Rais Magufuli relax, hawataki Urais wako bali wanataka ujivuruge

Rais Magufuli relax, hawataki Urais wako bali wanataka ujivuruge

Kwa hiyo mumeona Tundu Lissu hafai tena mumehamia kwa Membe?

Nani anamfagilia Membe? Hapa anapakwa mafuta kwa mgongo wa chuma ili kumuonyesha Magu kwamba watu hawamfagilii.
 
hahhah lazima utakuwa una ugonjwa fulani kichwani hahaha yani mwaka huu ni wa mwisho kwakuwa utampindua? hahahaha Magufuli ni mwenyekiti wa chama hahahahah
IQ yako ndogo, mi ni mwana CCM kindaki ndaki, nimelelewa na kunywa maji ya CCM, usilte ubwenge, Dr. Magufuli ndiye rais hakuna wa kumtoa, nilichoandika ni kuwa kinadharia mtu huweka misimamo ya uongozi kwa miaka 3, thereafter akiyumbushwa na kukubali kufurahisha watu wachache hupoteza muelekeo na ndo maana sasa wanakazana kwa sababu wanajua mwaka wake wa mwisho ktk nadharia.
 
Nani anamfagilia Membe? Hapa anapakwa mafuta kwa mgongo wa chuma ili kumuonyesha Magu kwamba watu hawamfagilii.
Aaah kumbe ni hayo tu. Watanzania bwana tunashabikia mambo utafikiri tuko serious kumbe hamna kitu.
 
Hii ya kumfanya apoteze focus ni ngumu sana kufanikishwa. ZZK anajaribu sana kumtoa jamaa kwenye reli lakini anaishia kuonekana kiroja. Kaongea sana kuhusu korosho, Birthday boy kafanya kazi jumapili jioni.

Jamii ya kisomi inaweza kuwa na hoja za mitandaoni lakini huwa hazina nguvu kule kwa wanaopigwa na jua huku wakilima kwa jembe la mkono.
 
Aaah kumbe ni hayo tu. Watanzania bwana tunashabikia mambo utafikiri tuko serious kumbe hamna kitu.

Nchi hii kuna mtu yuko serious basi? Kuanzia rais mpaka wananchi. Kama rais alisema Acacia hawajasajiliwa hapa nchini lakini bado wapo na wanaendesha shughuli zao unategemea nini?
 
Hii ya kumfanya apoteze focus ni ngumu sana kufanikishwa. ZZK anajaribu sana kumtoa jamaa kwenye reli lakini anaishia kuonekana kiroja. Kaongea sana kuhusu korosho, Birthday boy kafanya kazi jumapili jioni.

Jamii ya kisomi inaweza kuwa na hoja za mitandaoni lakini huwa hazina nguvu kule kwa wanaopigwa na jua huku wakilima kwa jembe la mkono.

So hapa unachojivunia ni uelewa finyu wa watu wengi!? Kwa taarifa yako wachache ndio hubadili mambo, wengi hufuata hilo kundi dogo la waelewa.
 
IQ yako ndogo, mi ni mwana CCM kindaki ndaki, nimelelewa na kunywa maji ya CCM, usilte ubwenge, Dr. Magufuli ndiye rais hakuna wa kumtoa, nilichoandika ni kuwa kinadharia mtu huweka misimamo ya uongozi kwa miaka 3, thereafter akiyumbushwa na kukubali kufurahisha watu wachache hupoteza muelekeo na ndo maana sasa wanakazana kwa sababu wanajua mwaka wake wa mwisho ktk nadharia.

Migambo wanaruka na kukanyagana. Kweli hili shambulio ni kali kali hadi mabeki wa timu moja mnafokeana.
 
Mika 5 inatosha; mwacheni akapumzike ili watu makini waongoze nchi maana nchi huwa haiongozwi kwa majaribio.
 
So hapa unachojivunia ni uelewa finyu wa watu wengi!? Kwa taarifa yako wachache ndio hubadili mambo, wengi hufuata hilo kundi dogo la waelewa.
Wachache wa mijini mara nyingi wanakuwa na mahusiano na wapigaji kama na wao sio wapigaji. Ni wafuasi wakubwa wa status quo ambayo haina faida kwa huko kwenye watanzania wavuja jasho.
 
Kwako Mh. Rais John Pombe Magufuli

Leo kwa mara ya kwanza toka nijiunge na JF nimeamua kuweka mada kwenye hii forum. Ni kwa ajili yako mkuu.

Nimeshawishika kuweka mada hii maalum kwa ajili yako hasa baada ya leo kuingia humu Jamii Forum na kukuta mada nyingi (posts)zisizopungua kumi (10) zikijadili au zikilenga KUMNADI Ndugu BERNAD MEMBE kuwa mgombea wa Urais wa Tanzania mwaka 2020.

Mh. Rais, Najua watu wako wapo humu, Namimi nawaomba kwa heshima sana wakufikishie ujumbe huu wenye TAHADHARI, USHAURI NA KUKUTIA MOYO.

Mh. Rais

1. Hawataki Urais bali wanataka UCHUKIE na uwachukulie hatua ili wapate pa kuanzia
Wao sio wajinga wanajua ni mapema sana kuanza chokochoko za urais na wanajua hata wakiutaka hiyo 2020 kwa utaratibu wa chama chenu hawawezi kupata. ILA wanafanya hivyo kwasababu kwa kiasi fulani wamekusoma tabia yako kuwa huwa unachukua hatua kali sana tena kwa haraka sana.

Any Panicky Reaction upon them utakuwa umewapa ushindi. Kusudio hapo ni wewe uwape sababu ya kukuita majina haya Diktekta,Muuaji, Hapendi kukosolewa,Anataka urais milele n.k. Baada ya hapo Wanaharakati, Mashirika ya Haki za kibinadamu hasa ya kimataifa wataingilia na kukuwekea vikwazo na kukuharibia.

PLEAAASE Mheshimiwa Rais nakuomba sana aidha UWAPUUZE KABISA au uwashughulikie in a very prudent way. Wanacheza mchezo wa akili.. CHEZA NAO.

2. SIO WAO KUNA WATU NYUMA YAO
Mhe. Rais, Unajua wazi kwamba upo kwenye vita ngumu dhidi ya Mabepari ambao wameapa kuvuruga utawala wako kwa gharama yoyote ile hata ikiwa ni kutumia watu wa chama chako mwenyewe.

List ya majina iliyotolewa na Cyprian Musiba sio ya kuipuuza sana. Ni watu wenye hasira na wewe na watu waluoumizwa kwa namna moja au nyingine kwenye maslahi yao binafsi na mtindo wa uongozi wako hivyo ni rahisi sana kwa wao kununulika na kukubali kuiharibu nchi.

NAOMBA SANA..Usireact kwa wepesi bila kuchimba zaidi wengi wao unao humohumo kwenye chama na mnajuana vizuri.

3. KUSUDIO NI KUKUTOA KWENYE RELI (To Make you Lose Focus)
Mpaka sasa upo kwenye njia sahihi. Mapungufu yapo hata me nayaona ila tutayaongelea siku nyingine kwa leo ni muhimu wewe ujue kuwa wanataka kukutoa kwenye right track uanze kuoambana nao ili wpate headlines z kutosha kwenye media then wataanza kuomba External Intervention then it's over KUFUMBA NA KUFUMBUA TUKO LIBYA.

SO FAR YOU ARE THE BEST PRESIDENT. PLEASE BE CAREFULY
Nimekusoma kiurahisi sana, wewe pamoja na wengine wenye mtazamo kama wako hamumpendi mkuu wetu! ungekuwa unampenda ungemshauri afanyie kazi mapungufu ili wale wote wanaotaka kumharibia wakose pa kuanzia, sasa wewe umebaki kusema mema wakati wote tunayaona!! kwani wewe hujui silaha ya adui ni mapungufu?? japo siyo makubwa??? Kila binadamu huwa anakosea na ili uweze kumsaidia ni kumpa mrejesho ( concrete feedback) ili afanye vizuri zaidi.

Umegusia swala msiba sijui nani huyo...huyu jamaa anachokifanya ni kumtengenezea mkuu wetu chuki mbaya sana ndani ya jamii yetu. Na napata mashaka sana kama kweli mkuu wetu anahitaji sana hizo sifa anazozitoa huyo msiba! unajua kuna wakati unamsifia mtu hata unaemsifu sasa anakukinai! maana hata yeye atajiuliza hivi hakuna eneo lolote kwenye taasisi sijaenda sawa? Yeye anajipambanua kueleza mema ya mkuu, ila najiuliza ni kweli sisi wengine hatuoni anachokifanya baba yetu? je hiyo nguvu kubwa kiasi hicho anayoitumia huyo msiba ni ya nini? haoni kama anataka kuuaminisha umma kuwa mkuu ana mapungufu kwa hiyo anataka kuyafunika?? Mimi nikushauri uliyeleta uzi huu, mtendeeni mkuu wetu haki kwa kumsaidia pale ambapo panahitajika ushauri pia mweleze na huyo msiba aache kuleta taharuki katika jamii yetu iliyostaarabika!
 
Wachache wa mijini mara nyingi wanakuwa na mahusiano na wapigaji kama na wao sio wapigaji. Ni wafuasi wakubwa wa status quo ambayo haina faida kwa huko kwenye watanzania wavuja jasho.

Kaka wala nisikudanganye, watu wa vijijini huwa wanaburuzwa na watu wa mjini kwa kila kitu sio siasa tu. Sasa kama tuko hapa mjini tunanunua gunia la mahindi kwa shilingi 30,000 unategemea nini? Sisi wa mjini tusiolima ndio tunawapangia bei tena bila kujali gharama na changamoto zao na wanakubali. Kwa hiyo watu wa vijijini usiwaongelee hapa kabisa. Kama huamini nenda kagombee ubunge uone kama hujashinda na kuja kuishi hapa mjini. Huko wako gizani, huu ni ukweli mchungu.
 
Nimesoma andiko lako kwa hasira ni nikakutafakari wewe na uzao wako kwa mapana yasiyo na ncha nikajiuliza wewe ni mwanamke? Au mwanaume.!?
Shida yako hasa kwa Taifa hili ni ipi? Baba yako awe rais au wewe mwenyewe uwe rais..?

Tunatofautiana mawazo na tafakuri lakini lazima mfike mahali mjue kuwa nchi hii ni zaidi ya matakwa yenu binafsi na hao wafadhiri wenu.! Kuna watu wanalala nje wanapata shida wanakesha kwa ajili ya usalama wa Taifa hili.
Kuna watu wamepoteza viungo kuna watoto wameachwa yatima kwa sabbu ya usalama wa Taifa hili, hizi chokochoko mnazotaka kizianzisha kwa lolote lile je mko radhi kupokea machungu yake?
Hivi wale walio chochea chokochoko za libya leo hii wako wapi? Wanaifurahia vipi demokrasia waliyo itaka.? Watoto wao wake zao na waume zao wana ndoto zilezile..?
Najua mna watu wanao wadanganya kwa namna yoyote ile ila kama watu wanaweza kupata shida huko wanakozipata kwa usalama wa Taifa hili ili kizazi chao waje warithi Taifa lililo salama na lenye muelekeo. Kuifumua JF na kuwapata watu kama nyinyi haiwezi kuwa sawa na kukesha huko wanakokesha..

Salam zikufikie wewe pamoja na wenzio.
Kazi nzuri ya tochi ni kumulika kwenye vichaka na gizani ili ukipate ukitakacho kwa wakati..
Wasalaam.
Kusema anamtaka membe ndo ukaamuwa kutoa hivi vitisho??? ....
 
Mwaka huu wa JPM ni wa mwisho. Akivuka basi hakuna kitakachomtoa kwenye reli. Ila akiyumba amekwisha na watanzania tumekwisha maana najua mabebari yanajua uzuri/umahiri wa kiongozi huwa ni miaka 3, yakimshindwa huwa yanakata tamaa. Naamini anawashauri wa UWT wazuri sana.
Mwaka huu?? Kwanini??[emoji15]
 
Kaka wala nisikudanganye, watu wa vijijini huwa wanaburuzwa na watu wa mjini kwa kila kitu sio siasa tu. Sasa kama tuko hapa mjini tunanunua gunia la mahindi kwa shilingi 30,000 unategemea nini? Sisi wa mjini tusiolima ndio tunawapangia bei tena bila kujali gharama na changamoto zao na wanakubali. Kwa hiyo watu wa vijijini usiwaongelee hapa kabisa. Kama huamini nenda kagombee ubunge uone kama hujashinda na kuja kuishi hapa mjini. Huko wako gizani, huu ni ukweli mchungu.
Mfumo wa maisha ya njia ya mkato tulioukumbatia kuanzia enzi za Mzee Mwinyi, madhara yake ndio hayo uliyoyaandika.

Hao wa vijijini ambao wanaonekana kutokuwa na umuhimu ndio zaidi ya asilimia 80 ya wapiga kura. Hawa wa majijini wanaishi kinyonyaji tu, aina ya maisha ambayo moja akitumbuliwa wanaumia watu 10,000.
 
Back
Top Bottom