Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ni hela za CSR ?Huko Geita Mkurugenzi kasimamishwa kazi. Ni safi sana!! Sababu ziko wazi. Pesa za CSR haziwezi kuwa za gari la Mkurugenzi, wakati shule hospitali na madaraja ni hovyo. Mbaya zaidi ni gari la milioni 400! Tatizo hili liko kote! Hiyo ofisi ya waziri mkuu inayopitisha vibali kama hivyo ina udhaifu wa kudumu na ni sehemu ya rushwa za manunuzi.
Hata vyuo vikuu kila leo kuna magari ya kifahari yananunuliwa kwa ajili ya viongozi wakati vyuo hivi haviwezi hata kulipa pesa za likizo za wafanyakazi, hawawezi kuboresha mazingira ya kusomea, hawawezi kujenga nyumba za wanafunzi. Rais Magufuli, tembelea UD, tembelea SUA, nenda UDOM, Mzumbe, Muhimbili, kote kuna magari ya aina hii yamenunuliwa kwa kipindi hiki.
Kama vyuo vikuu wako hivyo, unategemea nini kwenye halmashauri kwa madiwani? Wakurugenzi hawa wamesoma vyuo hivi visivyojua nini muhimu kuliko kingine na rushwa zao. Ni vyuo hivi hivi vilivyokuwa vinaiba pesa za wanafunzi kupitia bodi ya mikopo. Bahati mbaya sana, wanaachwa bila kuchukuliwa hatua. Hawa ndo wnaojenga tabia ya waajiliwa wa baadaye.
Kuubadili mfumo wa upigaji ni kazi sana maana wanufaika ni wengi na inapofika huko ushirikiano ni mkubwa na hawaangalii uchama, udini, utaifa, wala ukabilahii nchi ni vituko aisee,
yani matatizo ya hii nchi hayawezi kutatulika bila rais mwenyewe kwenda kukagua mahesabu ya manunuzi???
Kweli mkuu kama pale Muhas ndio balaa yan kuna miradi watu wanapiga hata kodi ya serikali haendi na serikali imesahau kutupia jicho katika vyuo vikuuKuubadili mfumo wa upigaji ni kazi sana maana wanufaika ni wengi na inapofika huko ushirikiano ni mkubwa na hawaangalii uchama, udini, utaifa, wala ukabila
Siamini kama kila kitu ni suala la CCM-CHADEMA. Mambo mengine ni ubovu wa uelewa na kama ilivyoletwa, vyeti vikubwa vya mashuleni bila uelewa. Inakuwaje wewe una digrii 1,2,3 au 4 kama Mwakyembe unapewa taasisi, unasoma utaratibu unakuruhusu kununua V8 nawe unafanya hivyo wakati taasisi hiyo haina hata choo. Haya siyo CCM! Hata CHADEMA wakitawala ni hayo hayo au huenda ni zaidi ya hayo.... sheria inasemaje? Huko vyuo vikuu wanaruhusiwa au hawaruhusiwi kununua magari ya hadhi hiyo? Kama wanaruhusiwa kosa liko wapi? Kama hadi Ofisi ya Waziri Mkuu imeridhia manunuzi hayo tatizo sio mnunuzi tatizo ni sheria na kanuni!
Hayo ndio matokeo ya watu kwenda Bungeni kugonga meza bila kujua kinachojadiliwa kinahusu nini na nini madhara yake kwa siku zijazo. Watu wakipiga kelele wanafukuzwa Bungeni; wanaondolewa majimboni; na wanabezwa "walikuwa wanatuchelewesha". CCM kwa asili yake haijawahi kuwa rafiki wa taifa hili hata chembe; zaidi ni hadaa za kisiasa ili wandelee kufaidi keki ya taifa wao na vizazi vyao.
Tatizo Mh Rais huwa anashughulikia tatizo kwa kuangalia mtu au kikundi.
Alitakiwa ashughulikie tatizo hili kimfumo na siyo ki mtu au kisehemu.
Office iliyotumiwa ni office ya waziri mkuu, ambae ni msaidizi wake mkuu. Hatujasikia maelekezo ya hadharani kutoka kwake kama alivyotoa ya wafanyakazi wa TMAA na Mkurugenzi wa Geita.
Mi nadhani kuna double standard katika kushughulikia matatizo ya nchi hii.
ni sawa kwa upande mwingine,ili ujue kabisa usimeze yai ambalo likigoma kupasuka utashindwa kulitapika.Tatizo Mh Rais huwa anashughulikia tatizo kwa kuangalia mtu au kikundi.
Alitakiwa ashughulikie tatizo hili kimfumo na siyo ki mtu au kisehemu.
Office iliyotumiwa ni office ya waziri mkuu, ambae ni msaidizi wake mkuu. Hatujasikia maelekezo ya hadharani kutoka kwake kama alivyotoa ya wafanyakazi wa TMAA na Mkurugenzi wa Geita.
Mi nadhani kuna double standard katika kushughulikia matatizo ya nchi hii.
kuubadili mfumo ni kupiga chini CCMKuubadili mfumo wa upigaji ni kazi sana maana wanufaika ni wengi na inapofika huko ushirikiano ni mkubwa na hawaangalii uchama, udini, utaifa, wala ukabila
Ikoje policy yao?
Hawa NHIF wanaoshirikiana na dispensaries kulipa malipo ya tiba isiyokuwepo? Kwa ujumla hapa tuzungumze udhaifu wa taasisi bila kujali ni kununua magari au la. Wengine hadi leo wanafanya sherehe za mamilioni kuaga viongozi. Hiyo niliisikia kule SUA! Hicho ni chuo kikuu, lakini kinatumia mamilioni kuaga viongozi!Bajeti ya utengenezaji magari Serikalini. Unanunua gari mpya tano
Only NHIF ndo Wana policy nzuri
Ulipoanza na swali eti, 'sheria inasemaje?' nimekumbuka mila yetu ya mkubwa kula firigisi! Yaani wewe uone mtoto pembeni yako hana mboga bado useme mila yetu ni mkubwa kula firigisi! That will be rubbish!Sheria inasemaje? Huko vyuo vikuu wanaruhusiwa au hawaruhusiwi kununua magari ya hadhi hiyo? Kama wanaruhusiwa kosa liko wapi? Kama hadi Ofisi ya Waziri Mkuu imeridhia manunuzi hayo tatizo sio mnunuzi tatizo ni sheria na kanuni!
Hayo ndio matokeo ya watu kwenda Bungeni kugonga meza bila kujua kinachojadiliwa kinahusu nini na nini madhara yake kwa siku zijazo. Watu wakipiga kelele wanafukuzwa Bungeni; wanaondolewa majimboni; na wanabezwa "walikuwa wanatuchelewesha". CCM kwa asili yake haijawahi kuwa rafiki wa taifa hili hata chembe; zaidi ni hadaa za kisiasa ili wandelee kufaidi keki ya taifa wao na vizazi vyao.
Hata akifika huko haitasaidia kituKwa kweli afike na huko
Maendeleo hayana vyama
Hili suala la V8 ni mzigo mzito kwa serikali. Nlitarajia kwa jinsi mheshimiwa anavyopenda kubana matumizi angeanza na hili alipoingia madarakani lakini hili kalifumbia macho. Ni ukweli kuwa hii idara ya manunuzi serikalini inatumia pesa kwa kufuja sana.
Hivyo vyuo vilivyotajwa hapo juu ni mfano tu lakini vyuo vyote vya serikali, vya juu na vya kati hali ni hiyo hiyo. Kuna matumizi mabaya ya pesa za umma kwenye suala la manunuzi na magari yasiyo na tija yananunuliwa tena kwa kulazimisha.
Issue siyo kwamba magari ya bei hizo, maofisa wa Serikali hawaruhusiwi kuyanunua, hapana isipokuwa ni kwamba yanaruhusiwa kununuliwa na pia kutumika kulingana na hadhi ya ofisa mhusika, ambaye anaruhusiwa kisheria kutumia gari la hadhi hiyo.Huko Geita Mkurugenzi kasimamishwa kazi. Ni safi sana!! Sababu ziko wazi. Pesa za CSR haziwezi kuwa za gari la Mkurugenzi, wakati shule hospitali na madaraja ni hovyo. Mbaya zaidi ni gari la milioni 400! Tatizo hili liko kote! Hiyo ofisi ya waziri mkuu inayopitisha vibali kama hivyo ina udhaifu wa kudumu na ni sehemu ya rushwa za manunuzi.
Hata vyuo vikuu kila leo kuna magari ya kifahari yananunuliwa kwa ajili ya viongozi wakati vyuo hivi haviwezi hata kulipa pesa za likizo za wafanyakazi, hawawezi kuboresha mazingira ya kusomea, hawawezi kujenga nyumba za wanafunzi. Rais Magufuli, tembelea UD, tembelea SUA, nenda UDOM, Mzumbe, Muhimbili, kote kuna magari ya aina hii yamenunuliwa kwa kipindi hiki.
Kama vyuo vikuu wako hivyo, unategemea nini kwenye halmashauri kwa madiwani? Wakurugenzi hawa wamesoma vyuo hivi visivyojua nini muhimu kuliko kingine na rushwa zao. Ni vyuo hivi hivi vilivyokuwa vinaiba pesa za wanafunzi kupitia bodi ya mikopo. Bahati mbaya sana, wanaachwa bila kuchukuliwa hatua. Hawa ndo wnaojenga tabia ya waajiliwa wa baadaye.
Kama serikali ina nia kweli ya kubana matumizi kwanini hii miaka 5 iliyopita imeshindwa kupiga marufuku manunuzi ya magari ya kifahari?Issue siyo kwamba magari ya bei hizo, maofisa wa Serikali hawaruhusiwi kuyanunua, hapana isipokuwa ni kwamba yanaruhusiwa kununuliwa na pia kutumika kulingana na hadhi ya ofisa mhusika, ambaye anaruhusiwa kisheria kutumia gari la hadhi hiyo.
Hao unaowalalamikia usikute wamekuwa wakitumia magari ya aina hiyo miaka yote kihalali kwa sababu kama isingekuwa hivyo, tayari wangekuwa wameshachukuliwa hatua au kuzuiwa kabla.
Na kama itatokea kwamba kweli hata hawa nao pia hawaruhusiwi kuwa na magari ya aina hiyo, basi zoezi zima linaweza hata likawa litahitaji "auditing" ya magari ya aina hii kwa nchi nzima kwenye taasisi zote za umma, mithili ya vile lilivyokuwa zoezi la vyeti feki.
Zaidi ni kuwa kama vilevile situation itakuwa kweli iko hivyo kama nilivyoidhania hapo juu, basi kuna uwezekano hata yule aliyepewa adhabu kwa kununua gari la iana hiyo, pengine akasamehewa ka sababu mazingira ya sehemu zingine kwenye taasisi nyingine nyingi tu yatakuwa yamem-favour kupata msamaha, assuming magari haya yametapakaa sehemu nyingi yakiwa yanatumika na maofisa ambao hadhi zao haziruhusu watumie magari ya aina hiyo.
Yeye anajua mfumo uko sawa, isipokuwa bado anakiri kuna matatizo ya hapa na pale, mithili ya hili tunalolijadili hapa muda huu.Tatizo Mh Rais huwa anashughulikia tatizo kwa kuangalia mtu au kikundi.