Rais Magufuli: Niliwahi kuwa dereva wa teksi bubu

Rais Magufuli: Niliwahi kuwa dereva wa teksi bubu

Mimi nilikuwa naenda ziwani kuvua dagaa wakati nikiwa mtumishi wa Umma....nilidhani navunja rekodi kabla sijakutana na mwalimu wa sekondari ya serikali (A level) akiwa mchimbaji mdogo wa dhahabu....anaingia shimoni usiku kesho yake asubuhi yupo zake class!
Uzi huu umenifanya niamini kwanini JF imejaa watu wa kulalamika na kukosoa tangu jua linachomoza hadi wanaenda kulala!
 
My take: Wakazi wa Dar es Salaam waambieni watoto wenu wasichague kazi. Kutwa wanashinda vijiweni wanajadili habari za Simba na Yanga,Diamond na Zari huku wakibweteka. Miaka ya nyuma mtu unapiga deiwaka ya udereva teksi huku unasoma.
Na hiki ndicho kilema kikubwa kwenye kizazi hiki, wakati wengine wakikesha kutafuta maisha wengine wanakesha kwenye mijadala ya Simba na Yanga, leo Diamond ametoka na gari nyekundu and the like, sijui ni nani atakuja pindua hizo fikra
 
Rais Magufuli ametoa siri hiyo leo wakati akizindua daraja la la Ubungo lililopewa jina la Kijazi Interchange.

Rais Magufuli amedai kuwa alipokuwa mwanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es Salaam alikuwa akipiga kibarua cha kuendesha teksi bubu ili ajipatie chochote kitu. Na kituo alichokuwa anapaki ni jirani na lilipojengwa daraja hilo la juu mahsusi kupunguza foleni.

Rais Magufuli amesema kazi ya urais ni ngumu sana maana pamoja na kuwa na hamu ya kuendesha gari lakini huwa anakatazwa na kuzuiliwa.

Mbali ya hayo rais wa JMT amesema kuwa maendeleo huwa wakati mwingine yanakuja na vikwazo sababu wakazi wa maeneo ya Ubungo mpaka Mbezi mwisho walichukia kubomolewa nyumba zao pamoja na kuwa zilikuwa ndani ya hifadhi ya barabara.

Rais Magufuli amesema sheria ni Msumeno ndio maana hata jengo la Serikali ambalo ni mali ya Tanesco lilivunjwa japokuwa aliyekuwa waziri mkuu kipindi cha awamu ya nne ndugu Mizengo Pinda hakuamini kama litakuja kuvunjwa.

My take: Wakazi wa Dar es Salaam waambieni watoto wenu wasichague kazi. Kutwa wanashinda vijiweni wanajadili habari za Simba na Yanga,Diamond na Zari huku wakibweteka. Miaka ya nyuma mtu unapiga deiwaka ya udereva teksi huku unasoma.
FIX 🤨🤣🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom