya huku mtandaoni, unaweza ukadhani hata kwenye mikutano yake (Magufuli) watu hawaendi.
 
Sisi Wafanyakazi wa Serikali tuliodhuliwa nyongeza ya Mishahara katika Miaka mitano ya Huyu Mhutu, huku tukifukuzwa kazi hovyo na kutukanwa, tutamnyoosha tarh.28 wiki ijayo, Hatutaki Ujinga
Inawezekana wewe ni familia masamaki wa nyumba 70 sikushangai ukimchukia JPM endelea kulia lakini 28/10/2020 kura za heshima kwa JPM nyingi mno.
 
Hyu ni muongo, tena asiwadanganye.
Kwanza hana hawapendi watu anapenda vitu, hasa maujenzi.
Aseme kimara _ mbezi atawalipa fidia lini
 
Hiyo ndiyo hasara ya kuandika uzi usio na mashiko ukihisi wasomaji wote wa JF ni vilaza wa kucheza wimbo wasioujua.
Revise and be wise otherwise no rise.
Karibu lunch hapa Tips Kiongozi
Peleka misosi hiyo kwa waliberali wenzio
 
Tupigieni kura,tayari fungu la kuwaongezea mishahara lipo,,wasiwasi wenu nini kwani?,tuaminiane...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…