Rais Magufuli relax, hawataki Urais wako bali wanataka ujivuruge

Kwa hiyo mumeona Tundu Lissu hafai tena mumehamia kwa Membe?

Nani anamfagilia Membe? Hapa anapakwa mafuta kwa mgongo wa chuma ili kumuonyesha Magu kwamba watu hawamfagilii.
 
hahhah lazima utakuwa una ugonjwa fulani kichwani hahaha yani mwaka huu ni wa mwisho kwakuwa utampindua? hahahaha Magufuli ni mwenyekiti wa chama hahahahah
IQ yako ndogo, mi ni mwana CCM kindaki ndaki, nimelelewa na kunywa maji ya CCM, usilte ubwenge, Dr. Magufuli ndiye rais hakuna wa kumtoa, nilichoandika ni kuwa kinadharia mtu huweka misimamo ya uongozi kwa miaka 3, thereafter akiyumbushwa na kukubali kufurahisha watu wachache hupoteza muelekeo na ndo maana sasa wanakazana kwa sababu wanajua mwaka wake wa mwisho ktk nadharia.
 
Nani anamfagilia Membe? Hapa anapakwa mafuta kwa mgongo wa chuma ili kumuonyesha Magu kwamba watu hawamfagilii.
Aaah kumbe ni hayo tu. Watanzania bwana tunashabikia mambo utafikiri tuko serious kumbe hamna kitu.
 
Hii ya kumfanya apoteze focus ni ngumu sana kufanikishwa. ZZK anajaribu sana kumtoa jamaa kwenye reli lakini anaishia kuonekana kiroja. Kaongea sana kuhusu korosho, Birthday boy kafanya kazi jumapili jioni.

Jamii ya kisomi inaweza kuwa na hoja za mitandaoni lakini huwa hazina nguvu kule kwa wanaopigwa na jua huku wakilima kwa jembe la mkono.
 
Aaah kumbe ni hayo tu. Watanzania bwana tunashabikia mambo utafikiri tuko serious kumbe hamna kitu.

Nchi hii kuna mtu yuko serious basi? Kuanzia rais mpaka wananchi. Kama rais alisema Acacia hawajasajiliwa hapa nchini lakini bado wapo na wanaendesha shughuli zao unategemea nini?
 


So hapa unachojivunia ni uelewa finyu wa watu wengi!? Kwa taarifa yako wachache ndio hubadili mambo, wengi hufuata hilo kundi dogo la waelewa.
 

Migambo wanaruka na kukanyagana. Kweli hili shambulio ni kali kali hadi mabeki wa timu moja mnafokeana.
 
Mika 5 inatosha; mwacheni akapumzike ili watu makini waongoze nchi maana nchi huwa haiongozwi kwa majaribio.
 
So hapa unachojivunia ni uelewa finyu wa watu wengi!? Kwa taarifa yako wachache ndio hubadili mambo, wengi hufuata hilo kundi dogo la waelewa.
Wachache wa mijini mara nyingi wanakuwa na mahusiano na wapigaji kama na wao sio wapigaji. Ni wafuasi wakubwa wa status quo ambayo haina faida kwa huko kwenye watanzania wavuja jasho.
 
Nimekusoma kiurahisi sana, wewe pamoja na wengine wenye mtazamo kama wako hamumpendi mkuu wetu! ungekuwa unampenda ungemshauri afanyie kazi mapungufu ili wale wote wanaotaka kumharibia wakose pa kuanzia, sasa wewe umebaki kusema mema wakati wote tunayaona!! kwani wewe hujui silaha ya adui ni mapungufu?? japo siyo makubwa??? Kila binadamu huwa anakosea na ili uweze kumsaidia ni kumpa mrejesho ( concrete feedback) ili afanye vizuri zaidi.

Umegusia swala msiba sijui nani huyo...huyu jamaa anachokifanya ni kumtengenezea mkuu wetu chuki mbaya sana ndani ya jamii yetu. Na napata mashaka sana kama kweli mkuu wetu anahitaji sana hizo sifa anazozitoa huyo msiba! unajua kuna wakati unamsifia mtu hata unaemsifu sasa anakukinai! maana hata yeye atajiuliza hivi hakuna eneo lolote kwenye taasisi sijaenda sawa? Yeye anajipambanua kueleza mema ya mkuu, ila najiuliza ni kweli sisi wengine hatuoni anachokifanya baba yetu? je hiyo nguvu kubwa kiasi hicho anayoitumia huyo msiba ni ya nini? haoni kama anataka kuuaminisha umma kuwa mkuu ana mapungufu kwa hiyo anataka kuyafunika?? Mimi nikushauri uliyeleta uzi huu, mtendeeni mkuu wetu haki kwa kumsaidia pale ambapo panahitajika ushauri pia mweleze na huyo msiba aache kuleta taharuki katika jamii yetu iliyostaarabika!
 
Wachache wa mijini mara nyingi wanakuwa na mahusiano na wapigaji kama na wao sio wapigaji. Ni wafuasi wakubwa wa status quo ambayo haina faida kwa huko kwenye watanzania wavuja jasho.

Kaka wala nisikudanganye, watu wa vijijini huwa wanaburuzwa na watu wa mjini kwa kila kitu sio siasa tu. Sasa kama tuko hapa mjini tunanunua gunia la mahindi kwa shilingi 30,000 unategemea nini? Sisi wa mjini tusiolima ndio tunawapangia bei tena bila kujali gharama na changamoto zao na wanakubali. Kwa hiyo watu wa vijijini usiwaongelee hapa kabisa. Kama huamini nenda kagombee ubunge uone kama hujashinda na kuja kuishi hapa mjini. Huko wako gizani, huu ni ukweli mchungu.
 
Kusema anamtaka membe ndo ukaamuwa kutoa hivi vitisho??? ....
 
Mwaka huu?? Kwanini??[emoji15]
 
Mfumo wa maisha ya njia ya mkato tulioukumbatia kuanzia enzi za Mzee Mwinyi, madhara yake ndio hayo uliyoyaandika.

Hao wa vijijini ambao wanaonekana kutokuwa na umuhimu ndio zaidi ya asilimia 80 ya wapiga kura. Hawa wa majijini wanaishi kinyonyaji tu, aina ya maisha ambayo moja akitumbuliwa wanaumia watu 10,000.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…