Rais Magufuli: Sitasomesha Wanafunzi waliopata ujauzito, siwezi kusomesha Wazazi

Rais Magufuli: Sitasomesha Wanafunzi waliopata ujauzito, siwezi kusomesha Wazazi

tujifunze na sisi kuwa na mambo yetu, na viwango vyetu vya maadili ambavyo tunavisimamia.
NGO na wafadhili wake ambao wengi ni wazungu wasilazimishe kuleta mambo ambayo sisi hatujaona maana yake.
Sawa kabisa...

Nipo pamoja na Rais kwa hili...
 
Ukisoma maoni ya watu wengi humu kuhusu mada hii utapata picha halisi ya kwanini maadili yanazidi kuporomoka hapa nchini! Wengi sana wanamkosoa Rais kwa kauli yake. Mimi nashauri kabla ya kusema tunayosema tujiulize maswali yafuatayo;
1.Binti huyo anakuwa na umri gani awapo shule ya msingi au sekondari!? Kama mzazi, unafurahia binti yako akuletee mjukuu katika umri huo!?
2. Ni kabila gani hapa Tanzania linawalea na kuwafundisha watoto wao kuwa tendo la ndoa linafanywa na yeyeto katika muda wowote hata kabla ya ndoa!?
3. Ni dini gani au dhehebu gani linafundisha watu wake kuanza ngono kabla ya kuolewa/kuoa!?
4. Hivi, unafikiri kiongozi kama Rais au Waziri au Bunge likisimama hadharani na kutangaza rasmi kuwa watakao pata mimba RUKSA kurudi shuleni, nini kitatokea kwa wanafunzi kimaadili!? Kutakuwa na Room tena kwa walimu na wazazi kuwaonya wanafunzi kuhusu swala zima la ngono kabla ya wakati!?
5. Vipi kuhusu mwanafunzi mwenyewe kisaikolojia na wenzake darasani? Na mwisho kabisa, unadhani wanafunzi wakiruhusiwa kufanya hivyo, likizo ya uzazi watapewa mimba ikiwa na miezi mingapi na atarudi kuendelea na masomo mtoto akiwa na umri gani na watakuwa na uwezo (maana lazima idadi itaongezeka) wa kumudu majukumu yote mawili kusoma na kulea!?
 
What happened to the mantra that " if you educate a girl you educate a family (nation)."

watakwambia hiyo ya kizamani,lol

kwa nchi km yetu ambayo bado inakua,to go forward is by educating,more and more people as possible,waliozaa shuleni,adults ambao hawakupata nafasi ya kusoma,disabled etc .serikali must invest on its people,sijui kwa sababu haina hela ndio inaona responsibility nyingine ni mzigo??? mweee
 
Kama kweli kasema hivyo basi kapotoka sana na sikubaliani naye kabisa.

Mwanafunzi wa kike kupata ujauzito siyo kosa kubwa hivyo hadi anyimwe fursa ya kujiendeleza kielimu.

Hapo adhabu haiendani kabisa na kosa!

Inapotokea mwanafunzi wa kike akabakwa kwa nguvu na akapata ujauzito, halafu unamwadhibu kuwa hakuna tena kurudi shule haoni huo utakuwa ni uonevu wa hali ya juu?? Adhabu ya Kosa la mimba lishughulikiwe kulingana na mazingira yaliyotokea wakti wa kupahuo ujauzito!!! Sidhani wanaotetea wanatetea msichana kaolewa kapata mtoto halafu anarudi darasani tena. Lakini pia serikali ya A4 iliwahi kuanzisha mpango wa MEMKWA(Mpango wa Elimu ya Msingi kwa Walioikosa) katika umri fulani whether ni mimba au kunyimwa fursa hiyo. Itasaidia kuliko kuona Rais anafoka na vitisho tu bila kutoa mwelekeo wa kutatua tatizo!!
 
Universal declaration of human rights:

Article 26.
(1) Everyone has the right to education. Education shall be free, at least in the elementary and fundamental stages. Elementary education shall be compulsory. Technical and professional education shall be made generally available and higher education shall be equally accessible to all on the basis of merit.

(2) Education shall be directed to the full development of the human personality and to the strengthening of respect for human rights and fundamental freedoms. It shall promote understanding, tolerance and friendship among all nations, racial or religious groups, and shall further the activities of the United Nations for the maintenance of peace.

(3) Parents have a prior right to choose the kind of education that shall be given to their children.

Article 27.
(1) Everyone has the right freely to participate in the cultural life of the community, to enjoy the arts and to share in scientific advancement and its benefits.

(2) Everyone has the right to the protection of the moral and material interests resulting from any scientific, literary or artistic production of which he is the author.

Article 28.
Everyone is entitled to a social and international order in which the rights and freedoms set forth in this Declaration can be fully realized.

Article 29.
(1) Everyone has duties to the community in which alone the free and full development of his personality is possible.

(2) In the exercise of his rights and freedoms, everyone shall be subject only to such limitations as are determined by law solely for the purpose of securing due recognition and respect for the rights and freedoms of others and of meeting the just requirements of morality, public order and the general welfare in a democratic society.

(3) These rights and freedoms may in no case be exercised contrary to the purposes and principles of the United Nations.

Article 30.
Nothing in this Declaration may be interpreted as implying for any State, group or person any right to engage in any activity or to perform any act aimed at the destruction of any of the rights and freedoms set forth herein.
MTU ambae anashindwa kufikiri au kufanya maamuzi kwa kusaidiwa na hizi madocuments huwa ananiboa sana,kama wewe unaetujazia saver za jf bure ...


We have our culture ,laws and manners, kwanini usichambue mambo ya nchi yako kwa kuzingatia hayo??? ...


Kwani hiyo universal declaration can't be challenged ??? .... Hata Kanisa La Anglican lilitokana kwa watu kuhoji ....


Hebu tuzungumzie hili kwa level ya nchi yetu
 
Tunatunza hayo maneno kuwa maeneo ya magereza yasichukuliwe ili siku mojanmae akikamatwa apate eneo la kulima

Haya sasa kwa hiyo wwnaobeba mimba waende private wakasome,aisee waliompa kura huyu baba wanafanana akili na magu
 
Good ..! Kuwarudisha darasani ni kupalilia haka ka mchezo.

Naunga mkono hoja!

hata msipowarudisha shuleni,hamjakata mzizi,

wasichana na wavulana at that age,wanajifunza kuexperiment mambo mengi yanayotokea/kubadilika na baiolojia zao,

hio ni nature,

hata nchi zilizoendelea kabisa,tatizo la mimba shuleni ni la kawaida.
 
Namuunga mkono Rais %100. Wazazi wameacha malezi bora ya watoto wanatetea Uasherati! Vijana wanaendekeza Ngono zembe licha ya mafunzo yote wanayopewa.
Malezi bora hapo unazungumzia maadili katika jamii. Kama ndivyo, itabidi uanze kujiuliza hivi: Hawa wanasiasa wetu wanaotaka mabinti zetu wasiendelee na masomo wakiishapewa ujauzito wao wana maadili kiasi gani?, wao si miongoni wa wale wanaowapa ujauzito mabinti zetu? Ni kundi gani katika jamii lina maadili? Wachungaji, waalimu au mashekhe?

Mkuu suala hili haliitaji nguvu linahitaji sana common sense! Ukienda pale wizara ya elimu takwimu za idadi ya wanafunzi wanaopewa ujauzito wakiwa shuleni zinatisha. Na ujue zinatisha wakati sheria hii ipo na inatekelezwa. Tafsiri yake ni kwamba, sheria wala haijawa msaada ambao ulitarajiwa. Lakini kubwa ni kwamba sheria yenyewe imetumika kuongeza idadi ya wajinga nchini, maana wazazi hawa wanaozuiwa kuendelea na masomo sio rahisi sana kujikwamua kimaisha na hivyo kuna uwezekano mkubwa kuwa hata hao watoto wanaowazaa wanashindwa kupata elimu na kubaki kuwa wajinga.

Tusifikir kwamba kila unaponyosha kitu kinaweza kunyoka, wakati mwingine kinachonyoshwa huvunjika. Tunakoelekea kuna hatari ya Tanzania kuvunjika badala ya kunyoshwa!
 
Huo ujinga wake aupeleke Chato lakini sio kutulazimisha watanzania wote tukubali.
Watoto wa kike hupata mimba kwa sababu mbalimbali ikiwemo Kubakwa, kutishwa, Kulaghaiwa, umaskini nk.

Kumnyima Elimu kisa tu amezaa ni sawa na kumuangamiza yeye na kizazi chake chote.
 
kwa hiyo amechagua ujinga.. tafuta wapiga kura mzee.. ukiwasomesha imekula kwa ccm
Wala, mbona toka zamani hili swala lililkuwepo?! Anachomaanisha, msichana akipata mimba lazima aache shule, atajiendeleza kivyake, either as a private candidate au kupitia Vocational Training, au hata ujasiriamali au kilimo, ila akizaa kurudi shule haipo, hata kwenye nchi zilizoendelea, hakuna upuuzi na uzuzu huo, ila kama hamjamuelewa basi nyie ndio mwataka kukaribisha uzuzu mashuleni...
 
Wanaouza madawa ya kutolea mimba.....wataikusanya mipesa safari hii
 
Contradiction.. Kama mwanafunzi wa kike ambae hajafikisha miaka 18, sheria inamtambua ni mtoto na hivyo mwanaume anaefanya nae mapenzi anachukuliwa kama amembaka, iweje sasa huyo anaetambuliwa kama mtoto na hana akili ya kuchambua maamuzi anayoyafanya na consequences zake leo aje kupewa adhabu kubwa simply tu kwa maamuzi (ambayo sheria inatambua ni ya kitoto), au kuiweka kisheria zaidi kwa kubakwa..?

Tumelogwa..
 
Kama kweli kasema hivyo basi kapotoka sana na sikubaliani naye kabisa.

Mwanafunzi wa kike kupata ujauzito siyo kosa kubwa hivyo hadi anyimwe fursa ya kujiendeleza kielimu.

Hapo adhabu haiendani kabisa na kosa!

aliyempa mimba na wazazi wake wamsomeshe private
 
Back
Top Bottom