Rais Magufuli: Sitasomesha Wanafunzi waliopata ujauzito, siwezi kusomesha Wazazi

Rais Magufuli: Sitasomesha Wanafunzi waliopata ujauzito, siwezi kusomesha Wazazi

Mheshimiwa Raisi amesema katika kipindi chake cha utawala, mwanafunzi wa shule ya msingi hadi sekondari atakayepata mimba, hataruhusiwa kurudi shuleni.

"Awe kaipata kwa raha zake, awe kaipata kwa bahati mbaya, akishapata mimba, elimu ya serikali basi"
 
our no 1,leo amegusia topic muhimu mno ambaye yeye kama kawaida kaiweka kimihemko,please wana JF tujaribu kuidadisi hapa,ni kweli kila mzazi anapenda mtoto wake aelimike shuleni,

mtoto wa kike inapotokea anapata mimba why anaathibiwa yeye tu,maana anafukuzwa shule hadi yule wa kiume aliyempa mimba anaachiwa aendelee na masomo,kwangu huu ni utaratibu dume na unaendeleza ukandamizaji wa watoto wa kike,halafu baadaye tunakuja kupiga kelele ohooo mbona hatuna wasomi wengi wa kike,

kumbe wengi wao wameathiriwa na mfumo dume,solutions watoto wa kike waruhusiwe kuendelea na shule baada ya kuzaa,iandaliwe kampeni nchi nzima ili watoto wa kike wanaopenda wapigwa sindano za kuzuia mimba,na hizi zinatofautiana kutoka mwezi mmoja hadi miezi sita,ila ni lazima kila mmoja kupimwa maana zina side effects kutegemeana na mhusika,condoms zigawiwe bure mashuleni na iandamane na elimu nzuri how to use it safely,

its time noe tabia hii ya kuwafukuza shule only girls ife maana ni ya kibaguzi.
 
Kama kweli kasema hivyo basi kapotoka sana na sikubaliani naye kabisa.

Mwanafunzi wa kike kupata ujauzito siyo kosa kubwa hivyo hadi anyimwe fursa ya kujiendeleza kielimu.

Hapo adhabu haiendani kabisa na kosa!
Kuna binti alipata ujauzito akiwa form 2 miaka ya nyuma kidogo.. akajifungua salama mtoto akawa mwaka moja kasoro wazazi wake wakapambana akarudi shule.. leo hii ni Mwalimu mshahara analipwa na anawasaidia watu wengine wakiwemo wazazi wake na serikali inakata kodi kama kawaida

Magu kwa upande wa vision hamna kabisa anajenga taifa la omba omba
 
Ee Mwenyezi Mungu mnyooshe huyu mtu wako sawasawa na anavyotufanyia sisi
 
Kuna binti alipata ujauzito akiwa form miaka ya nyuma kidogo.. akajifungua salama mtoto akawa mwaka moja kasoro wazazi wake wakapambana akarudi shule.. leo hii ni Mwalimu mshahara na anawasaidia watu wengine wakiwemo wazazi wake na serikali inakata kodi kama kawaida

Magu kwa upande wa vision hamna kabisa anajenga taifa la omba omba

Lakini huo mtazamo wa Magu ni mtazamo wa watu wengi pia.

Wewe subiri tu uone maoni ya watu humu....utashangaa!!
 
Je kama mwanafunzi alibakwa? Je mwanafunzi akipewa ujauzito na mwalimu? Matineja wengi hawajapevuka kiakili kiasi cha kujua madhara wanayofanya. Si haki kuwanyima fursa adhimu kama ya elimu.
 
Hapo sio kumnyima haki ya elumu hiyo ni adhabu tu
Hivi mmewaza na kufiria nini kikatokea ikiwa itatamkwa hadharani kwamba hata mwanafunzi akipata mimba ataendelea na masomo?

Kwa upande wangu
Sioni kosa lake kutoa hilo tamko, ila hiyo ni moja ya adhabu tu kupunguza ama kuondoa kabisa tabia mbaya hasa mapenzi kwa wanafunzi.
 
Wananchi kumsifia sana kumempa kiburi siku hizi anatema ugoro.
Yaani kafananisha wadada wenye mimba na mashoga? Alafu anajua vizuri akishaleta neno ushoga kwenye jamii ya watanzania atapewa pongezi kubwa maana sijawahi ona watu homophobic kama wabongo.

NGOs anazionea tu, NGO haikufanyi shoga, labda angeongelea sababu nyingine. Kama mtu aliye juu namna hii kichwa kipo hivi basi njia bado ni ndefu zaidi ya tunavyofikiria.

I'm so done with this guy, ana mdomo mbaya sijawahi pata kuona.
 
Back
Top Bottom