Lord Sauron
JF-Expert Member
- May 4, 2017
- 224
- 170
Ile video clip ya mzee rungwe nilishindwa kuifuta Ni ushahidi tosha kuwa tz hamna haina viongoziHalafu Mzee Rungwe bado unabisha kuwa nchi haijapinda?!!😀😀😀😀
Wapo watoto wachache wamepata mimba kwa kubakwa kwa nguvu lakini wengi hubakwa kwa hiyari(makubaliano na under 18).Kuna msemo mmoja aliutumia JK kuhusu hawa watoto ni kweli kabisa kama huamini kaa karibu na wanafunzi, wakati wewe unamchukulia kama mtoto mwenzio anajiona mtu mzima mwenzio na hakuogopi kimahusiano. Sasa hivi mwanafunzi asiye na mpenzi huonekana mjinga na mwenye mpenzi huonekana mjanja. Ata kama serikali itawaruhusu kusoma haitakiwi Rais atangaze maana watu hawatawajibika watazitafuta mimba kwa kudhani hakuna kitakachoharibika.Mtoto anakosa haki ya kupata elimu tena kwa familia ambazo hazina uwezo wa kumpeleka private school
Nadhani paragraph ya tano kwa maoni yang nimeligusia kidogo hili suala la kubakwa, hata na mie pia nilikua mtoto wa kike ndio mana nikaileta makala hiiWakati mnapongezana ujinga lazima muelewe,kuna watoto wanabakwa wakiwa wanatembea kwenda mashuleni hasa vijijini ambako shule ziko mbali, njia ni mapori. Na asilimia kubwa ya mimba za utotoni ni Vijijini.
Hizo tamaa zinsababishwa na nini?Wewwww nani kakwambia ni ugumu wa maisha......tamaa tu za mabinti wa siku hizi hakuna lolote
Sent from my H8501 using JamiiForums mobile app
Tunaishi kwenye jamii na tunaona jinsi visichana vya shule hasa sekondari vinavyokimbizana na vijana na Wababa waliowazidi umri.Huo Upuuzi wa kusingizia kubaka futa, ndio nyie Mnasemaga bikra ilitoka kwa kuendesha baiskeli Kumbe umeanza ngono na miaka 10.Wakati mnapongezana ujinga lazima muelewe,kuna watoto wanabakwa wakiwa wanatembea kwenda mashuleni hasa vijijini ambako shule ziko mbali, njia ni mapori. Na asilimia kubwa ya mimba za utotoni ni Vijijini.
Hakuna mtoto anaetoka nyumbani na nia ya kwenda kufanya mapenzi, wengi wanalazimishwa na watu wazima, walimu n.k. sasa mtoto innocent kama huyo unamnyimaje fursa ya kusoma.
Mkuu tafuta clip ya rais akiongea Bagamoyo, halafu isikilize vizuri kabla hujafikia hatua ya kutoa maoni. Nenda youtube utaiona.Kwa hiyo Veta Ni Taasisi ya Elimu isiyo na Heshima? Je Na Wavulana Watakaowapa Watoto wa Kike Magufuli Atawafukuza Pia? Au ni selective justice!
Samahani kwa hili swali mkuu. Umemuuliza mama yako alikuzaa akiwa na umri gani. Siwatetei wanaopata mimba shuleni, ila hao unaowasema ni asilimia ndogo wanaopata mimba ,kwani wanajua hadi kumeza vidonge vya kuzuia mimba au kutoa.Tunaishi kwenye jamii na tunaona jinsi visichana vya shule hasa sekondari vinavyokimbizana na vijana na Wababa waliowazidi umri.Huo Upuuzi wa kusingizia kubaka futa, ndio nyie Mnasemaga bikra ilitoka kwa kuendesha baiskeli Kumbe umeanza ngono na miaka 10.
HATUSOMESHI WAZAZI
Ni kweli shule za mchanganyiko. Pia mavazi na simu za mikononi ni mtego mwingine wa kuwanasia wanafunzi wa kike.A
..nakuelewa.
..sijui umri wako, lakini enzi zangu shule za sekondari zilikuwa tofauti kwa wavulana na wasichana.
..naamini mazingira hayo yalitusaidia kutuepusha na vishawishi vya ngono.
..lingine lilikuwa ni marafiki niliokua nao. Wengi walikuwa makini sana ktk masomo na hawakuendekeza starehe.
..mazingira sasa hivi yamebadilika. Shule ni za mchanganyiko.
Kama alibakwa akapata mimba inakuwaje?
Ni kweli shule za mchanganyiko. Pia mavazi na simu za mikononi ni mtego mwingine wa kuwanasia wanafunzi wa kike.
Umbali wa kutoka nyumbani kwenda shuleni ukichanganya na pato dogo la wazazi, pia huchangia mimba za shuleni.
Unakuta mwanafunzi anaishi Bunju B na anasoma Benjamini Mkapa pale Ilala...kila siku aamke saa kumi na moja na kuanza shughuli ya usafiri kwenda shuleni, ni mtihani kwao.
Kuna dada mmoja miaka ya 2000 mwanzoni alikuwa akitembea na dereva wa daladala, kwa sababu tu binti alikuwa haiwezi ile shughuli ya kugombea kuingia ndani kupitia mlangoni, hivyo dereva akawa anamruhusu aingie kupitia mlango wake.
Yapo mengi ambayo kwa kweli ni chanzo cha hawa mabinti kujikuta wameingia kwenye mtego wa mahusiano wakiwa shuleni.