Rais Magufuli: Sitasomesha Wanafunzi waliopata ujauzito, siwezi kusomesha Wazazi

Rais Magufuli: Sitasomesha Wanafunzi waliopata ujauzito, siwezi kusomesha Wazazi

Contradiction.. Kama mwanafunzi wa kike ambae hajafikisha miaka 18, sheria inamtambua ni mtoto na hivyo mwanaume anaefanya nae mapenzi anachukuliwa kama amembaka, iweje sasa huyo anaetambuliwa kama mtoto na hana akili ya kuchambua maamuzi anayoyafanya na consequences zake leo aje kupewa adhabu kubwa simply tu kwa maamuzi (ambayo sheria inatambua ni ya kitoto), au kuiweka kisheria zaidi kwa kubakwa..?

Tumelogwa..

mpe mimba ndio mjadala utakuwa mzuri zaidi
 
Tuwafundishe vijana wetu maadili mema, mimba nyingi za wanafunzi ni zakujitakia tu!

Leo visichana vidogo vya miaka 15 vimeshaharibika kabisa havina tofauti na vizee.. Tukiwafunza maadili mema hawatafanya hayo!
 
Atakayefanya kama alivyosema RAIS atakuwa MZAZI mpumbavu.Kuna shule za private,kama anauwezo ampeleke mtoto wake private.

Huu ujinga ati mtoto sababu amepata Mimba asisome aupeleke Lumumba na Chato

ndio ana maana hiyo!!

kamsomeshe kwa hela zako.period
 
Simpendi Magufuli,siipendi ccm,lkn ktk hili namuunga mguu kwa 100%. Kwanza ukiruhusu hilo na wasichana wanavyopenda kuvua nguo za ndani kipindi hiki,kweli unaweza kukuta Darasa zima wasichana wamezaa!

Ili kuweka nidhamu ni lazima kuzuia hili. Huu ndo mfumo wetu wa tangu zamani. Suala la kubakwa pia mazingira wanayatengeneza wenyewe.

Unaenda kujisomea kwenye chumba cha kijana tena mkiwa wawili tu au wavulana wawili msichana upo peke yako na umevaa sindiria ya kupiga jeki manyonyo,sketi nayo fupi kwa nn usiliwe!!?? Magu kanyaga twende Baba hakuna kusomesha wazazi....!!
 
Tuwafundishe watoto kutumia majira, ili wasipate mimba zisizotarajiwa.
Majira ni mbaya sana usizuie ujauzito wakati hujui kizazichako kipovip...anaeruhusiwa kutumia ni yule aliezaa tu.
 
Kama Taifa ni lazima tuwe na msimamo. Anae ona kuzaa ni kuzuri akazae ! Waadilifu wasome. Kwa mara ya kwanza tumekubaliana!
 
BADO MIAKA MITATU, KWELI TUTASIKIA MENGI, NA YULE MWINGINE ALISEMA NI VIHEREHERE VYAO.
 
Mkuu Malizia yote pia amesema watakaowapa mimba wanafunzi miaka therathini jela, mimi namuunga mkono kwa sababu nina watoto wengi wa kike
Kuna msichana yoyote aliyemaliza sekondari akiwa bado bikira?tatizo hili ni sugu hapa nchini na sidhani kama litaisha
 
Kuna binti alipata ujauzito akiwa form 2 miaka ya nyuma kidogo.. akajifungua salama mtoto akawa mwaka moja kasoro wazazi wake wakapambana akarudi shule.. leo hii ni Mwalimu mshahara analipwa na anawasaidia watu wengine wakiwemo wazazi wake na serikali inakata kodi kama kawaida

Magu kwa upande wa vision hamna kabisa anajenga taifa la omba omba

magu anasema kumsomesha kwa hela za serikali!! watanzania hamuelewi na ndio maana mnaibiwa mpaka makinikia
 
mpe mimba ndio mjadala utakuwa mzuri zaidi

Ha ha ha ha.. Kila siku wanapewa mimba.. wanabakwa na kupewa mimba.. Mie nawajua ni watoto sifanyi nao zinaa.. Miguberi ipo kibao huko iliyokubuhu, na mafundi pia..
 
Huyu jamaa aandikiwe hotuba, kumnyima mtu elimu ni kumkatalia haki yake ya kibinadamu yale maazimio tuliyosaini yatawabana watakaotekeleza huu ujinga.

Juzi kawaponza trafiki wawili.
Na kumpa mimba Je?
[HASHTAG]#NamuungaMkonoRais[/HASHTAG]
 
mi na huyu mheshimiwa tunapishana kwenye namna anavyofikisha ujumbe wake tu basi;...kwanini inakuwa katika mtindo wa mipasho sana?!!!!! na kwanini anawaita watu wanaotusaidia wezi? wamemuibia nini na kwanini asiwakamate?
Maneno yako sahihi mkuu......ikiletwa misaada wanafurahia kichizi
 
Lakini waziri si alisema ruksa ? Au ndo mkuu kashapigilia msumari
 
Sasa picha ndio linaanza.
Mkuu keshasema na alishatamka kwamba hapangiwi na mtu.

But my take mheshimiwa sana rais wetu nadhani inatakiwa awe na akiba japo kidogo ya maneno because alwayz what goes around comes around too that thats the law of karma.

Kuna mazingira mengine ya upatikanaji mimba ambayo unaweza kumhukumu bure kabisa mtoto wa kike i.e ubakaji
 
Back
Top Bottom