Huko Geita Mkurugenzi kasimamishwa kazi. Ni safi sana! Sababu ziko wazi. Pesa za CSR haziwezi kuwa za gari la Mkurugenzi, wakati Shule, Hospitali na Madaraja ni hovyo. Mbaya zaidi ni gari la milioni 400! Tatizo hili liko kote! Hiyo ofisi ya waziri mkuu inayopitisha vibali kama hivyo ina udhaifu wa kudumu na ni sehemu ya rushwa za manunuzi.
Hata vyuo vikuu kila leo kuna magari ya kifahari yananunuliwa kwa ajili ya viongozi wakati vyuo hivi haviwezi hata kulipa pesa za likizo za wafanyakazi, hawawezi kuboresha mazingira ya kusomea, hawawezi kujenga nyumba za wanafunzi. Rais Magufuli, tembelea UD, tembelea SUA, nenda UDOM, Mzumbe, Muhimbili, kote kuna magari ya aina hii yamenunuliwa kwa kipindi hiki.
Kama vyuo vikuu wako hivyo, unategemea nini kwenye Halmashauri kwa madiwani? Wakurugenzi hawa wamesoma vyuo hivi visivyojua nini muhimu kuliko kingine na rushwa zao. Ni vyuo hivi hivi vilivyokuwa vinaiba pesa za wanafunzi kupitia bodi ya mikopo. Bahati mbaya sana, wanaachwa bila kuchukuliwa hatua. Hawa ndo wnaojenga tabia ya waajiliwa wa baadaye.