Lord Sauron
JF-Expert Member
- May 4, 2017
- 224
- 170
Serikali inapaswa kurudi kwenye wajibu wake wa kusimamia sheria halali zilizotungwa na bunge dhidi ya kunajisi na kubaka watoto wa shule badala ya kupanga kuwaadhibu wahanga wa jinai hizo kwa kuwakatishia elimu.
Malengo ya elimu ya msingi na sekondari ni maendeleo binafsi ya mwanafunzi, kuwafanya watoto kuwa raia wema na kuwaandaa kujitafutia vipato vyao maishani na hivyo kuliingizia taifa mapato.
Kuwazuia wasichana wasiendelee na masomo kwa sababu tu wamepata uja uzito ni kulikomoa taifa lote na si wanafunzi husika tu.