Rais Magufuli: Niliwahi kuwa dereva wa teksi bubu

Hahaaaa
Nakumbuka hata mimi alinipeleka msasani, ila bahati mbaya tulidaiana chenji alipaswa kunirudishia jero (Tsh 500) kwa sababu alinicharge Tsh 2,500 na mimi nilitoa Tsh 3,000 yaani noti 3 za Tsh 1,000

Basi tuliposhindwana dereva huyo wa Tax bubu ambae alikuwa mwanafunzi wa UDSM ikabidi anirushe alipo nichukulia pale ubungo kona ya chuo lucha ya kuwa nilikubali kumuachia lile Jero lakini aligoma kwa madai kwamba yupo kwenye vita ya uchumi na Mabeberu wapanda Taxi

Kwakweli hii vita yake ya kiuchumi na mabeberu wapanda Taxi kaianza muda mrefu sana nafikiri mnakumbuka hata wakati akiwa waziri, ase!!! maamuzi yake ya hovyo na jeuri bila busara yapo kwenye damu tangu akiwa Tax driver pale Ubungo [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] haki sinto sahau !!!

MITANO TENA!!!
 
Kilele cha Maisha ni lazima kiwe na historia bhana cha mambo mtu ameyafanya na kukutana Nayo kabla ya hapo
 
Rais Magufuli ametoa siri hiyo leo wakati akizindua daraja la la Ubungo lililopewa jina la Kijazi Interchange.

Rais Magufuli amedai kuwa alipokuwa mwanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es Salaam alikuwa akipiga kibarua cha kuendesha teksi bubu ili ajipatie chochote kitu. Na kituo alichokuwa anapaki ni jirani na lilipojengwa daraja hilo la juu mahsusi kupunguza foleni.

Rais Magufuli amesema kazi ya urais ni ngumu sana maana pamoja na kuwa na hamu ya kuendesha gari lakini huwa anakatazwa na kuzuiliwa.

Mbali ya hayo rais wa JMT amesema kuwa maendeleo huwa wakati mwingine yanakuja na vikwazo sababu wakazi wa maeneo ya Ubungo mpaka Mbezi mwisho walichukia kubomolewa nyumba zao pamoja na kuwa zilikuwa ndani ya hifadhi ya barabara.

Rais Magufuli amesema sheria ni Msumeno ndio maana hata jengo la Serikali ambalo ni mali ya Tanesco lilivunjwa japokuwa aliyekuwa waziri mkuu kipindi cha awamu ya nne ndugu Mizengo Pinda hakuamini kama litakuja kuvunjwa.

My take: Wakazi wa Dar es Salaam waambieni watoto wenu wasichague kazi. Kutwa wanashinda vijiweni wanajadili habari za Simba na Yanga,Diamond na Zari huku wakibweteka. Miaka ya nyuma mtu unapiga deiwaka ya udereva teksi huku unasoma.

Kuwa Tax bubu kumbe na yeye alikuwa mvunja sheria!!!??
 
Akiwa UDSM tayari alishakuwa Mwalimu.
Aache usanii huyu Mzee
 
Back
Top Bottom