our no 1,leo amegusia topic muhimu mno ambaye yeye kama kawaida kaiweka kimihemko,please wana JF tujaribu kuidadisi hapa,ni kweli kila mzazi anapenda mtoto wake aelimike shuleni,
mtoto wa kike inapotokea anapata mimba why anaathibiwa yeye tu,maana anafukuzwa shule hadi yule wa kiume aliyempa mimba anaachiwa aendelee na masomo,kwangu huu ni utaratibu dume na unaendeleza ukandamizaji wa watoto wa kike,halafu baadaye tunakuja kupiga kelele ohooo mbona hatuna wasomi wengi wa kike,
kumbe wengi wao wameathiriwa na mfumo dume,solutions watoto wa kike waruhusiwe kuendelea na shule baada ya kuzaa,iandaliwe kampeni nchi nzima ili watoto wa kike wanaopenda wapigwa sindano za kuzuia mimba,na hizi zinatofautiana kutoka mwezi mmoja hadi miezi sita,ila ni lazima kila mmoja kupimwa maana zina side effects kutegemeana na mhusika,condoms zigawiwe bure mashuleni na iandamane na elimu nzuri how to use it safely,
its time noe tabia hii ya kuwafukuza shule only girls ife maana ni ya kibaguzi.