Rais Magufuli: Sitasomesha Wanafunzi waliopata ujauzito, siwezi kusomesha Wazazi

Rais Magufuli: Sitasomesha Wanafunzi waliopata ujauzito, siwezi kusomesha Wazazi

Amesema ushoga basi.
Au kwa lugha ingine dawa yenu inachemka ikiisha wiva mtainywa bila ganzi wala vipimo.
 
Comment za page ya kwanza na kuendelea zinampiga juhudi za rais za kukemea ushoga, Raia wa Tanzania walisha data.... Kama upinzani ndiyo huu wa kutetea mashoga ni bora msajili wa vyama akavifutia usajili vyama vya upinzani vyote....
 
Mmmh, mie watu wa kanda ya ziwa kila wanapotoa mifano ya mbuzi katika mambo haya huwa nafikiria michezo waliyokuwa wakifanya na mbuzi wakiwa bado wadogo....Ni common knowledge.
 
Ukitazama kwa jicho la tatu utagundua NGO'S nyingi sana hapa bongo zinapata support kutoka nje ambazo zina masharti magumu kiasi kwamba endapo watashindwa na misaada inasitishwa, so wao wanaangalia matumbo yao na kufumbia macho athari katika jamii!
 
Habari wanaJF,

Leo akiwahutubia wakazi wa Bagamoyo, Mkoani Pwani. Rais Magufuli amesema hakuna Mwanafunzi aliyebeba ujauzito atakayerudi shule katika utawala wake. Akaongeza kuwa hawezi kufanya kazi ya kusomesha wazazi.

" Inaweza kufika kipindi darasa zima linawatoto, Mwalimu akifundisha wao wanatoka nje kwenda kunyonyesha".

Hata kama ni watoto wangu, yani nikupeleke shule alafu upate mimba nikurudishe? Aende akapate mimba aone kama nitamrudisha.

Mimi nimetoa fedha ili mwanafunzi asome bure, halafu leo mtu apate mimba arudi shule? Ndani ya utawala wangu, haitotokea.

Wakati mwingine ukizikiliza hizo NGOs zitakuwa zinalipeleka taifa pabaya. Ndani ya utawala wangu haitotokea. NEVER.

Hizi NGOs kama zinawapenda sana hao watoto zikafungue shule zao za kusomesha wazazi. Serikali haiwezi kuwasomesha.

Hawa wanaotuletea haya mambo hawatupendi ndugu zangu. Wametuletea dawa za kulevya, wameleta ushoga ambao hata ng'ombe hawana.

Huku kuiga iga tutakuja kuiga mambo ambayo hata hayafai. Wanakuja na misaada ambayo ni mali zetu wametuibia.

Nyie wafugaji mmefuga lakini hamjawahi kuona hata mbuzi au nguruwe amekosea huu mchezo. Lakini wao wanataka Watanzania wakosee.

Wakati huo huo, Rais amesema kuwa anawaomba msichukue maeneo ya Magereza, hata mimi nikifungwa siku moja nipate sehemu ya kulima.

Rais Magufuli ametoa eneo la ekari 65 kwa wananchi lililokuwa na mgogoro kati yao na Jeshi la Magereza.
Hatuna Raisi kwa kweli anasema yeye anauwezo wa kusomesha hata private je wasio na uwezo kuna wazazi kibao wenye uwezo baada ya kufanya makosa watoto wao waliwarudisha shule na hao watoto wakafanya vyema sana watoto wa masikini ndio watakaoliwa kama haelewi hakuna hata senti tano aliyotoa yeye mfukoni mwake kodi zetu ndio zinasomesha watoto asituambie mambo ya kujipa kiki hapa
 
Jamani nani ajui mwanafunzi akianza ngono anakuaje kwa mwl wake sembuse azae kweli tufurahi upuuzi wa kufanya ngono na kuzaa ebu tujiulize kwa makini
 
Mimi ninahangaika kutafuta pesa ili wao wasome bure, malipo yake baada ya kusoma kwa bidii waje kulisaidia taifa badala yake wanatuletea MIMBA
 
Huu Mchezo Hauitaji Asira

Waiter Zungusha Tena [emoji482] [emoji482] [emoji482] [emoji482] [emoji482] [emoji482] [emoji482] [emoji482] [emoji482]
 
Kama kawaida ya mzee wa visasi, hivi hajui kuna watu wana chukua masters na tayari wana watoto wenye watoto.

Elimu ni haki ya kila mtu, hata kama mtoto wa sekondari kapata mimba haimaanishi hiyo haki yake inapotea, aendelezwe baadaye aje kuokoa mtoto sio kukaa anaongeza idadi ya wajinga wasio na kazi. Midingi yenye phd feki ndo haiwezi kuliona hili. Tz won't be saved by this guy, he's a joke.
Umeelewa alichomaanisha au unakurupuka tu ku coment kwa chuki zako?
Utaratibu wa mwanafunzi mwenye masomo kukatihwa masomo ulifutwa lini labda?
 
Kwani kuna tafauti gani kumfundisha mwanafunzi mzazi na mwanafunzi wakawaida?
Kwani kuna tatizo gani mwanafunzi mzazi kumuomba mwalimu ruksa kwenda kumyonyesha mtoto wake? au serikali itapungukiwa nanini katika mpango wake wa elimu bure? Je hao wanafunzi wazazi ikiwa niwazuri kwa masomo ya sayansi nahesabu, watakapo fukuzwa lengo la taifa kufanikisha kupata mainjinyia, madokta na wahasibu ambae ni wachache litafanikiwa? Mbona ulaya na marekani mambo hayapo hivyo?
 
Hii ndio Roho mbaya! Kwani wakipata elimu baada ya kujifungua kuna tatizo gani? Kwa hiyo Rais anataka kutuambia MTU akipata ujauzito basi hana future tena Au elimu yake inakuwa haramu?
 
our no 1,leo amegusia topic muhimu mno ambaye yeye kama kawaida kaiweka kimihemko,please wana JF tujaribu kuidadisi hapa,ni kweli kila mzazi anapenda mtoto wake aelimike shuleni,mtoto wa kike inapotokea anapata mimba why anaathibiwa yeye tu,maana anafukuzwa shule hadi yule wa kiume aliyempa mimba anaachiwa aendelee na masomo,kwangu huu ni utaratibu dume na unaendeleza ukandamizaji wa watoto wa kike,halafu baadaye tunakuja kupiga kelele ohooo mbona hatuna wasomi wengi wa kike,kumbe wengi wao wameathiriwa na mfumo dume,solutions watoto wa kike waruhusiwe kuendelea na shule baada ya kuzaa,iandaliwe kampeni nchi nzima ili watoto wa kike wanaopenda wapigwa sindano za kuzuia mimba,na hizi zinatofautiana kutoka mwezi mmoja hadi miezi sita,ila ni lazima kila mmoja kupimwa maana zina side effects kutegemeana na mhusika,condoms zigawiwe bure mashuleni na iandamane na elimu nzuri how to use it safely,its time noe tabia hii ya kuwafukuza shule only girls ife maana ni ya kibaguzi.

Kwanza watoto wa kike wanaopewa mimba na wanafunzi wenzao ni wachache mno, wengi wanapewa na watu wa mtaani

Hivi shule gani hiyo ambayo mvulana akimpa mimba mwanafunzi mwenzake anaendelea na masomo? Au umemaanisha nini kusema anaachwa aendelee na masomo?
 
Back
Top Bottom