Rais Magufuli: Sitasomesha Wanafunzi waliopata ujauzito, siwezi kusomesha Wazazi

Rais Magufuli: Sitasomesha Wanafunzi waliopata ujauzito, siwezi kusomesha Wazazi

"Serikali imeweka dira itakayowawezesha wasichana kuendelea na masomo baada ya kujifungua huku wale waliowapa mimba, wakishughulikiwa kikamilifu." Paulina Mkonongo, Mkurugenzi wa Elimu ya Sekondari, Wizara ya Elimu - 01 Disemba 2015.
______________________________________________
SERIKALI II
"Serikali imeamua kuwa wanafunzi wa kike wanaopata mimba wakiwa shuleni wasifukuzwe, bali waendelee na masomo." Ummy Mwalimu, Waziri wa Afya, akiwa Chuo kikuu kishiriki cha UDSM cha Elimu (DUCE), 27 Aprili 2017.
______________________________________________
SERIKALI III
"Serikali inaelekeza Wasichana wanaojifungua warudi na kuendelea na masomo shuleni." Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan (06 June 2017- Mugumu-Serengeti).
______________________________________________
SERIKALI IV
"Katika kipindi changu cha utawala, mwanafunzi yeyote wa kike (shule ya msingi na sekondari) akipata mimba ni marufuku kurudi shuleni. Siwezi fanya kazi ya kusomesha wazazi." Rais John Pombe Magufuli, 22 Juni 2017, Bagamoyo - Pwani.
 
HII KAULI ITAWAAHUSU WATOTO WA MASIKINI AMBAO MKUBWA KILA KUKICHA ANASEMA YEYE YUKO KWA AJILI YA KUWASAIDIA. MTOTO WA MWENYE NAZO AKISHAJIFUNGUA ATAMPELEKA PRIVATE SCHOOL. Napenda kumjulisha Rais wangu kwamba sio wote waliopata mimba wanapenda, ELIMU NI HAKI KWA KILA MTOTO, haijalishi hali yake.
Wengi wao ni vijijini kusema kwamba labda kungekua na japo shule ya private basi akapelekwa.... aangalie vizuri hata historia katika wabunge na mawaziri wake aone kama hakuna aliyepitia huko na leo yuko kama mfano..... mfyuuuu anaropoka bila kipimo
 
"Serikali imeweka dira itakayowawezesha wasichana kuendelea na masomo baada ya kujifungua huku wale waliowapa mimba, wakishughulikiwa kikamilifu." Paulina Mkonongo, Mkurugenzi wa Elimu ya Sekondari, Wizara ya Elimu - 01 Disemba 2015.
______________________________________________
SERIKALI II
"Serikali imeamua kuwa wanafunzi wa kike wanaopata mimba wakiwa shuleni wasifukuzwe, bali waendelee na masomo." Ummy Mwalimu, Waziri wa Afya, akiwa Chuo kikuu kishiriki cha UDSM cha Elimu (DUCE), 27 Aprili 2017.
______________________________________________
SERIKALI III
"Serikali inaelekeza Wasichana wanaojifungua warudi na kuendelea na masomo shuleni." Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan (06 June 2017- Mugumu-Serengeti).
______________________________________________
SERIKALI IV
"Katika kipindi changu cha utawala, mwanafunzi yeyote wa kike (shule ya msingi na sekondari) akipata mimba ni marufuku kurudi shuleni. Siwezi fanya kazi ya kusomesha wazazi." Rais John Pombe Magufuli, 22 Juni 2017, Bagamoyo - Pwani.
 
Kauli zake zinapingana na maono yake....maono ni kujenga tanzania ya viwanda...kauli na matendo ni kuendeleza ujinga...unapowanyima watoto wa kike another chance...an oppurrunity to correct their mistakes...wao wenyewe watakuwa hawana elimu na watoto wao pia watawambukiza huo ujinga..miaka kumi yake atatuachia taifa la wajinga..
Word!!!!
 
Tangu enzi za uhuru hakuna mwanafunzi aliyepata mimba akarudi shule ( YA SERIKALI) ila kumpeleka private mwanao inawezekana na wengi huenda huko,...mtoa mimba asilimia kubwa hukimbia,kufichwa na mwenye mimba au kumalizana na wazazi kwa kigezo cha nani atalea mtoto akifungwa ila wakuu wa shule hutoa barua na kumpa mzazi ya kutoa maelezo polisi ila wakifika huko kesi inaisha kimyakimya,Wazazi tulee watoto katika maadili baaaas
 
Kama kawaida ya mzee wa visasi, hivi hajui kuna watu wana chukua masters na tayari wana watoto wenye watoto.

Elimu ni haki ya kila mtu, hata kama mtoto wa sekondari kapata mimba haimaanishi hiyo haki yake inapotea, aendelezwe baadaye aje kuokoa mtoto sio kukaa anaongeza idadi ya wajinga wasio na kazi. Midingi yenye phd feki ndo haiwezi kuliona hili. Tz won't be saved by this guy, he's a joke.
Mkuu unaongea kwa uchungu...huyu mzee hafai hata kuwa na diploma kwa kauli zake
 
Atakayefanya kama alivyosema RAIS atakuwa MZAZI mpumbavu.Kuna shule za private,kama anauwezo ampeleke mtoto wake private.

Huu ujinga ati mtoto sababu amepata Mimba asisome aupeleke Lumumba na Chato
Ndugu kama una uwezo mbona kitu cha kawaida kumsomesha mwanao lakini tatizo yule wa kijijini asiye na A wala B maisha duni,mtoto wa 12 akipata mimba unadhani ataweza kumpeleka shule ya private kweli?
Nimeona wadada wengi sana ambao walipata ujauzito form one,form two ila walirudi shule na wanafanya vizuri na sasa wana maisha mazuri na watoto wao kama wadogo zao just imagine wangeachwa??
 
sipati picha mwalimu amejaziwa wamama darasani eti anawafundisha huku yeye mwenyewe hajawahi kupata mtoto, badala ya kuwa ticha yeye ndio inabidi aombe shule kwao, labda ianzishwe shule maalum kwa wote wababa na wamama ambapo watakuwa free muda wowote akitaka kungonoka inakuwa ruksa akipata mimba anazaa akimaliza anarudi shule hata akiamua kubeba mimba ya 1, 2,3,4 na kuendelea ila walimu wake muwe ninyi mnaounga mkono wazazi kusoma na nyie muone kazi maana mnadhani ualimu ni kama kupiga porojo kama hizi mnazopiga humu jf
Waaapi ulishawahi kuona darasa limejaa wazazi.... statistic za wapi hizo??? Watu wasielewa maana ya kuwa mzazi utamjua tu... we hata shule uliyosoma kumbuka ni wanafunzi wangapi walipata mimba.. darasa zima ama????
 
Namuunga mkobo na mguu, Serikali isisomeshe wazazi, wazazi watumie mifumo mingine iliyopo kujiendeleza ki - elimu. Ipo Ngumbaru, Qt's, Private schools waende huko. Walipe malipo ndio adhabu ya kosa la kuchezea nafasi waliyopewa.
Ushaona private school kolomije???
 
Siongezi wala kupunguza ni C&P.

View attachment 529091
Sioni aliloongea la ajabu katika hotuba yake.Mbona NGOs kwenye mafunzo yao mengine they are even more straight forward, lakini hamuwasemi.Na haya makampuni ya simu yanayotumia mabinti zetu kufanya mambo ya ajabu kwenye majukwaa mbona hamyanyoshei vidole.You will criticize everything unfairly kwa kuwa decision yake ni against your wishes.However the fact is, he is the President,the decision is made,and there is no away you can change it period.Uzuri ni kwamba maamuzi ya wanafunzi wanaopata mimba kutorudi mashuleni ni wish ya Watanzania wengi walio na akili zao timamu.Ninyi deviants hamtusumbui sana,we know you are being used,either kwa kujua au kwa kuto kujua.
 
Naona members wengi wemekwazika kwa kauli ya Dk.Magufuli, tunacho sahau tulio wengi ni kwamba JPJM aliwahi kusoma Seminary, sasa mtu mwenye background ya namna hiyo si rahisi ku-accept uzazi out of wedlock - kwa maoni yangu nafikiri kuna umuhimu wa Dk.Magufuli kukaa chini wa Viongozi wenzake preferably makamu wa Rais mama S.Hassan, Waziri Mkuu na katibu mkuu kiongozi wakapitia tena kauli ya Rais na kuifanyia marekebisho kidogo - binafsi naona ni vema Wasichana wanao pewa mimba kwa bahati mbaya wapewe a second chance, ila wakirudia kwa mara ya pili basi watimuliwe mara moja na kuhamishiwa shule za VETA - tukiwa wakali kupindukia Wasichana watalazimika kwenda kwenye backyard abortion clinics na kuhatarisha maisha yao - je hilo ndilo tunataka kama Taifa? Namshauri Rais wetu ajaribu ku-tone down stance yake akubaliane na hali alisi - sisemi tu encourage mambo ya ndiyo sivyo kwenye secondary schools zetu - far from it.
 
KWA KAULI YA MH.RAIS NATAMANI HATA NIMPE ZAWADI YA KUKU TU ILA SIJUI ITAMFIKIAJE. AMENIFURAHISHA SAAANA! WOTE TUNAJUA MAPENZI NA ELIMU NI SUMU NA MSHIKA MAWILI MOJA HUMPONYOKA! WAAMUE AMA SHULE AU MIMBA!
Tuambie ukweli... we ulianza mapenzi baada ya kumaliza chuo au ni vile haikutokea bahati mbaya??? Ni kweli mapenzi hayafai kabla ya wakati.. basi serikali pia iweke sheria hakuna kumtongoza mtoto wa kike mpk amalize shule
 
Yuko sahihi, wakati mwingine ukitumia busara watu hawalitilii maanani unalolizungumza
 
Basi suluhisho ni kwa serikali kujenga shule maalum kwa ajili ya waliojifungua ili 'wasiwaambukize' wenzao tabia 'mbaya' na sio kuwanyima fursa ya elimu.

By the way, nimefurahi kuona kuwa unaamini ujauzito ni upele au kipindupindu kwamba unaambukiza😛😛.
Ni uwezo wake wa kufikiria umeishia hapo.... hajui kwanza mwanafunzi mwenye mimba huwa anaficha na huwa wanaona aibu sana... wanatengwa na wenziwe ili wasionekane ni kundi moja... nimeshuhudia nikiwa primary na mwingine sekondari...
 
Ngoja tuone kama wabunge wataendelea na habari hii maana wengi walitaka wanafunzi wanaopata mimba wapate fursa ya kusoma. Hapa ndipo itadhihirika mhimili gani una nguvu.
 
Hello Dear
is me juliana (juliana22_4u@hotmail.com) awaiting to hear from you,Juliana
 
Waaapi ulishawahi kuona darasa limejaa wazazi.... statistic za wapi hizo??? Watu wasielewa maana ya kuwa mzazi utamjua tu... we hata shule uliyosoma kumbuka ni wanafunzi wangapi walipata mimba.. darasa zima ama????
Miaka ya nyuma hii sheria ilikuwepo ndio maana hakukuwa na wanafunzi wenye watoto darasani.
Aliyepata mimba alifukuzwa shule. Na mwanafunzi wa kiume aliyegundulika kampa mimba mwanamke naye alifukuzwa shule, ndio maana nidhamu ilikuwepo. Siyo siku hizi watoto wanajiachia sana badala ya kuzingatia masomo!
 
Ingekuwa wanaume wanapata ujauzito sidhani kama angetoa hilo tamko, usikute na yeye angesha zaa kama hao anaowabeza.
 
Back
Top Bottom