Rais Magufuli: Sitasomesha Wanafunzi waliopata ujauzito, siwezi kusomesha Wazazi

Rais Magufuli: Sitasomesha Wanafunzi waliopata ujauzito, siwezi kusomesha Wazazi

mi huyu baba simuelewi make ni mzee wa kuanza kumalizia saa daaaaaaaah mzee wapi noah zetu jamaa hawajaleta mpunga au ndo changa la macho

Hahaha. Usicheze na siasa za CCM. Bado kidogo watasema TUNDU LISSU kawakataza wasitulipe hela yetu ya Noah.
 
Utakapoamua kuwa mwanasiasa nawe utakuwa na tabia kama hizo hata kama utapewa kuwa Rais wa Afrika nzima. Hautaacha kupiga vijembe wale wanaoonekana kama wanakupinga.

Mabadiliko katika jamii yoyote ni lazima na Uongozi wowote utakuwa na malengo binafsi, namuunga mkono Rais ila jamani si kwake tu, na kwa mwengine yyt haya maneno machafu yaacheni, nachukizwa tu na baadhi ya vitendo vya wanasiasa Afrika kwanza kuwa uchaguzi umeisha halafu bado wanazozana au kuzungumzana, pili kuwa masuala ya msingi na hakki za Raia kuzinadi kuwa maendeleo, kweli neno maendeleo ni kutoka sehemu, mahala flani kwenda mahala flani lkn yanazingatio, maana Hatua kubwa ni hisia za Raia kwenye kutafuta aman ya Roho, hv anapokuja mtu kusema Maendeleo ni barabara kutoka mahala flani mpaka mahala flani ndio maendeleo? umekamilisha hisia za Raia? au kumrahisishia na kumpa tu hakki yake ya msingi, kurahisisha usafiri maana wapo wengi watatumia barabara ile na maisha bado yapo chini sina maana kuwa zisejengwe bali Rais gani duniani towa Afrika kanadi kuwa maendeleo ni barabara au maji wakati ni hakki zao.

Kwa kumaliza tu ni kwamba Juhudi za kuinua Tanzania ya Viwanda ihusike vyema kwenye akili zetu ni dhana njema kustawisha Uchumi wa Taifa hongera Rais lkn Usiisahau Zanzibar maana ni Nusu ya Tanzania.

Ahsanteni wadau.
 
Hapo kapotoka sana na sikubaliani naye kabisa.

Mwanafunzi wa kike kupata ujauzito siyo kosa kubwa hivyo hadi anyimwe fursa ya kujiendeleza kielimu.

Hapo adhabu haiendani kabisa na kosa!
kosa ni kosa hamna cha kosa kubwa wala kosa dogo. au ww unakipimo gani cha kujua kosa kubwa au kosa dogo???
 
Your thinking is flawed.

1/ Kwa kuwa sikutetea wanafunzi watoro wasifukuzwe shule hakuninyimi haki ya kutetea wahanga wa mimba za utotoni kupata fursa za elimu. Philosophically speaking, you do not justify a wrong by citing another wrong. That said, mambo ya mwanafunzi kumpiga mwalimu na msichana kupata mimba akiwa shuleni hayafanani. It shows that unajaribu kujadili tatizo ambalo hata hulielewi. Unasukumwa na mihemko. Kama una hoja ya kutetea mwanafunzi anayempiga mwalimu iweke mezani, badala ya kulazimisha wanaopinga kauli ya Rais inayokandamiza wasichana wa nchi hii wawatete wanafunzi waliompiga mwalimu.

2/ You are claiming causality simply based on gut feeling. Hoja kwamba kuruhusu wasichana wanaopata mimba kuendelea na masomo ni "kuzigeuza korido za shule sawa na zile za zahanati" is empty, hollow, and populistic. You are simply reproducing your religious biases in the name of maadili.

3/ Ni maadili gani ya nchi hii unayozungumza? Kuiba mali za umma? Ubabaishaji?
Mkubwa umeongea kwa mbwembwe nyingi lakini ukweli unabaki pale pale kwamba asilimia ya wanaopata mimba kwa kubakwa sio kubwa kuliko inavyowekwa na hizi taasisi zenye matangazo yao kwenye runinga za Tanzania.

Wapo wanafunzi ambao wanajilengesha wenyewe kwenye vishawishi vya ngono zembe, wapo ambao ni kwa sababu ya umaskini wa wazazi wao. Lakini bado hatupaswi kuhalalisha uhuni na umalaya kuanzia shule ya msingi na sekondari.

Maadili mema, ni aina ya maisha ambayo wengi yametukuza. Naongelea kutanguliza malengo ya kimasomo kuliko tamaa za kutaka kuvaa kama dada mwenye kazi yake wakati msichana bado anaishi kwa wazazi wake.

Zamani kabla dunia haijawa kijiji kama leo, hakukuwa na ukosefu wa heshima kama hali ilivyo sasa. Kila mtu aliijua mipaka yake kwenye jamii aliyoishi na aliridhika na ule ukweli kwamba siku inakuja na yeye atakuwa na maisha ya hadhi ya juu.
Kwa ufupi wanafunzi wa kike waanze kubadilisha hulka zao za maisha ya kila siku. Hii kauli ya rais ni changamoto mpya kwao.
 
Mambo mengine yanahitaji kupata muda mzuri wa kutafakari, kabla ya kuyaamua au kuyaunga mkono. Nitajitahidi sana kuwaletea simulizi kutoka katika Biblia.

2Samweli 12:1-25

1Basi Mwenyezi-Mungu akamtuma nabii Nathani kwa Daudi. Nathani alimwendea Daudi, akamwambia, “Kulikuwa na wanaume wawili katika mji mmoja; mmoja alikuwa tajiri na mwingine alikuwa maskini. 2Yule tajiri alikuwa na kondoo wengi na ng'ombe wengi. 3Lakini yule maskini alikuwa na mwanakondoo mdogo mmoja jike, ambaye alikuwa amemnunua. Alimtunza, naye akakua nyumbani mwake pamoja na watoto wake. Alimlisha mwanakondoo huyo chakula kilekile kama chake na kunywea kikombe chake naye pia alikuwa akimpakata kifuani. Mwanakondoo huyo alikuwa kama binti kwa yule mtu maskini. 4Siku moja, yule tajiri alifikiwa na mgeni. Basi, tajiri huyo hakutaka kuchukua mmoja wa kondoo wake mwenyewe au ng'ombe wake, amchinjie mgeni wake, ila alikwenda na kumnyanganya yule maskini mwanakondoo wake, akamchinjia mgeni wake.” 5Daudi aliposikia hayo, akawaka hasira dhidi ya yule tajiri. Akamwambia nabii Nathani, “Naapa kwa Mwenyezi-Mungu aliye hai kwamba mtu aliyefanya jambo hilo anastahili kufa! 6Ni lazima amlipe yule maskini mwanakondoo huyo, tena mara nne, kwani ametenda jambo baya na hakuwa na huruma!”
7Nathani akamwambia Daudi, “Wewe ndiwe huyo mtu! Sasa, Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli, anasema hivi: ‘Mimi nilikupaka mafuta uwe mfalme juu ya Israeli na kukuokoa mikononi mwa Shauli. 8Nilikupa nyumba ya bwana wako na wake zake wawe wako, tena nikakupa watu wa Israeli na wa Yuda uwatawale. Na kama haya yangekuwa kidogo mno kwako ningekuongezea mara mbili zaidi ya hayo. 9Kwa nini basi, umedharau neno langu mimi Mwenyezi-Mungu ukafanya uovu huu mbele yangu? Umemuua Uria Mhiti, kwa upanga, ukamchukua mke wake kuwa mkeo. Umewatumia Waamoni kumwua Uria vitani! 10Kwa hiyo basi, kwa kuwa umenidharau na umemchukua mke wa Uria Mhiti, kuwa mkeo, mauaji hayataondoka katika jamaa yako’. 11Sikiliza, Mwenyezi-Mungu asema, ‘Tazama, nitazusha maafa katika jamaa yako mwenyewe. Nitawachukua wake zako ukiona kwa macho yako mwenyewe na kumpa jirani yako, naye atalala nao hadharani. 12Wewe ulifanya jambo hilo kwa siri, lakini mimi nitayafanya haya mbele ya Waisraeli wote hadharani.’”
13Basi, Daudi akamwambia Nathani, “Nimetenda dhambi dhidi ya Mwenyezi-Mungu.” Nathani akamwambia, “Mwenyezi-Mungu amekusamehe dhambi yako, nawe hutakufa. 14Hata hivyo, kwa kuwa kwa tendo lako umemdharau kabisa Mwenyezi-Mungu, mtoto wako atakufa.” 15Kisha Nathani akarudi nyumbani kwake.


Kisa hiki kinatusaidia kuwa yatupasa kutafakari kabla ya kutoa maamuzi. Hivi hao wanaoshangili jambo hili la watoto waliobebshwa mimba kutoruhusiwa kurudi kwenye shule za serikali wametafakati au wanafanya kama alivyofanya Daudi kumbe jambo lilimhusu yeye mwenyewe.
 
Mkuu NGOs zimefanya kazi kubwa ya indoctrination, na hatimaye kubadili mitizamo ya watu.Usi down play their contribution,it's huge.
NImesema tatizo ni primitive thinking. Fikra za mwaka 1430 katika karne ya 21...
 
NImesema tatizo ni primitive thinking. Fikra za mwaka 1430 katika karne ya 21...
Huja address point,umeingia na povu tu.Hata hivyo haisaidii,the decision has already been made. Vi-NGO uchwara haviwezi kutuyumbisha,ni lazima tuheshimu culture yetu na morals zetu.
 
Huja address point,umeingia na povu tu.Hata hivyo haisaidii,the decision has already been made. Vi-NGO uchwara haviwezi kutuyumbisha,ni lazima tuheshimu culture yetu na morals zetu.
I choose not to address anything with you. Mawazo ya karne ya 4 na yale ya karne ya 21 haviwezi kutangamana..
 
Masimango hayaishi.
Ndo wajue vya bure vina kero
 
Kama kawaida ya mzee wa visasi, hivi hajui kuna watu wana chukua masters na tayari wana watoto wenye watoto.

Elimu ni haki ya kila mtu, hata kama mtoto wa sekondari kapata mimba haimaanishi hiyo haki yake inapotea, aendelezwe baadaye aje kuokoa mtoto sio kukaa anaongeza idadi ya wajinga wasio na kazi. Midingi yenye phd feki ndo haiwezi kuliona hili. Tz won't be saved by this guy, he's a joke.
Hao wajinga twaweza wameshawaelezea kuwa ndo wanaoiunga mkono SISIEM
 
Nauliza tu je Mwanafunzi wa shule ya msingi matatizo akimpa mimba mwanafunzi mwenzeka je kuna kesi hapo
 
Mwanafunzi wa shule ya msingi ampe mtu mimba???Mkuu ushawaona watoto wa shule ya msingi lakini!!!
 
Obvious kama kampa dawa yake yule aliepewa amrudishie aliempa!!
Hii itasaidia sana maana naona hizo mimba ni kama kifurushi tu watu wanapeana.
 
Nauliza tu je Mwanafunzi wa shule ya msingi matatizo akimpa mimba mwanafunzi mwenzeka je kuna kesi hapo
Je mwanafunzi akimpa mimba Mwalimu wake? 'Tatizo hapa ni maadili katika jamii zetu' inatakiwa tutatue tatizo na siyo kulikimbia
 
Back
Top Bottom