Rais Magufuli: Nitaheshimu ukomo wa miaka 10 ya Urais kulingana na Katiba ya Tanzania

Rais Magufuli: Nitaheshimu ukomo wa miaka 10 ya Urais kulingana na Katiba ya Tanzania

Nakumbuka Kagame alijifanya hapendi ila wananchi walipomuomba akakubali shingo upande..... nawasihi msimalize popcorn zenu kabla hata hakujacha ....
 
Rais Magufuli akiwa Korogwe Tanga amesema hayuko tayari kuendelea kuongoza baada ya miaka 10 iliyowekwa kikatiba. Ameyasema haya baada ya Mbunge wa Korogwe Vijijini, Steven Ngonyani (Prof. Maji Marefu) kusema Rais anastahili kuongezwa muda ilia afanye mambo mengi zaidi.

Its official kuwa Magufuli hataongeza muda wa kukaa kwenye kiti cha urais. Hii kauli imemaliza wasiwasi wa watu wote waliokuwa na speculation kuwa Rais anaweza kuongeza muda wa kukaa madarakani.

We ata unafikiri anaaminika huyo, leo anaongea hiki kesho anaongea kingine
 
Watanzania tutaandana kuibadilisha katiba, watanzania ndo wenye katiba hivyo tutaibadili. Kama ataendelea na spidi hii au ataiongeza zaidi, tutaibadilisha katiba kwa ajili yake tu kisha tutairejesha atakapotaka kupumzika.
 
Kumi yote hiyo ataipataje kwa mfano!!

mzee mzima haishiwi maneno
 
Akizindua stand mpya ya mabasi korongwe mkoani Tanga, Rais Magufuli ameweka wazi kikwazo kinachomzuia kutawala zaidi ya "miaka kumi"

Yeye, kwa kutumia "mafumbo katika kuongea ameweka wazi na na kufikisha ujumbe na kutueleza Watanzania kuwa;

"Anaheshimu sana katiba ya nchi" iliyowekwa na wananchi, na kwa maana hiyo Katiba ndiyo "kikwazo" kikubwa kinachomzuia kuwepo madarakani kwa mda mrefu, licha ya kuwa watanzania wanampenda ila katiba ikibadilishwa yupo tayari kuwepo madarakani.

Ni dhahiri kuwa Rais Magufuli, kwa mda mchache aliokaa madarakani(miaka miwili), ameonesha kuwa anaouwezo mkubwa wa kuifikisha Tanzania mahali salama kimaendeleo na katika uchumi na hali nzuri waitakayo watanzania.

Hii inatokana na juhudi zake kubwa katika kulinda na kutetea rasilimali za nchi
kutokana na "mtukufu huyu kukubalika na kupendwa na watu, imepelekea hadi baadhi ya viongozi wakubwa nchini, Rais mstaafu, Mzee Mwinyi na wabunge mbalimbali na pia wananchi kutoka kila kona ya Tanzania kudai/kuomba Rais Magufuli tumwongezee muda.

Kwa hili ningelipenda watanzania tuanzishe mchakato wa kubadili katiba ili Rais Magufuli aweze kukaa madarakani kwa muda mrefu(zaidi ya miaka 10)

Rais ametuambia kuwa katiba ndiyo inamzuia kuwepo kwa kipindi kirefu licha ya yeye kuwa na ndoto za kuivusha Tanzania.

Sasa ni jukumu letu wananchi kuondoa hiki kikwazo ili rais wetu mpendwa aweze kuendelea kuwepo madarakani.

Watanzania wengi tumemwelewa na tumempenda ni Rais jasiri, mkweli na muwazi, anayetekeleza na kutenda watakavyo wananchi pia sio fisadi wala mwenye tamaa na pesa kama wafanyavyo wengine kujilimbikizia mali wawapo madarakani.

###Magufuli baki madarakani##

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hizi ni kauli za watu wasiojielewa..Amebakiza miaka miwili/mitatu amalize AWAMU YA KWANZA YA UONGOZI WAKE then am sure atagombea ampewe miaka mingine mitano..jumla nane..JE WEWE UNATAKA ATAWALE KWA MIKA MINGAPI WKT HATA HII YAKE KIKATIBA HAJAIMALIZA!!

My take:
Kuna watu wanaropokaga bila kujitambua wanaongea nini..hii inaonesha jinsi gan watz tuna Uwezo mdogo wa kufikiri.(IQ)

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Vitu vingine vinakera sana

Ngoja ninyamaze nisije nikapimwe mkojo.
 
Mkuu naomba nipingane na wewe, taifa lina watu wengi sana hata uwe na mazuri mengi sana itafika mahali mawazo mapya yatahitajika kulivusha taifa tena. Uongozi mzuri ni kuamini kuwa wapo watu wengine wana uwezo wa kuongoza na kwa utaratibu ule ule uliotumika kumweka madarakani ndio utumike pia kumpisha mwingine atuongoze pindi mh. Rais Magufuli atakapomaliza muda wake.

sent from kuzimu
 
Kisheria Magufuli anayo miaka mitano tu ya "kuongoza" serikali. Ingawa katiba inamruhusu kugombea muhula mwingine wa miaka mitano.Na ikumbukwe hilo litawezekana pale tu chama atakachoombea kuwania kitakapomteua tena. Na ukomo wake kufikia hapo. Sasa, hizo ngonjera nyingine zinatokea wapi?
 
Mwacheni na yeye apumzike baada ya kipindi chake Kikatiba kuwa kimeisha. Kwanza miaka kumi (10) ni mingi mno.
Mi nadhani muda umefika tukibadili Katiba, muhula wa kukaa madarakani uwe ni Miaka minne (4) kwa muhula au nane (8) kwa mihula miwili.
 
Hizi tetesi mbn zinajitokeza mara kwa mara tunatumbukia kusiko, Rais anatakiwa alikemee hili jambo kwa dhati kama siyo wazo lake.
Huanza hivi hivi ud..teta huanzaga hivi hivi Sadam mzuri sana, Mobutu mzuri sana Idd Amin mzuri sana hivi hivi.
Mkuu awakemee watamharibia tu wamuogope
 
Akizindua stand mpya ya mabasi korongwe mkoani Tanga,Rais Magufuli ameweka wazi kikwazo kinachomzuia kutawala zaidi ya
"miaka kumi"
Yeye,kwa kutumia "mafumbo katika kuongea ameweka wazi na na kufikisha ujumbe na kutueleza
Watanzania kuwa

"anaheshimu sana katiba ya nchi" iliyowekwa na wananchi,na kwa maana hiyo Katiba ndiyo "kikwazo" kikubwa kinachomzuia kuwepo madarakani kwa mda mrefu,licha ya kuwa watanzania wanampenda
ila katiba ikibadilishwa yupo tayari kuwepo madarakani.!!

Ni dhahiri kuwa Rais magufuli,kwa mda mchache aliokaa madarakani(miaka miwili),ameonesha kuwa anaouwezo mkubwa wa kuifikisha Tanzania mahali salama kimaendeleo na katika uchumi na hali nzuri waitakayo watanzania.

.Hii inatokana na juhudi zake kubwa katika kulinda na kutetea rasilimali za nchi

kutokana na "mtukufu huyu kukubalika na kupendwa na watu

imepelekea hadi baadhi ya viongozi wakubwa nchini,Rais mstaafu,Mzee Mwinyi na wabunge mbalimbali na pia wananchi kutoka kila kona ya Tanzania kudai/kuomba Rais magufuli tumwongezee muda.

Kwa hili ningelipenda watanzania tuanzishe mchakato wa kubadili katiba ili Rais magufuli aweze kukaa madarakani kwa muda mrefu(zaidi ya miaka 10)

Rais ametuambia kuwa katiba ndiyo inamzuia kuwepo kwa kipindi kirefu licha ya yeye kuwa na ndoto za kuivusha tanzania.

sasa ni jukumu letu wananchi kuondoa hiki kikwazo ili rais wetu mpendwa aweze kuendelea kuwepo madarakani.

Watanzania wengi tumemwelewa na tumempenda ni Rais
Jasiri,mkweli na muwazi,anayetekeleza na kutenda watakavyo wananchi Pia sio fisadi wala mwenye tamaa na pesa kama wafanyavyo wengine kujilimbikizia mali wawapo madarakani

###Magufuli baki madarakani##

Sent using Jamii Forums mobile app
Ifike mahali tuache huu upuuzi tena tuukemee kwa nguvu zote, mzahamzaha mwisho itakuwa kweli

Hapa tuko Tanzania na hatuko Rwanda au Uganda. Tunafuata Taratibu zetu za democracy na katiba inavyosema. Sijui utakuwa umetumwa?????
 
Amenukuliwa na vyombo vya habari, akipinga maoni ya wana CCM wanaotaka aendelee kutawala hata muda wake wa uongozi kikatiba utakapoisha.

JPM "Sitakua tayari kuvunja katiba"

MAGAZETINI.

SWALI:- Vipi kupiga marufuku shughuli za vyama vya siasa sio kuvunja katiba?
 
Back
Top Bottom