Rais Magufuli: Sitasomesha Wanafunzi waliopata ujauzito, siwezi kusomesha Wazazi

Rais Magufuli: Sitasomesha Wanafunzi waliopata ujauzito, siwezi kusomesha Wazazi

Wananchi kumsifia sana kumempa kiburi siku hizi anatema ugoro.
Yaani kafananisha wadada wenye mimba na mashoga? Alafu anajua vizuri akishaleta neno ushoga kwenye jamii ya watanzania atapewa pongezi kubwa maana sijawahi ona watu homophobic kama wabongo.

NGOs anazionea tu, NGO haikufanyi shoga, labda angeongelea sababu nyingine. Kama mtu aliye juu namna hii kichwa kipo hivi basi njia bado ni ndefu zaidi ya tunavyofikiria.

I'm so done with this guy, ana mdomo mbaya sijawahi pata kuona.

Mnapenda mdanganywe sio!! Spade itabaki kuwa spade tu wala sio kijiko kikubwa
 
Halafu Mzee Rungwe bado unabisha kuwa nchi haijapinda?!!😀😀😀😀
 
Kama kweli kasema hivyo basi kapotoka sana na sikubaliani naye kabisa.

Mwanafunzi wa kike kupata ujauzito siyo kosa kubwa hivyo hadi anyimwe fursa ya kujiendeleza kielimu.

Hapo adhabu haiendani kabisa na kosa!

Hajanyimwa kujiendeleza Kielimu , kunyimwa kuwa Mwanafunzi wa Shule ( School Candidate)
 
tujifunze na sisi kuwa na mambo yetu, na viwango vyetu vya maadili ambavyo tunavisimamia.
NGO na wafadhili wake ambao wengi ni wazungu wasilazimishe kuleta mambo ambayo sisi hatujaona maana yake.
Kabisa hizi NGOs zinamambo ya ajabu kweli ilifika wakati wakawa wanagawa hadi vilainishi eti kuzuia michubuko.!
 
Ameyasema hayo leo akiwa Bagamoyo kwenye uzinduzi wa barabara.

"Kwenye utawala wangu siko tayari kuruhusu ujinga kama huu, kama wanaona inafaa basi wafungue shule za wazazi ili huku wakiendelea na masomo waendelee kunyonyesha watoto wao."

Ameongeza kuwa hizo NGOs ndio zimeleta mambo ya ajabu ajabu hadi wanaume kwa wanaume kuingiliana, wanawake kwa wanawake kuingiliana.

"Hata wanyama hawafanyi hivyo mbuzi Ng'ombe huwezi kuwaona wakikosea ile sehemu...Wachungaji si mpo hapa mmewahi kuwaona mbuzi wakikosea au ng'ombe wakikosea"....aliongeza Magufuli.
Asilimia 500% naunga mkono!!
 
What?! Haki ya naniiiii ipo shida tena shida kubwa sana. Matamko ya namna hii tusilaumiane 2020
 
Ameyasema hayo leo akiwa Bagamoyo kwenye uzinduzi wa barabara.

"Kwenye utawala wangu siko tayari kuruhusu ujinga kama huu, kama wanaona inafaa basi wafungue shule za wazazi ili huku wakiendelea na masomo waendelee kunyonyesha watoto wao."

Ameongeza kuwa hizo NGOs ndio zimeleta mambo ya ajabu ajabu hadi wanaume kwa wanaume kuingiliana, wanawake kwa wanawake kuingiliana.

"Hata wanyama hawafanyi hivyo mbuzi Ng'ombe huwezi kuwaona wakikosea ile sehemu...Wachungaji si mpo hapa mmewahi kuwaona mbuzi wakikosea au ng'ombe wakikosea"....aliongeza Magufuli.
Mmh?![emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji85] [emoji85] [emoji85] [emoji85]
 
Kabisa hizi NGOs zinamambo ya ajabu kweli ilifika wakati wakawa wanagawa hadi vilainishi eti kuzuia michubuko.!
Kuna mdau aliwahi kwenda kwenye NGO moja akakuta watu pale hawaeleweki, yaani kama ushogaushoga.. ibadidi akimibie interview kwa sababu ya atmosphere ya eneo husika...
Bora walivyozifunga hizo NGO tata, kama zimebaki zimaliziwe tu.
 
Hao anaodai kuwa wanatuibia, ndio haohao wanaosaidia hadi bajeti na misaada mingine kibao mfano ACACIA, Huku akitaka kujadiliana na wezi haohao anaowatuhumu wanatuibia. Nashauri aandikiwe hotuba lasivyo ishakuwa shida sasa.
 
Back
Top Bottom