Juzi kanda ya kaskazini (manyara) mwana lumumba kavunja "UMOJA WA WATU WA KILIMANJARO" (Umoja wa watu wa kaskazini), na amesema hataki kusikia maswala ya umoja huo.
Songwe mwezi uliopita "ADMINI MEKU" aliombwa serikali iwavutie maji kijiji na mwanamke mtu mzima, jibu aliopewa aende akamuombe "MUME WAKE, DIWANI WAKE au MBUNGE WAKE", akiashiria akaombe viongozi wa upinzani waliowachagua eneo hilo (bila ya kujua kama mama huyo ni mwana CCM au MPINZANI).
Kanda ya ziwa leo "MEKU" anasifia maswala ya umoja wao, sambamba akisifia na kutoa pongezi kwa ushindi mkubwa wa CCM.
* Kanda ya Kaskazini marufuku umoja, Kanda ya Ziwa ruhusa na pongezi kwa umoja, Kanda ya Kusini-Magharibi kaombeni misaada wapinzani mliowachagua na umoja wenu.
* Umoja wetu tanzania ndio huo kwenye "SPEECH" ni umoja madhubuti, ila kwenye uhalisia (practical) viongozi hawaoneshi umoja na wanaonesha matabaka wazi wazi na kuambatana na chuki dhahiri.
Unapovunja Umoja wa raia una "ASISI" kitu gani kama sio "DIVISION OF UNION" hata raia wasiwe na umoja wa kusaidiana, kushauriana na kuelimishana pindi mmoja wao anapopatwa na tatizo/shida. Raia wawe na matabaka ya mimi CCM nitasaidiwa, wewe MPINZANI hautasaidiwa.
#Watanzania sijui viongozi wetu wanatuona ni wapumbavu kiasi gani. Sijui mpaka lini wataacha kuchezea akili za raia wanyonge.