Rais Magufuli: Sitasomesha Wanafunzi waliopata ujauzito, siwezi kusomesha Wazazi

Hivi MAGUFURI HAYO MANENO UWA UNASEMA KAMA MANENO BINAFSI(PRIVATE ) KAMA MSOMI AU VIPI

Shida moja ya nchi yetu naimani ni kutokuwa na sheria na kifuatacho ndio maana rais au mtu mwenye mamlaka akisema kitu tunadhani ndio mwisho wa usemi na mwisho wa mjadala. Sasa rais kuamka kusema mambo hivi inamaana haipo sheria inayoongelea wanafunzi wanaopata mimba. Au yeye ndio mtungaji sheria wa nchi. Kama yeye ni mtungaji sheria wa nchi tuelewe.

Sababu mara kibao nimesikia mara hivi mara hivi. Hivi weww rais magufuri uwe wakati unaongea unasema hivi naongea kama binafsi au naongea kadiri ya sheria. Ili asiwepo mtu hata kama ni rais azungumze juu ya sheria na kwa mabavu. Hivyo hatuendi na utatufikisha pabaya.Hata viongozi wengine unakuta anaropoka tu sasa I amaana haipo sheria hadi tufikie kusema katika uongozi wangu. Au katika sheria tulizo jiwekea.

Tuache ushabiki wa maneno maneno au kutaka kujikuza katika madaraka ya mtu aliyonayo. Hii sio sahihi. Tufuate sheria ndio haki na mwelekeo. Sio "mimi katika uongozi wangu", hii sentensi ni ya ajabu. Ni ya ajabu maana;
1.Kwa hiyo kiongozi atakae kuja nae aje na amri yake. Je itakuwa nchi au jalala la kujiamlia na kuumiza wa chini.
2. Ni sheria sasa iandikwe kwenye mkutano wako au tunatunga sheria kwa chombo gani.

Nieleweke siko upande wowote ila baadhi ya kauli zinazotolewa na viongozi wetu sio nzuri. Bali ukiwa mkutanoni tueleze mambo ya maendeleo lakini suala la kuamua sheria ya watoto kusoma au kutosoma ipitishwe na chombo cha kutunga sheria sio kusimama au kuamka kwenye kitanda chako na kwenda mkutanoni unaropoka ropoka ili kwa mawazo yako ya siku hiyo ichafue Tanzania yetu yenye sheria zake.

Tunakuheshimu ila sio maana ukikosea sheria zilizopo usiambiwe itakuwa upofu wa ajabu sana.

Kwa hili ukubali umeamka kitandani bila kufikiria maneno ya kusema. Na ni hatari sana ukiendelea hivi.
 
Basi suluhisho ni kwa serikali kujenga shule maalum kwa ajili ya waliojifungua ili 'wasiwaambukize' wenzao tabia 'mbaya' na sio kuwanyima fursa ya elimu.

By the way, nimefurahi kuona kuwa unaamini ujauzito ni upele au kipindupindu kwamba unaambukizaπŸ˜›πŸ˜›.
 
KWA KAULI YA MH.RAIS NATAMANI HATA NIMPE ZAWADI YA KUKU TU ILA SIJUI ITAMFIKIAJE. AMENIFURAHISHA SAAANA! WOTE TUNAJUA MAPENZI NA ELIMU NI SUMU NA MSHIKA MAWILI MOJA HUMPONYOKA! WAAMUE AMA SHULE AU MIMBA!
Kwa kusema hivyo yeye ndo mtunga sheria au yuko juu ya sheria. Nini kinachotuongoza sheria au maneno ya mkutanoni.
 
Kwani Ja.neet katoa ngapi kabl ya kuwa pale alipo?
 
Mbona kauli kuhusu suala la mimba zinachanganya?? Waziri wa afya, makamu wa rais na rais kauli zao zinatofautiana.
Hii awamu hawajawahi kuwa na safu inayoonana. Kila mtu na lwake. Mwisho rais anatoa uamuzi unaoacha tahayari au anatumbua alieenda tofauti.

Kuna wakati humu ilisemwa mtu na makamu wake hawaelewani. Hili la mimba ni ushahidi tosha. Laiti kama inafaa kutumbua makamu!!
 
Pig up sana mr presedent
 


Tanzania ina inashika mkia kwa elimu, kwasababu kila Rais wetu aliyeingia madarakani elimu waliiweka kitu cha mwisho huku wakisomesha watoto wao. Umasikini kwenye jamii ambao ndiyo wengi ni kukosa elimu. Wakati Rais wetu anasema bila ya aibu na mawazo yake ya kizamani hasoneshi wazazi, wazazi anaowaita ni watoto waliopata mimba kwa shida mbali mbali, hana Wakati wa kuwasikiliza, ni kuwazika wazima kwa kuwapa adhabu bila ya haya. Rais Magufuli hapa anavunja haki za binaadamu, na hii itamvunjia heshima yake ulimwenguni Kate na yote anayoyafanya yataonekana hovyo. Wakati anasema hivyo nchi jirani wamepitisha kwenye katiba yao mtoto wa kike asikataliwe masomo kwajiri ya ujauzito. Tatizo la mamba Tanzania ni kubwa zaidi kati ya nchi za East Afrika, hii kwasababu ya kukosa elimu na ugumu wa maisha ya watoto wengi wao wanatoka kwenye familia masikini, kwa hiyo Tanzania kwa semi wa Rais Magufuli, ukizaliwa masikini hakuna chance ya maisha ni kufa masikini. Leo Tanzania Pamoja na Mali zote tunakuwa masikini, jibu, miaka NENDA miaka rudi Viongozi wetu wametunyima elimu ya maana. Nyerere alikosea, lakini hawa wote waliokuja nyuma yake walikuwa na nafasi ya kuribadilisha hili taifa, lakini wamelididimiza kwa kudharau kudumisha elimu. Ukimuelimisha mama unaelimisha familia nzima.

 
Kabisa hizi NGOs zinamambo ya ajabu kweli ilifika wakati wakawa wanagawa hadi vilainishi eti kuzuia michubuko.!
Hazifanyi kazi kiwiziwizi lakini, tusiangalie tulipoanguka pia tuangalie pale tulipojikwaa.
 
japo simkubali sizonje ila hili aliloliongea kuhusu ushoga ni ukweli mtupu hata wanyama hawaingiliani kinyume na maumbile
 
Kwa kusema hivyo yeye ndo mtunga sheria au yuko juu ya sheria. Nini kinachotuongoza sheria au maneno ya mkutanoni.
kasisitiza tu hajatubga sheria kama sheria ipo miaja mingi tu kaamua kukukumbusheni
"SERIKALI HAITOSOMESHA WAZAZI!" WANATUHARIBIA WENZAO WADOGO WAONE NI JAMBO LA KAWAIDA KUZAA UKIWA MWANAFUNZI
 
kuna watu tunawajua wamezaa na kurudi shule na mmoja alikuwa anasoma jangwani, na hili linafahamika. ??

utoaji mimba upo lakini hauwezi kulinganisha na haya makatazo ambayo yanawekwa yataongeza zaidi

huyo rais hawezi kusomesha wazazi mbona makazini anasomesha wazazi???
 
Umenielewa vibaya kwa bahati mbaya. Ndio maana mkuu kaziambia hizo NGOs ziwajenge shule hao mabinti wanaopata uja uzito.

Sooth, kumbuka kuwa kimtazamo dada mwenye uja uzito au aliye tayari na mtoto anakuwa ameshapevuka kiakili kulinganisha na wenzake mle darasani. Hao wenzake hawatakawia kuona kwamba uja uzito masomoni ni jambo jepesi tu.

Na ni dhana mbaya sana kwa mfano kwa darasa zima kuwa na wasichana ambao akili zipo nusu darasani na nusu kwenye fikra za kwenda gesti jioni.

Madhara mengine ya mchanganyiko wa mwanafunzi aliyejifungua na wale ambao bado, unaweza hata kuonekana kwenye vyombo vya usafiri, unakuta kundi la wasichana wanaongea mambo ya kiutu uzima mbele ya mzee anayeweza kuwa babu yao au bibi yao.

Sababu ni kule kuwahi kujihusisha na ngono wakiwa bado wapo shuleni. Utotoni mwetu miaka ya 80 ilikuwa ni vigumu kwa kundi la wasichana kujiachia kimaongezi mbele ya watu wanaoweza kuwa wazazi wao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…