Rais Magufuli: Sitasomesha Wanafunzi waliopata ujauzito, siwezi kusomesha Wazazi

mi huyu baba simuelewi make ni mzee wa kuanza kumalizia saa daaaaaaaah mzee wapi noah zetu jamaa hawajaleta mpunga au ndo changa la macho

Hahaha. Usicheze na siasa za CCM. Bado kidogo watasema TUNDU LISSU kawakataza wasitulipe hela yetu ya Noah.
 
Utakapoamua kuwa mwanasiasa nawe utakuwa na tabia kama hizo hata kama utapewa kuwa Rais wa Afrika nzima. Hautaacha kupiga vijembe wale wanaoonekana kama wanakupinga.

 
Hapo kapotoka sana na sikubaliani naye kabisa.

Mwanafunzi wa kike kupata ujauzito siyo kosa kubwa hivyo hadi anyimwe fursa ya kujiendeleza kielimu.

Hapo adhabu haiendani kabisa na kosa!
kosa ni kosa hamna cha kosa kubwa wala kosa dogo. au ww unakipimo gani cha kujua kosa kubwa au kosa dogo???
 
Mkubwa umeongea kwa mbwembwe nyingi lakini ukweli unabaki pale pale kwamba asilimia ya wanaopata mimba kwa kubakwa sio kubwa kuliko inavyowekwa na hizi taasisi zenye matangazo yao kwenye runinga za Tanzania.

Wapo wanafunzi ambao wanajilengesha wenyewe kwenye vishawishi vya ngono zembe, wapo ambao ni kwa sababu ya umaskini wa wazazi wao. Lakini bado hatupaswi kuhalalisha uhuni na umalaya kuanzia shule ya msingi na sekondari.

Maadili mema, ni aina ya maisha ambayo wengi yametukuza. Naongelea kutanguliza malengo ya kimasomo kuliko tamaa za kutaka kuvaa kama dada mwenye kazi yake wakati msichana bado anaishi kwa wazazi wake.

Zamani kabla dunia haijawa kijiji kama leo, hakukuwa na ukosefu wa heshima kama hali ilivyo sasa. Kila mtu aliijua mipaka yake kwenye jamii aliyoishi na aliridhika na ule ukweli kwamba siku inakuja na yeye atakuwa na maisha ya hadhi ya juu.
Kwa ufupi wanafunzi wa kike waanze kubadilisha hulka zao za maisha ya kila siku. Hii kauli ya rais ni changamoto mpya kwao.
 
Mambo mengine yanahitaji kupata muda mzuri wa kutafakari, kabla ya kuyaamua au kuyaunga mkono. Nitajitahidi sana kuwaletea simulizi kutoka katika Biblia.

2Samweli 12:1-25

1Basi Mwenyezi-Mungu akamtuma nabii Nathani kwa Daudi. Nathani alimwendea Daudi, akamwambia, “Kulikuwa na wanaume wawili katika mji mmoja; mmoja alikuwa tajiri na mwingine alikuwa maskini. 2Yule tajiri alikuwa na kondoo wengi na ng'ombe wengi. 3Lakini yule maskini alikuwa na mwanakondoo mdogo mmoja jike, ambaye alikuwa amemnunua. Alimtunza, naye akakua nyumbani mwake pamoja na watoto wake. Alimlisha mwanakondoo huyo chakula kilekile kama chake na kunywea kikombe chake naye pia alikuwa akimpakata kifuani. Mwanakondoo huyo alikuwa kama binti kwa yule mtu maskini. 4Siku moja, yule tajiri alifikiwa na mgeni. Basi, tajiri huyo hakutaka kuchukua mmoja wa kondoo wake mwenyewe au ng'ombe wake, amchinjie mgeni wake, ila alikwenda na kumnyanganya yule maskini mwanakondoo wake, akamchinjia mgeni wake.” 5Daudi aliposikia hayo, akawaka hasira dhidi ya yule tajiri. Akamwambia nabii Nathani, “Naapa kwa Mwenyezi-Mungu aliye hai kwamba mtu aliyefanya jambo hilo anastahili kufa! 6Ni lazima amlipe yule maskini mwanakondoo huyo, tena mara nne, kwani ametenda jambo baya na hakuwa na huruma!”
7Nathani akamwambia Daudi, “Wewe ndiwe huyo mtu! Sasa, Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli, anasema hivi: ‘Mimi nilikupaka mafuta uwe mfalme juu ya Israeli na kukuokoa mikononi mwa Shauli. 8Nilikupa nyumba ya bwana wako na wake zake wawe wako, tena nikakupa watu wa Israeli na wa Yuda uwatawale. Na kama haya yangekuwa kidogo mno kwako ningekuongezea mara mbili zaidi ya hayo. 9Kwa nini basi, umedharau neno langu mimi Mwenyezi-Mungu ukafanya uovu huu mbele yangu? Umemuua Uria Mhiti, kwa upanga, ukamchukua mke wake kuwa mkeo. Umewatumia Waamoni kumwua Uria vitani! 10Kwa hiyo basi, kwa kuwa umenidharau na umemchukua mke wa Uria Mhiti, kuwa mkeo, mauaji hayataondoka katika jamaa yako’. 11Sikiliza, Mwenyezi-Mungu asema, ‘Tazama, nitazusha maafa katika jamaa yako mwenyewe. Nitawachukua wake zako ukiona kwa macho yako mwenyewe na kumpa jirani yako, naye atalala nao hadharani. 12Wewe ulifanya jambo hilo kwa siri, lakini mimi nitayafanya haya mbele ya Waisraeli wote hadharani.’”
13Basi, Daudi akamwambia Nathani, “Nimetenda dhambi dhidi ya Mwenyezi-Mungu.” Nathani akamwambia, “Mwenyezi-Mungu amekusamehe dhambi yako, nawe hutakufa. 14Hata hivyo, kwa kuwa kwa tendo lako umemdharau kabisa Mwenyezi-Mungu, mtoto wako atakufa.” 15Kisha Nathani akarudi nyumbani kwake.


Kisa hiki kinatusaidia kuwa yatupasa kutafakari kabla ya kutoa maamuzi. Hivi hao wanaoshangili jambo hili la watoto waliobebshwa mimba kutoruhusiwa kurudi kwenye shule za serikali wametafakati au wanafanya kama alivyofanya Daudi kumbe jambo lilimhusu yeye mwenyewe.
 
Mkuu NGOs zimefanya kazi kubwa ya indoctrination, na hatimaye kubadili mitizamo ya watu.Usi down play their contribution,it's huge.
NImesema tatizo ni primitive thinking. Fikra za mwaka 1430 katika karne ya 21...
 
NImesema tatizo ni primitive thinking. Fikra za mwaka 1430 katika karne ya 21...
Huja address point,umeingia na povu tu.Hata hivyo haisaidii,the decision has already been made. Vi-NGO uchwara haviwezi kutuyumbisha,ni lazima tuheshimu culture yetu na morals zetu.
 
Huja address point,umeingia na povu tu.Hata hivyo haisaidii,the decision has already been made. Vi-NGO uchwara haviwezi kutuyumbisha,ni lazima tuheshimu culture yetu na morals zetu.
I choose not to address anything with you. Mawazo ya karne ya 4 na yale ya karne ya 21 haviwezi kutangamana..
 
Masimango hayaishi.
Ndo wajue vya bure vina kero
 
Hao wajinga twaweza wameshawaelezea kuwa ndo wanaoiunga mkono SISIEM
 
Nauliza tu je Mwanafunzi wa shule ya msingi matatizo akimpa mimba mwanafunzi mwenzeka je kuna kesi hapo
 
Mwanafunzi wa shule ya msingi ampe mtu mimba???Mkuu ushawaona watoto wa shule ya msingi lakini!!!
 
Obvious kama kampa dawa yake yule aliepewa amrudishie aliempa!!
Hii itasaidia sana maana naona hizo mimba ni kama kifurushi tu watu wanapeana.
 
Nauliza tu je Mwanafunzi wa shule ya msingi matatizo akimpa mimba mwanafunzi mwenzeka je kuna kesi hapo
Je mwanafunzi akimpa mimba Mwalimu wake? 'Tatizo hapa ni maadili katika jamii zetu' inatakiwa tutatue tatizo na siyo kulikimbia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…